AY anusurika kifo, aokolewa na polisi, alala sero! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

AY anusurika kifo, aokolewa na polisi, alala sero!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutunga M, Aug 3, 2009.

 1. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2009
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Wakuu
  mwanamuzi Ambwene Yesaya (AY) usiku wa kuamkia jana alinusurika kifo kufuatia mashabiki kuvamia katika guest alikokuwa amefikia katika wilaya ya karagwe mkoani kagera wakishinikza kurudishiwa fedha zao walizotozwa kama kiingilio na kisha kutoonekana ukumbini.

  Full tukio ni hivi.
  AY aliletwa na mwanamama Dina ili ashiriki katika onesho la mavazi liloandaliwa na kampuni ya Dina Fashion ya jijini Dar na alitakiwa kufanya maonesho mawili katika miji ya Bukoba na Karagwe kwa malipo ambayo hayajajulikana.

  Hata hivyo inadaiwa kuwa baada ya kufanya onesho pale ukumbi la Linas Club Mjini Bukoba alilipwa ujira nusu na kuahidiwa kuwa angelipwa fedha zilizosalia baada ya kufika Karagwe lakini waandaaji walishindwa kufanya hivyo.

  Kutokana na hilo AY aligoma kutoka hoteli alikokuwa amefikia ili aende kupanda jukwaani hali iliyowafanya mashabiki kulalama na kuamua kumfuata hotelini hapo na kwa lengo la kumdhuru kabla ya kukolewa na polisi.

  Baada ya hapo, polisi walimchukua AY, waandaaji na baadhi ya washiriki wa mavazi waliokuwa wametoka Bukoba na kuwasweka LUPANGO katika kituo cha Polisi Karagwe ambapo walilala hadi jana asubuhi.

  Taarifa za hivi punde ni kuwa AY na waandaaji wa shindano hilo ameachiwa baada ya kuelewana lakini mashabiki WAMETAPELIWA.

  SASA SIJUI ALAUMIWE, AY, DINA FASHION AU MASHABIKI ? Kazi kwenu
   
 2. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  kwa nini polisi wamekuwa involved? hili swala ni la private law...breach of a contract. Polisi wangetakiwa kuchapa mashabiki bakora kisha wawaachia Ay na hao wa DIna wenyewe wamalizane.
   
 3. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #3
  Aug 3, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Rutunga bwan aasa alaumiwe AY kwa lipi? yeye yuko kazini na anafanya kazi kwa kufuata taratibu, waandaaji wamekiuka then imekula kwao
   
 4. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  kutaka hela ya dhuluma ndo hapo,ujinga mtupu kwa hawa watu wa aina hii, wapo wengi sana tz hii, sasa kuuziana mbuzi ktk gunia nani alaumiwe? pia may be AY angefanya ustaarabu yeye km staa apande jukwaani awaeleze mashabiki upuuzi huo then wao waamue!kama kumpiga au kumhurumia!!
   
 5. Sasha Fierce

  Sasha Fierce JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 362
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hao ndiyo ma-super star wetu wa kibongo.yeye kama amedhulumiwa angetakiwa kuhitokeza mbele ya wapenzi wake na kueleza issue nzima ila kujidai kuzira na kubakia hotelini yaani the whole thing hai-make sense kabisa.Wanatakiwa ku-thamini fans zao na siyo pesa mbele,fans ndiyo watakao kumake or destroy you inabidi kujipendekeza sana kwao hata kama huwa-mind.
   
 6. Van Walter

  Van Walter Senior Member

  #6
  Aug 3, 2009
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 171
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Dina ndo wakulaumiwa hapo...kile kidada kifanye mambo zake za utangazaji..huku kwe mziki na matamasha hawezi.atafungwa kwa tabia hizo.
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huyu Dina ni yupi jamani wa clouds au yupi?
   
 8. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kitendo cha washabiki kumfuata hoteli kwa makusudi ya mkudhuru ni uvunjifu wa amani( a sort of mob justice) kitu ambacho ni kosa na polisi walichofanya ni sahihi kuzuia hali hiyo isitokee, kuwaweka ndani wahusika ni kwa usalama wao kutoka kwa wananchi waliokuwa tayari kuchukua sheria mikononi mwao.
   
