Auto Market App: Suluhisho la Kidijitali kwa Biashara ya Magari na Vipuri Tanzania

KENGE 01

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2021
Posts
1,769
Reaction score
4,389
NRNE

Takriban miezi 6 hadi 7 iliyopita, nilikuja hapa jukwaani kuelezea nia yangu ya kuanzisha jambo lenye manufaa katika sekta ya usafirishaji kupitia uzi huu:

Kama ilivyo kwa kila nia, njia haikosi changamoto. Katika kipindi hiki cha miezi 6 hadi 7, nimejitahidi sana kuhakikisha nazalisha kitu cha kisasa na chenye tija, hasa nikizingatia maendeleo ya teknolojia yalipo sasa. Kwa neema ya Mungu, licha ya kuwa kazi haijakamilika kwa asilimia 100%, lakini naweza kusimama Kifua mbele na kusema “HAPA NIMETOA KITU.”

Auto Market App: Suluhisho Kabambe kwa Biashara ya Vipuri na Magari.

img6.png

Leo narudi kwenu kuwatambulisha rasmi App hii inayoitwa Auto Market – ni jukwaa la kibiashara lenye mfumo wa B2B (Business to Business) na B2C (Business to Customer). Naposema B2B na B2C, simaanishi kwa jina tu; App hii ina mfumo unaomtambulisha muuzaji wa jumla na wa rejareja kwa uwazi kabisa.

Changamoto

Kama msemo unavyosema, "mwanzo ni mgumu." Changamoto kubwa ilikuwa ni uendeshaji wa App yenyewe. Ili App kama hii ifanye kazi kwa ufanisi, inahitaji uwekezaji mkubwa – hasa kwenye mifumo ya kisasa kama database thabiti, muonekano (UI/UX), usalama wa malipo, na ufuatiliaji wa oda. Kwa sababu hiyo, nimeamua kwa sasa kufokus kwenye bidhaa za spare parts pekee. Kama mipango itaenda sawa, tutajitanua zaidi hadi kwenye uuzaji wa magari na huduma nyinginezo.
IMG4.png

Ni Nani Anaweza Kutumia App Hii?

Auto Market App imetengenezwa kwa ajili ya watu wote wanaohusiana na magari, wakiwemo:

  • Wamiliki wa magari.

  • Mafundi wa gereji

  • Wamiliki wa maduka ya vipuri

  • Watu wanaopenda au kufuatilia masuala ya magari (automotive hobbyists)

Baadhi ya Features Muhimu ndani ya App:

Utafutaji wa vipuri kwa urahisi – Weka Car Make, Model, na Year kisha pata vipuri vinavyolingana.
IMG1.png

Malipo salama kwa njia ya Escrow – Pia kuna mfumo wa refund endapo kutatokea changamoto.

Forum (Jukwaa) – Kama JF, unaweza kuanzisha mjadala, ku-comment, ku-like na kupata taarifa (real-time notification) pale mtu anapojibu au kupenda mchango wako.

Customer Care ya kiwango cha SGR – Kupiga simu, WhatsApp, au email – majibu ni ya haraka.

Kujadiliana bei – Unaweza kuomba upunguzwe bei moja kwa moja na muuzaji.

System ya Reviews & Ratings – Wanunuzi wanaweza kutoa maoni na nyota kwa bidhaa na wauzaji.

Notification ya oda mpya – Muuzaji hupokea taarifa moja kwa moja endapo mteja amenunua bidhaa kutoka dukani kwake.

IMG2.png

Kwa Wamiliki wa Maduka ya Vipuri (Shop Owners)

Unaweza kujisajili kama mmiliki wa duka, kisha ukaorodhesha bidhaa zako. Wateja watakaponunua, malipo yanaingia kwenye Escrow, na unapata taarifa papo hapo. Pia, kuna nafasi ya kupata reviews na ratings zitakazoongeza uaminifu na kukuza duka lako.

NB: Lazima uwe na TIN namba na Nida kujisajili kama mmiliki wa duka..Pia itachukua masaa kadhaa ili kuApprove duka lako kuepuka Utapeli

Kwa Mafundi au Wamiliki wa Gereji

Unaweza pia kujisajili kama fundi au gereji. Ingawa bado hatujakamilisha baadhi ya vipengele vya kitengo hiki, kwa sasa unaweza kutumia App kama mtumiaji wa kawaida – ukisubiri toleo lililoboreshwa litakapozinduliwa rasmi.

Jinsi ya Kuipata App

Kwa sasa, App ipo katika hatua ya majaribio (beta testing) kwa muda wa wiki 2 hadi 3 kwenye Google Play Store. Kama ungependa kuwa mmoja wa TESTER, tafadhali jaza barua pepe yako kwenye fomu hii:

Utaanza kupokea email yenye link ya ku-download App moja kwa moja kutoka Play Store.

NB: Kwa watumiaji wa iOS (Apple), bado App haijapatikana lakini iko kwenye mipango. Pia tunatengeneza tovuti rasmi itakayosaidia usajili na ufuatiliaji.
IMG5.png

Nakaribisha...

Wamiliki wa maduka ya vipuri, wauzaji wa rejareja, mafundi, wafuatiliaji wa masuala ya magari, na hata content creators – nyote mnakaribishwa kujiunga na kutuunga mkono.

Ahsante
 
Safi sana ngoja niiweke Ford ranger ya 2017,Diesel 2.2 auto nauza ipo Arusha naileta Daslm wiki hii..
 
