Mfumo mbovu wa Elimu Tanzania

Ndosh

Member
Oct 14, 2020
31
13
Habari ndugu zangu.

Kwa machozi mengi naandika juu ya jambo hili. Mimi Ni mmoja kati ya wahitimu katika kozi ya "DIPLOMA IN TECHNICAL EDUCATION" 2019 katika chuo Cha Ualimu Kleruu.

Nia yangu ilikuwa Ni kuendelea katika ngazi ya juu Zaidi ya Elimu, lakini , nimepambana kwa nguvu zote nikaomba mkopo nikakamilisha kila kitu, suala la AVN NUMBER likafuatia, hakika AVN Ni kirusi kwangu, kila kitu kiligonga mwamba, baada ya kufuatilia kwa kina, shida ilionekana NECTA wamenidhurumu haki yangu maana nimefanya mtihani wa NECTA, lakini NECTA wamekumbatia haki zetu (hawataki kupeleka taarifa zetu NACTE), Tafadhali kama kuna waliokaribu na NECTA uzi huu uwafikie, wafanye kazi kwa weledi.

Kama hawawezi basi watujulishe ili tukasome kozi zingine, kinachonishangaza ni kwamba chuo Ni Cha Serikali lakini uzembe mtupu nimeumia sana kupoteza gharama zangu bure kwa uzembe wa watu fulani
 
Habari ndugu zangu. Kwa machozi mengi naandika juu ya Jambo hili,,, Mimi Ni mmoja kati ya wahitimu katika kozi ya "DIPLOMA IN TECHNICAL EDUCATION" 2019 katika chuo Cha Ualimu Kleruu. Nia yangu ilikuwa Ni kuendelea katika ngazi ya juu Zaidi ya Elimu, lakini , nimepambana kwa nguvu zote nikaomba mkopo nikakamilisha kila kitu,, suala la AVN NUMBER likafuatia , hakika AVN Ni kirusi kwangu, kila kitu kiligonga mwamba,, baada ya kufuatilia kwa kina , shida ilionekana NECTA wamenidhurumu haki yangu maana nimefanya mtihani wa NECTA, lakini NECTA wamekumbatia haki zetu( hawataki kupeleka taarifa zetu NACTE) , Tafadhali Kama Kuna waliokaribu na NECTA uzi huu uwafikie, wafanye kazi kwa weledi, Kama hawawezi basi watujulishe ili tukasome kozi zingine, , kinachonishangaza ni kwamba chuo Ni Cha Serikali lakini uzembe mtupu,, nimeumia Sana kupoteza gharama Zangu bure kwa uzembe wa watu fulani

Yaani yote uliyojifunza kwenye hiyo technical education hakuna hata moja linaloweza kukusaidia maishani? Kama jibu ni ndiyo basi elimu yetu (ya technical) kweli ni mbovu. Vinginevyo unachokiongelea ni uzembe tu wa wafanyakazi wa taasisi fulani kwenda nyingine na hakina uhusiano na ubovu wa mfumo wa elimu uliyoipata. Nimekosea?
 
Hii ni Mara ya pili unaeleza hili suala humu ndani, Binafsi naona hili suala limekuumiza sana mkuu wangu!!

Kikubwa Nakuomba uende Huko NACTE tu wakomalie haswaaa Hadi kieleweke mkuu huku sijui Kama utapata msaada zaidi!!
 
Halafu huku analalamikia mfumo wa elimu wakati tatizo analolieleza ni la uzembe na ukiritimba wa watendaji tu. Akikomaa kama ulivyomshauri anaweza kulitatua hili tatizo aisee...
 
Yaani yote uliyojifunza kwenye hiyo technical education hakuna hata moja linaloweza kukusaidia maishani? Kama jibu ni ndiyo basi elimu yetu (ya technical) kweli ni mbovu. Vinginevyo unachokiongelea ni uzembe tu wa wafanyakazi wa taasisi fulani kwenda nyingine na hakina uhusiano na ubovu wa mfumo wa elimu uliyoipata. Nimekosea?
Ni mfumo mbovu mkuu maana bora wangeweka njia mbadala ya kujiendeleza kielimu tofauti na ile ya ulazima wa kuwa na AVN.
 
Pole sana

AVN ni bora sana sema ww unashindwa kwenda NACTE zonal office au HQ kulifatilia mguu kwa kichwa, na pia tatizo lipo kwa examination officer wenu wa chuo hakuwasajili NACTE, na kashindwa kutuma taarifa zenu NACTE maana huwa wanazituma chuoni online kwenda kwenye panel ya NACTE
 
Elewa kuwa nimefanya mtihani wa NECTA,, chuo kinahusikaje hapo? Wakati matokeo yangu yapo NECTA!! chuo kinafuata mfumo wa NECTA siyo NACTE.
 
Kumbe kuna diploma inatolewa kwa mtaala wa NECTA ? nilijua ni certificates tu za ualimu grade B sijui A.

Usiwe mbishi kitu ambacho hujui, AVN inatolewa na NACTE na ndo imepewa mamlaka ya kutunza taarifa za kozi zote under diploma, ko ww huwezi kuendelea hadi NECTA yako ipeleke taarifa zako NACTE inatakiwa ukafatilie DSM mikocheni karibu na TBC
 
Okay,, ahsante
 
Habari ndugu zangu.

Kwa machozi mengi naandika juu ya jambo hili. Mimi Ni mmoja kati ya wahitimu katika kozi ya "DIPLOMA IN TECHNICAL EDUCATION" 2019 katika chuo Cha Ualimu Kleruu.

Nia yangu ilikuwa Ni kuendelea katika ngazi ya juu Zaidi ya Elimu, lakini , nimepambana kwa nguvu zote nikaomba mkopo nikakamilisha kila kitu, suala la AVN NUMBER likafuatia, hakika AVN Ni kirusi kwangu, kila kitu kiligonga mwamba, baada ya kufuatilia kwa kina, shida ilionekana NECTA wamenidhurumu haki yangu maana nimefanya mtihani wa NECTA, lakini NECTA wamekumbatia haki zetu (hawataki kupeleka taarifa zetu NACTE), Tafadhali kama kuna waliokaribu na NECTA uzi huu uwafikie, wafanye kazi kwa weledi.

Kama hawawezi basi watujulishe ili tukasome kozi zingine, kinachonishangaza ni kwamba chuo Ni Cha Serikali lakini uzembe mtupu nimeumia sana kupoteza gharama zangu bure kwa uzembe wa watu fulani
Pole sana boss
 
Elewa kuwa nimefanya mtihani wa NECTA,, chuo kinahusikaje hapo? Wakati matokeo yangu yapo NECTA!! chuo kinafuata mfumo wa NECTA siyo NACTE.
Usiwe mbishi kijana elewa unacho ambiwa,
Nilipatwa na tatizo kama lako 2018, nikashauriwa na mtu niende NACTE nikaenda nacte makao makuu niliweka kambi kama siku 3 mfululizo mpaka jamaa ilibidi wafatilie swala langu kwa kina,
Nakushauri ukishakuja huku mtandaoni ukaeleza tatizo watu wakakupa njia ya kufanya fata hiyo njia uone matokeo yake walau kwa wiki moja ungekomaa ofisi yoyote ya NACTE iliyo karibu na wewe ungeshapata ufumbuzi na ungejiunga chuo. Anza kufatilia saa hizi ili kufika mwakani usipate shida kukimbiakimbia na saa hizi pilikapilika kwenye ofisi za NACTE zimepungua kwa hiyo itakua vizuri kufatiliwa swala lako.
 
Back
Top Bottom