AVN number ilivyokatisha ndoto zangu

AVN number ilivyokatisha ndoto zangu

Habari ,

Ninasikitika kusema kuwa jambo ambalo laonekana kuwa dogo, hilolohilo limekatisha ndoto za vijana wengi nchini Tanzania, nimefanya application ya mkopo ili niendelee na chuo kikuu, nimesoma kozi ya technical education in electrical engineering.

Lakini baada ya kufuatilia avn kila kitu kiligonga mwamba,, kwa kifupi kozi yetu haipo kwenye database ya NACTE.

Pamoja na kwamba nimesoma chuo cha serikali, na nimefanya mtihani wa baraza, NECTA.

Hivyo basi naomba kama kuna wahusika katika mamlaka hizo mbili (nacte & necta), wafanye kazi yao kwa weledi mkubwa, kama hawawezi basi hizo mamlaka hazifai kuwepo, wabuni mbinu nyingine yenye ufanisi mkubwa.

Nimeumia kiasi cha kufa kwa kupoteza gharama zangu nyingi bila mafanikio[emoji33][emoji33][emoji33]
kupata avn kuna taarfa unazijaza kwa usahihi......endapo usipojaza kwa usahihi avn huwez pata hapo ndo unapoambiwa hutambulikiii......chuo kama kreluu hakiwezi endesha koziii ambayo haitambulikiii its imposiiblee brow....kua maqn kwenye ujazajii wa taarfaa
 
Kila Jambo linawakatu wake Mimi mwenye mwka juzi nilikosa kila kitu kisa avn nilipoteza hela nyingi sna
Lakini mwaka unaokuja nikipata kila kitu nacho mshukul mungu
Kwaio bro wait mwakana uombe Tena
Pole sana kwa yaliyokukuta naomba namba yako ya kidato cha nne na mwaka uliomaliza nikusaidie kujua nini tatizo na soln yake by kesho
Am still waiting tuone hicho unachokisema usahihi wake upo wapi bwana ndosh
Inaelekea kuna tatizo mahali fulani, haiwezekani kila mwaka watu wanalia kitu hicho hicho. Kusuburu mwaka ni gharama kubwa ambayo unaweza usiione na una uhakika gani mwakani utafanikiwa?
Mkuu Murugu nimekusoma na inaelekea una nafasi nzuri ya kujua kinacho endelea. Ni vizuri kumsaidia Mkuu Ndosh kama ulivyo mueleza. Lakini mimi ningetaka kujua hawa NACTE wanalionaje jambo hili? Je hakuna njia ya kurekebisha mapungufu yaliyopo. Kwa mfano waka jana nilikutana na kijana anamaliza diploma yake lakini alikuwa field wakati dirisha la udahili lina yoyoma. Aliniambia ataomba chuo mwakani (mwaka huu) hivyo mwaka mzima ameupoteza. Na wako wengi wa aina hiyo. Je NACTE wanafanya nini kurekebisha hili ili admission cycle yao iende sambamba na vyuo. Vyuo vibanwe na kuleta matokeo in time. Au labda kuna njia nyingine. Ahsante
 
ndugu sema umesoma chuo gani jieleze vizuri usaidiwe maana vyuo ambavyo vipo chini ya NACTE Hawafanyi mtihani wa baraza, kama vile kozi za afya huwa hazipo chini ya NACTE , jambo la pili ukiwa kama mwanafunzi inabidi kutazama mwanzoni kabisa kama chuo unachosoma kipo sahihi na kinatambulika, jambo la mwisho elewa sio kila diploma inatambulika na NACTE kuna baadhi ya diploma kama zinazotolewa UDSM na UDOM hazipo chini ya NACTE
AVN haijalishi umesoma wapi, kama una diploma na unataka kwenda chuo kikuu/degree program hapa Tanzania lazima upate AVN namba. Mfano umemaliza Udom na una diploma yao-lazima upate hiyo NVN namba vinginevyo imekula kwako.
 
Suluhisho, Ni kuweka kozi katika mifumo husika, na wawe updated, kuwe na link nzuri kati ya NECTA & NACTE.
 
AVN haijalishi umesoma wapi, kama una diploma na unataka kwenda chuo kikuu/degree program hapa Tanzania lazima upate AVN namba. Mfano umemaliza Udom na una diploma yao-lazima upate hiyo NVN namba vinginevyo imekula kwako.
Mkuu umeeleza Safi sana ila Ningependa unieleweshe kidogo kuhusu hili Kuna baadhi ya vyuo mfano vyuo vya Afya huwa wanaDiploma ambazo Kimsingi wao wanakuwa chini ya TCU na sio NACTE hapo unaweza kweli kuipata hiyo AVN!?
 
