Pamoja na mifano yako ya majina ya kikristo, bado azam wana udini sana. Sio kwenye tv tu, hata biashara zake nyingine. Bakhresa anaingiza imani yake kwenye biashara ambazo wateja wake sio wa din yake tu.
Ningemwelewa angeomba leseni ya kufungua biashara zinazofuata misingi ya dini ya kiislamu. Mwanzoni mimi nilikuwa shabiki mkubwa wa azamfc. Nimeachana nayo kwa sababu ya elements za udini katika uendeshaji wake.
Kitu rahisi ambacho angeweza kufanya ni kuruhusu, kwa mfano ibada za kikristu siku ya jumapili kwa muda mfupi tu. Halafu akaweka sala/ibada ya ijumaa hata siku nzima ya ijumaa.
Kidogo sasa inapokuwa pasaka au krismasi unaona matangazo yenye ladha ya ukristu. Lakini mwanzo, hakuonyesha chochote katika siku hizo muhimu kwa wakristo. Ni muhimu huyu mzee akaangalia hisia za wateja wake kwa ujumla.
Ushauri wa bure tu.