Azam decoder chaneli nyingi zisizo na maana

BoManganese

JF-Expert Member
Jun 10, 2017
979
2,671
Habari wanaJF.

Ni imani yangu kubwa pia humu wamo watumiaji wa king'amuzi cha Azam sasa kitu kilicho nipelekea kufungua uzi huu ni ile kero kwenye king'amuzi hicho kuwa na chaneli nyingi zisizo na mantiki unakuta kuna chaneli kibao zimejazana sijui za malawi, Burundi, Rwanda n.k nasema hazina mantiki kwasababu mara nyingi katika chaneli hizo hata lugha zinazotumiwa hazieleweki sio kiswahili wala kingereza.

Kama king'amuzi cha Azam kinatoa pia huduma zake huko kwenye hizo nchi ni bora wangeweka vifurushi vyao special vyenye chaneli zao kuliko mtu kulipia kifurushi unakuta michaneli mingi imejazana ambayo haieleweki.

Au wadau mnasemaje.
 
Lakini pia Azam wana tatizo kubwa la kuto update chaneli zao baada ya kulipia na hasa ukilipia siku ambazo muda wa kifurushi umeisha. Wawe systematic kama ving'amuzi vingine mbona DSTV hata kama muda umeisha lakini ukilipia hawachelewi kuwasha lakini Azam ni KEEEROOOOO
 
Lakini pia Azam wana tatizo kubwa la kuto update chaneli zao baada ya kulipia na hasa ukilipia siku ambazo muda wa kifurushi umeisha. Wawe systematic kama ving'amuzi vingine mbona DSTV hata kama muda umeisha lakini ukilipia hawachelewi kuwasha lakini Azam ni KEEEROOOOO
Kweli mkuu hii nayo kero nyingine
 
Azam ni waarabu wanataka kutufanya waarabu na sisi machanel ya mashariki ya mbali kibao sijui wanatangaza utamaduni?KWANINI WASIJIUNGE NA ABUDHABI SPORTS ILI TUCHEKI EPL LIVE NA HAO NI WAARABU WENZAO!WANAWEZA JIUNGA NAO TUKAPATA VITU VIZURI ILI DSTV WAACHE KUTUNYANYASA NA BEI ZA HOVYO YA VIFURUSHI!!
 
Hawa jamaa washukuru wanaonyesha ligi kuu labda na La liga kidogo ila wangekimbiwa tu
 
Kama ile channel ya Uganda inayoitwa West, wanazungumza ligha ya asili sijui Kinyankole, Azam wameiweka ya nini? Nyingine sijui ya Comoro nk hazina maana maana hata lugha zao hatuzijui.

Vv
 
Back
Top Bottom