 9. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  jamani huyu ni Dina yupi? wa clouds FM au mwingine?
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Aug 3, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mh.... hapa ntamtetea AY; yaani ajitokeze akazidi kuchafua hewa??? alifanya jambo sawa na waliomfuata hotelini kwake ni wahalifu wanastahili kuchukuliwa hatua. AY hakuwa na makubaliano yoyote na washabiki, bali washabiki walikuwa na makubaliano na muandaaji wa onesho.... he is a victim

  Na hayo si kwa mastaa wa bongo pekee, hata wa majuu hukatisha shoo/tours kama mikataba yao haijafuatwa ipasavyo

  Duh...
   
 11. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #11
  Aug 3, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  inawezekana kwa usalama wa AY na Dina kama ilifikia kuwafata hotelini huoni wangeweza kuumizwa...
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Aug 3, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Hivi AY hana walinzi..?
   
 13. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #13
  Aug 3, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mkuu, naona utani wako uko juu sana.

  BTW. Koffi Olomide alipanda jukwaani na akagoma kuimba. Chupa zilirushwa na hadi anakuja kueleza na kueleweka, alilowana. A Y alifanya la maana kutokufika pale.
   
 14. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #14
  Aug 3, 2009
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Hali kama hii pia ilishawahi kumsababishia matatizo Mr Nice kule Mkoani Lindi. Promota alikiuka mkataba waliokubaliana na Mr. Nice, hivyo msanii akagoma kupanda jukwaani. Matokeo yake Mr Nice aliokolewa na polisi, lkn ninachokumbuka nui kwamba mashabiki waliondoka na viti ukumbini, kama kipoozeo cha hasira zao!

  promotaz wasipobadilika, there is more worse situstion to come!
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Aug 3, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Inafaa AT awashitaki polisi kwa kumzuia bila sababu, kumuweka rumande wakati hana kosa
   
 16. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #16
  Aug 4, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mh, nilipopata tatizo la kuelewa ni hapa:
  "Baada ya hapo, polisi walimchukua AY, waandaaji na baadhi ya washiriki wa mavazi waliokuwa wametoka Bukoba na kuwasweka LUPANGO katika kituo cha Polisi Karagwe ambapo walilala hadi jana asubuhi.

  Taarifa za hivi punde ni kuwa AY na waandaaji wa shindano hilo ameachiwa baada ya kuelewana lakini mashabiki WAMETAPELIWA."

  Inaonyesha Polisi waliwashika mpaka walipoelewana? Mimi sina tatizo na wao kuwalinda raia kuzuia 'mob justice' lakini sio kazi yao ku-solve private issues.
   
 17. Bazobonankira

  Bazobonankira Senior Member

  #17
  Aug 4, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuna mdau kauliza, Dina Fashion ni Dina wa Clouds FM. Inawezekana anahusishwa kwa kuwa na yeye nanatokea Kagera.

  Mtoa taarifa fafanua tafadhali
   
 18. Wa mmoja

  Wa mmoja Member

  #18
  Aug 4, 2009
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  AY,hawezi kulaumiwa kwa sababu yeye hakuingia mkataba na mashabiki,mkataba wake unamuhusu yeye na huyo Dina..So Dina ndo wa kumlaumu kwa kutokukamilisha malipo ya watu...AY yupo kazini so Dina inabidi aheshimu kazi ya mwenzake kama anavyoheshimu ya kwake...
   
 19. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #19
  Aug 4, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Walimweka sehemu yenye usalama.
  Angeumiliwa mingeu mngekuja tena Polisi kazi yao nini si kulinda raia? Yeah walimweka mahala penye usalama zaidi ili kuokoa maisha yake.
   
 20. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #20
  Aug 4, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  kaka navyomfahamu AY anao walinzi ila ndio hawa walinzi wetu wa mitaani "mabaunsa" wawili....

  SWALI SASA....kwa walinzi hao "mabaunsa" tena wasiokuwa hata na silaha yoyote ile unadhani wangefanya nini kupambana na wananchi zaidi ya 1000 wenye "hasira kali" na possibly silaha za jadi kama visu, chupa na hata mapanga...na inawezekana kabisa washabiki wengine walikuwa wametokea nchi jirani na kagera hasa zile zilizowahi kupitia machafuko ya kivita....tafakari...CHUKUA HATUAAA....ni maoni tuu
   
Loading...