Unapata AVN baada ya chuo husija kupeleka matokeo yako yote ya semester zote pamoja na semester ya mwisho na wao kuhakiki kwamba hauna supp na kwamba umefaulu kozi husika , tatizo linakuja kuna vyuo makusudi wanachelewa kupeleka matokeo NACTE kipindi mimi nafuatilia AVN ilibidi niwapigie NACTE wakaniambie wala usisumbuke nenda chuoni kwenu kawaambie watume matokeo kwetu, sisi hatuwezi kuwaambia sababu wao wanajua jukumu hilo
 
Mimi Wala siwezi kutuhumu chuo, Ni uzembe wa baraza la mtihani,NECTA, maana nifanya mtihani wa NECTA!!!!! sijasoma kwa semesters!!!
 
Mkuu umeeleza Safi sana ila Ningependa unieleweshe kidogo kuhusu hili Kuna baadhi ya vyuo mfano vyuo vya Afya huwa wanaDiploma ambazo Kimsingi wao wanakuwa chini ya TCU na sio NACTE hapo unaweza kweli kuipata hiyo AVN!?
Mkuu hapo juu nilitoa mfano wa diploma za Udom ambazo ziko chini ya TCU na wao lazima wanafunzi wao wakitaka degree waende NACTE wapate AVN. Kwa muktadha huo naamini hata hao wanaotoa diploma za afya lazima muombaji apate AVN. Hata waliosoma nje walika na diploma zao inabidi wapite NACTE kwani bila AVN huwezi kudahiliwa chuo chochote nchi hii.
 
Unapata AVN baada ya chuo husija kupeleka matokeo yako yote ya semester zote pamoja na semester ya mwisho na wao kuhakiki kwamba hauna supp na kwamba umefaulu kozi husika , tatizo linakuja kuna vyuo makusudi wanachelewa kupeleka matokeo NACTE kipindi mimi nafuatilia AVN ilibidi niwapigie NACTE wakaniambie wala usisumbuke nenda chuoni kwenu kawaambie watume matokeo kwetu, sisi hatuwezi kuwaambia sababu wao wanajua jukumu hilo
Naona NACTE hapa wanakwepa kuwajibika kuna vyuo viko chini yao moja kwa moja hivi wangeweza kuvidhibiti. Na chuo chochote kinachochelewesha kupeleka matokeo wangeweza kutoa adhabu husika. Si vyema vijana kuteseka halafu mtu anasema hawana madaraka. Wangehakikisha vyuo vyote vinafuata agreed admission cycle kwa kupanga mihula vizuri na timetable za vyuo viendane na hiyo admission cycle. Hivi inaeleweka kwa nini kijana apoteze mwaka mzima kwa kosa ambalo sio lake halafu wahusika wanatupiana mpira?
 
🤝
 
Habari ,

Ninasikitika kusema kuwa jambo ambalo laonekana kuwa dogo, hilolohilo limekatisha ndoto za vijana wengi nchini Tanzania, nimefanya application ya mkopo ili niendelee na chuo kikuu, nimesoma kozi ya technical education in electrical engineering.

Lakini baada ya kufuatilia avn kila kitu kiligonga mwamba,, kwa kifupi kozi yetu haipo kwenye database ya NACTE.

Pamoja na kwamba nimesoma chuo cha serikali, na nimefanya mtihani wa baraza, NECTA.

Hivyo basi naomba kama kuna wahusika katika mamlaka hizo mbili (nacte & necta), wafanye kazi yao kwa weledi mkubwa, kama hawawezi basi hizo mamlaka hazifai kuwepo, wabuni mbinu nyingine yenye ufanisi mkubwa.

Nimeumia kiasi cha kufa kwa kupoteza gharama zangu nyingi bila mafanikio😱😱😱
usifike hatua ya kutaka kufa ni kufuru...nenda nacte kwwa ushauri
 
Niko mbali Sana na makao makuu Dar, nipo Arusha, siwezi kupoteza pesa kwa kitu ambacho nishapoteza matumaini nacho , ngoja nikae kimya Lakini ole wao nitakapokuwa madarakani[emoji21]
Oooh...! Hiyo sahau
 
Back
Top Bottom