Avunjika mguu akicheza kwenye mvua uchi usiku.

Mfanyakazi mwenzangu amevunjika mguu alipokuwa akicheza uchi kwenye mvua.

Kisa hiki cha ajabu kimetokea nyumbani kwake Kimara B, usiku wa kuamkia leo mvua ilipokuwa ikinyesha.

Jamaa huwa anapenda sana kucheza cheza kwenye mvua, alimtoroka mke wake kitandani, kisha akatoka nje na kuanza kukimbia huku na huko huku akiwa uchi wa mnyama.

Ikatokea bahati mbaya akateleza na kuanguka anguko lililopelekea mguu kuvunjika.

Jamaa akajiburuza hadi kwenye tiles ndipo akaanza kumuita mke wake. Mke wake alipofika akakuta mume wake yuko uchi na amevunjika mguu.


Mke akaingia ndani, akachukua tracksuit na kumvalisha ndipo wakanipigia simu kuomba msaada wa gari, sababu mimi ninaendesha Alphard la ofisini.

Nilipofika nikaona mguu umevunjika vibaya nikashauri tuite ambulance ili tusije sababisha madhara zaidi.

Ambulance ikaja, tukampeleka jamaa Muhimbili kitengo cha mifupa Moi ambako amelazwa huko akisubiri upasuaji kwani amevunjika vipande vitatu.

Jamaa anasema tukio hili lina mkono wa mtu, kwani ana shamba Vikindu, jirani yake alimega kipande cha shamba hilo. Wamehangaishana kwenye baraza la ardhi la kata, jamaa yangu akashinda. Yule jirani yake akamwambia lazima amfanye kitu mbaya
Lengo la uzi ni kutueleza unaendesha alphard la ofisi,, pumbav
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom