egentle
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 808
- 392
- Thread starter
- #61
Mwaka 1994 wanafunzi wa Tambaza walikuwa wana fujo na tambo za kila aina hivyo hawakupenda kuona mwanafunzi yeyote wa Tambaza anaonewa.Tulikuwa tunatembea kwa vikundi na mwanafunzi yeyote Wa shule ya Azania,Kinondoni Muslims au Jitegemee akituona lazima akimbie.Siku moja alivamiwa mwanafunzi Wa Tambaza na wanafunzi Wa Azania maeneo ya Fire.Hilo lilipelekea Tambaza kutaka kulipiza kisasi na tulifanikiwa kufika ndani ya shule ya Azania wengine tulilazimishwa na wababe Wa shule.Hapo mapambano yalianza kati ya Polisi na wanafunzi Wa Tambaza wakati huo wanafunzi wa Azania wamefungiwa madarasani.Polisi wakirusha mabomu ya machozi Tambaza wanarusha mabomu ya Petroli.Mapambano yaliendelea na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa wakiwemo Polisi.Bahati mbaya au nzuri mwenye kiberiti cha kuwashia mabomu ya petroli alipoteza kiberiti hicho na hilo lilipelekea Tambaza kuzidiwa nguvu.Fujo hizo zilisababisha form one na baadhi ya form two kuhamishiwa katika shule mbalimbali za mikoa ya Tanzania Bara.Waliachwa form three na four wakamalizia miaka yao.Huo ndio ulikuwa mwisho wa O level Tambaza fujo zilizidi mpaka BBC Swahili wakaitaja kama shule ya pili kwa fujo Afrika mashariki na kati.Hakika viongozi wa miaka hiyo enzi ya Mzee Mwinyi walifanya maamuzi ya busara.
Shule ya kwanza ilikuwa.ni.ipi?? Police walikuja kuwatawanya madenti, ila si kweli.kama azaboy walikuw wamezdiwa nguvu,.mazima.
Mliingia hadi shulen mkatega mabomu kwenye Lab zetu. Mtiti ulikolea hapo. Bt tifu lilizimwa na police maana tulikuw tunatiririshan kwa zamu