Award Verification Number (AVN) updates

Arch.katunzi

JF-Expert Member
Sep 18, 2014
250
143
Habari zenu waungwana!

Leo 15/09/2020, katika kalenda ya NACTE ya 2020 ilikuwa kuanza kwa zoezi la vyuo kuweka matokeo kwenye mfumo wa data wa NACTE (Uploading Diploma Results to NACTE Database).

Nilijaribu kufatilia kama zoezi limefanyika bila mafanikio. Niliwasiliana na chuo ambako nimesoma, wao wanasema hawana taarifa hiyo.

Sasa kwa yeyote mwenye updates ya suala hili naomba atujuze, ili kujua kinacho endelea. Nimeingia katika website ya NACTE mara kadhaa kuona kama kuna taharifa yoyote, lakini wapo kimya hao jamaa.

Nilijaribu kuwatafuta kupitia zile namba zao zilizo kwenye admission page yao bila mafanikio yoyote.

Kama kuna yeyote mwenye mawasiliano ya NACTE ya moja kwa moja basi aweke hapa ili kuwasiliana nao juu ya jambo hili...!

Kupata AVN limekuwa suala gumu sana kwa upande wangu nisijue kwa wenzangu. Vyuo tunako soma wanatuangusha sana, hawatimizi wajibu wao. Unasoma unamaliza unaanza kuhangaika nao ili wapeleke taharifa zako NACTE, hii siyo sawa sawa.

Wale ambao bado wako vyuoni,hasa vyuo hivi vya elimu ya kati hakikisheni mnafuatilia kama vyuo mnako soma wanapeleka matokeo yenu nacte na yanasomeka katika system.Yasije kuwakuta haya tunayopitia sisi kwa sasa.
 
Yaaah mkuuu, ratiba ya NACTE inaonesha jana wameanza kuruhusu kutuma kwa matokeo hasa ya diploma tena ni ndani ya siku 15 tu.
Ila ukitazama vyuo vingi bado hawajatoa matokeo kwa semester hii ya pili na bado wapowapo tu hata hawasomeki wajinga hawa yaan wanaboa sana sijui wanachajiwa kiasi gani cha pesa mpaka wanachelewesha kutuma matokeo.

Ili kuondoa hii adha NACTE inabidi waanzishe sheria ya kupiga fine kwavyuo vinavyochelewesha kutuma matokeo
 
Nenda pale Nacte system zao bado mbovu ukienda ofisini wanaku update then wanakutumia control number unalipia wanakutumia taarifa, pia naona hii ku verify Nacte wizi mtupu kwanini mtu ukiomba chuo wasiwe na database mtu aki click information apate matokeo
Acha kabisa mkuu, na utaalamu wote wa haya mambo ila ile siku nilichemka.

Nikasema isiwe shida, ngoja tu niachane nao.

Bahati nzuri nikafanikiwa kuapply pasipo hiyo AVN.
 
Nacte contacts
Screenshot_20200627-013550.jpeg
 
Acha uongo, kwa mtu wa diploma huwezi kuapply chuo pasi kuwa na AVN.. Kama umetokea vidato hapo sawa
Acha kabisa mkuu, na utaalamu wote wa haya mambo ila ile siku nilichemka.

Nikasema isiwe shida, ngoja tu niachane nao.

Bahati nzuri nikafanikiwa kuapply pasipo hiyo AVN.
 
Acha uongo, kwa mtu wa diploma huwezi kuapply chuo pasi kuwa na AVN.. Kama umetokea vidato hapo sawa
Sidhani kama ni sahihi kuongea mambo ambayo usiyoyajua. Kama una Diploma kaapply TIA au hata CBE uone kama itagoma.

Usipende kumuita mtu muongo kama hujawahi kufanya hizi Application.
 
Acha kabisa mkuu, na utaalamu wote wa haya mambo ila ile siku nilichemka.

Nikasema isiwe shida, ngoja tu niachane nao.

Bahati nzuri nikafanikiwa kuapply pasipo hiyo AVN.
Hii inchi bora Hawa CCM tusiwape kura.. Maana wizi njenje kila mahali, sasa hii 10,000 tunayolipia ni ya kazi gani.. Yaan index number yangu ya mtihani nilipie hali ya kuwa nimefanya gharama za kujisomesha hadi napata Award yangu..
Yaan hawa nacte ni WASENGE kinoumah, tena bora hadi AVN yenyewe ingekuwa inapatikana kirahisi ila iko very complicated.

Wanaboa sana, yaan wanatengeneza mambo ili mradi wapate hela, kwani miaka ya nyuma waliokuwa wanatokea diploma walikuwa wanaombaje na naamini haya mambo ya AVN hayakuwepo
 
Sidhani kama ni sahihi kuongea mambo ambayo usiyoyajua. Kama una Diploma kaapply TIA au hata CBE uone kama itagoma.

Usipende kumuita mtu muongo kama hujawahi kufanya hizi Application.
Kwahiyo unataka kunambia hii AVN inahitajika baadhi ya vyuo tu..?
 
Hii inchi bora Hawa CCM tusiwape kura.. Maana wizi njenje kila mahali, sasa hii 10,000 tunayolipia ni ya kazi gani.. Yaan index number yangu ya mtihani nilipie hali ya kuwa nimefanya gharama za kujisomesha hadi napata Award yangu..
Yaan hawa nacte ni WASENGE kinoumah, tena bora hadi AVN yenyewe ingekuwa inapatikana kirahisi ila iko very complicated.

Wanaboa sana, yaan wanatengeneza mambo ili mradi wapate hela, kwani miaka ya nyuma waliokuwa wanatokea diploma walikuwa wanaombaje na naamini haya mambo ya AVN hayakuwepo
Hivi kupata AVN unalipia pia?
 
Back
Top Bottom