NRNE

Takriban miezi 6 hadi 7 iliyopita, nilikuja hapa jukwaani kuelezea nia yangu ya kuanzisha jambo lenye manufaa katika sekta ya usafirishaji kupitia uzi huu:

Kama ilivyo kwa kila nia, njia haikosi changamoto. Katika kipindi hiki cha miezi 6 hadi 7, nimejitahidi sana kuhakikisha nazalisha kitu cha kisasa na chenye tija, hasa nikizingatia maendeleo ya teknolojia yalipo sasa. Kwa neema ya Mungu, licha ya kuwa kazi haijakamilika kwa asilimia 100%, lakini naweza kusimama Kifua mbele na kusema “HAPA NIMETOA KITU.”

Auto Market App: Suluhisho Kabambe kwa Biashara ya Vipuri na Magari.

View attachment 3364728
Leo narudi kwenu kuwatambulisha rasmi App hii inayoitwa Auto Market – ni jukwaa la kibiashara lenye mfumo wa B2B (Business to Business) na B2C (Business to Customer). Naposema B2B na B2C, simaanishi kwa jina tu; App hii ina mfumo unaomtambulisha muuzaji wa jumla na wa rejareja kwa uwazi kabisa.

Changamoto

Kama msemo unavyosema, "mwanzo ni mgumu." Changamoto kubwa ilikuwa ni uendeshaji wa App yenyewe. Ili App kama hii ifanye kazi kwa ufanisi, inahitaji uwekezaji mkubwa – hasa kwenye mifumo ya kisasa kama database thabiti, muonekano (UI/UX), usalama wa malipo, na ufuatiliaji wa oda. Kwa sababu hiyo, nimeamua kwa sasa kufokus kwenye bidhaa za spare parts pekee. Kama mipango itaenda sawa, tutajitanua zaidi hadi kwenye uuzaji wa magari na huduma nyinginezo.
View attachment 3364731

Ni Nani Anaweza Kutumia App Hii?

Auto Market App imetengenezwa kwa ajili ya watu wote wanaohusiana na magari, wakiwemo:

  • Wamiliki wa magari.

  • Mafundi wa gereji

  • Wamiliki wa maduka ya vipuri

  • Watu wanaopenda au kufuatilia masuala ya magari (automotive hobbyists)

Baadhi ya Features Muhimu ndani ya App:

Utafutaji wa vipuri kwa urahisi – Weka Car Make, Model, na Year kisha pata vipuri vinavyolingana.
View attachment 3364729

Malipo salama kwa njia ya Escrow – Pia kuna mfumo wa refund endapo kutatokea changamoto.

Forum (Jukwaa) – Kama JF, unaweza kuanzisha mjadala, ku-comment, ku-like na kupata taarifa (real-time notification) pale mtu anapojibu au kupenda mchango wako.

Customer Care ya kiwango cha SGR – Kupiga simu, WhatsApp, au email – majibu ni ya haraka.

Kujadiliana bei – Unaweza kuomba upunguzwe bei moja kwa moja na muuzaji.

System ya Reviews & Ratings – Wanunuzi wanaweza kutoa maoni na nyota kwa bidhaa na wauzaji.

Notification ya oda mpya – Muuzaji hupokea taarifa moja kwa moja endapo mteja amenunua bidhaa kutoka dukani kwake.

View attachment 3364730
Kwa Wamiliki wa Maduka ya Vipuri (Shop Owners)

Unaweza kujisajili kama mmiliki wa duka, kisha ukaorodhesha bidhaa zako. Wateja watakaponunua, malipo yanaingia kwenye Escrow, na unapata taarifa papo hapo. Pia, kuna nafasi ya kupata reviews na ratings zitakazoongeza uaminifu na kukuza duka lako.

NB: Lazima uwe na TIN namba na Nida kujisajili kama mmiliki wa duka..Pia itachukua masaa kadhaa ili kuApprove duka lako kuepuka Utapeli

Kwa Mafundi au Wamiliki wa Gereji

Unaweza pia kujisajili kama fundi au gereji. Ingawa bado hatujakamilisha baadhi ya vipengele vya kitengo hiki, kwa sasa unaweza kutumia App kama mtumiaji wa kawaida – ukisubiri toleo lililoboreshwa litakapozinduliwa rasmi.

Jinsi ya Kuipata App

Kwa sasa, App ipo katika hatua ya majaribio (beta testing) kwa muda wa wiki 2 hadi 3 kwenye Google Play Store. Kama ungependa kuwa mmoja wa TESTER, tafadhali jaza barua pepe yako kwenye fomu hii:

Utaanza kupokea email yenye link ya ku-download App moja kwa moja kutoka Play Store.

NB: Kwa watumiaji wa iOS (Apple), bado App haijapatikana lakini iko kwenye mipango. Pia tunatengeneza tovuti rasmi itakayosaidia usajili na ufuatiliaji.
View attachment 3364733

Nakaribisha...

Wamiliki wa maduka ya vipuri, wauzaji wa rejareja, mafundi, wafuatiliaji wa masuala ya magari, na hata content creators – nyote mnakaribishwa kujiunga na kutuunga mkono.

Ahsante

Ongoza features kama:
1. Freelance kwa mafundi magari
2. Car scanner with device , powered by AI.
3. AI features : Ushauri kutokana na matokeo ya car scanner.
4. Marketplace with AI-based suggestions. Mteja anatafuta taa ya gari kulingana na model ya gari, AI inamtafutia shop au shops .
5. Nearby - aone maduka ambayo yako karibu(1-5km).
6. Recommended for you. Pendekezo based on preferences and budget..

OVA.
 
Back
Top Bottom