Aunt Ezekiel kusomewa albadil | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aunt Ezekiel kusomewa albadil

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, Jan 30, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  [​IMG] [​IMG]

  Gazeti kiwango kwa habari za mastaa nchini, Risasi Mchanganyiko lipo kwenye nafasi nzuri ya kuliandika hilo baada ya kunasa matamshi ya Sarah ambaye ameeleza kuwa anafikiria kusoma albadili ili kukata mzizi wa fitina.

  Sarah alisema, baada ya yeye kumfumania Aunt akiwa kwenye kitanda chake na Silva, huku wote wakiwa watupu, kumekuwa na kauli nyingi za upotoshaji, hivyo kusisitiza kuwa pengine ikisomwa albadili (dua ya kulaani), ukweli unaweza kujulikana.

  Alisema, hapo kabla hakuwahi kuwa na ugomvi na Aunt kiasi cha kufikia hatua ya kumzushia fumanizi, isipokuwa alichokitekeleza ni kile alichokishuhudia kwa macho yake kwamba mrembo huyo alimsaliti kwa kutoka na aliyekuwa mchumba wake ambapo aliwanasa kitandani kwake.

  “Nimekuwa nikimsikia Aunt anatangaza kuwa sikumfumania, isipokuwa ni chuki zangu binafsi, ameniudhi sana, yaani anataka Watanzania wanione mimi ni muongo ila mkweli ni yeye,” alisema Sarah na kuongeza:

  “Nafikiri ni lazima Watanzania waufahamu ukweli ni upi, mimi nilimfumania Aunt kwa macho yangu, kama anabisha basi awe tayari isomwe albadili ili imdhuru yule ambaye anasema uongo, nipo tayari wakati wowote.”

  Aliendelea kusema, Aut ni msaliti kwa sababu aliufahamu fika uhusiano wake na Silva, ila kwa sababu ana tamaa ndiyo aliona ni vema kuingilia penzi lake, kitu ambacho ni kibaya kwa watu wanaofahamiana.

  Sarah alisema, baada ya kumfumania Aunt, mrembo huyo alitoka nguo mkononi, hivyo anashangaa kuona anavyowahadaa watu ili wadanganyike kuwa hakufumaniwa, bali anasingiziwa.

  “Nimsingizie kwa kipi hasa? Sina sababu ya kufanya hivyo wala siwezi kupata maslahi yoyote kwa kufanya hivyo, labda yeye ndiyo mwenye maslahi kwangu kwa sababu alikuwa anakula jasho langu kupitia kwa Silva ambaye nilikuwa namfadhili kila kitu.
  “Nipo tayari sasa, najua anatumia nguvu nyingi kujisafisha lakini tunaweza kumaliza ubishi, isomwe albadili halafu tuone nani ni mkweli. Muongo atadhurika, kwahiyo Watanzania watapata jawabu kupitia mimi na yeye,” alisema.

  Baada ya kuongea na Sarah, gazeti hili lilichoma muda wake kuongea na Shehe Yusuf Kinduka wa msikiti mmoja jijini Dar es Salaam ambaye alisema kuwa albadili ni kisomo cha kiapo kwa watu ambao wanasuguana.

  “Ni kiapo tu, huyu anaweza kumtuhumu mwenzake ambaye naye anakuwa anapinga, kwahiyo albadili husomwa hapo kwa lengo kwamba kama ni kweli mtuhumiwa ni mkosaji basi apate adhabu kutoka kwa Mungu endapo atakuwa amesingiziwa, adhabu itamrudia yule mlalamika.

  “Si dua nzuri kuisoma kwa mtu kwa sababu inapojibu, huwa inakuwa kali mno kwa yule inayemshukia. Kwa kawaida haina gharama, ni bure kwa sababu ni kumshtakia Mungu ila unaweza kuamua kutoa sadaka pale unapoona inabidi,” alisema Shehe Yusuf.

  Aunt, alifumaniwa hivi karibuni na Sarah, kisha gazeti hili katika toleo lake la Jumamosi ndilo lilikuwa la kwanza kuripoti habari hiyo, ingawa mrembo huyo anayewika kwenye kiwanda cha filamu hivi sasa, amekuwa akijitembeza kukanusha.


  http://www.globalpublisherstz.com/2009/11/25/aunt_ezekiel_kusomewa_albadil.html
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,253
  Likes Received: 19,383
  Trophy Points: 280
  hii Albadir naomba isisomwe manake itampitia jamaa yetu humu JF anaitwa NDUGU.jamaa amezimika sana kwa huyu binti hadi alimuanzishia thread.D;D;D
   
 3. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hivi visomo vingine ni dini au ulozi?
   
 4. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #4
  Jan 30, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  mimi sielewi matumizi ya hiyo kitu inaitwa Albadir, maana mtu akikukosea unamtihia kumsomea, and how it work....Tumain atatoa ufafanuzi , kama mtu akinikera naweza kumchapa na hiyo kitu.
   
 5. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #5
  Jan 30, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Hii imekaaje wadau; mbona sioni adhabu anayoelekea kuipata Silva (Mchumba) na kwanini Aunt ndio aonekane yeye ndio msaliti pekee; huyu mchumba hana makosa hapa? Hii kitu inanifanya nipateshida na je baada ya hili uchumba umeendelea?
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Jan 30, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,253
  Likes Received: 19,383
  Trophy Points: 280
  hii ipo kwenye jokes?huh.
   
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  Jan 30, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160

  [​IMG]
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Jan 30, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  kwani nielimisheni mwenzenu kwani Aunt EZEKIELI ni nani hasa...? maana naanza kushangaa mwenyewe kumbe ni mtu maarufu sana, kiasi cha watu kuwa hata na picha zake
   
 9. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #9
  Jan 30, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   
 10. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #10
  Jan 30, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  ooh asante sana, je unaweza ukanipatia na cell namba kake...asante
   
 11. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #11
  Jan 30, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

   
 12. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #12
  Jan 30, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Kwani ni kweli huwa vinafanya kazi au ni hofu tu ya watu?:confused:
   
 13. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #13
  Jan 30, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Kibunango napata wsiwasi hapa message kwa khanga tena!? Mipasho au unadumisha mila?
   
 14. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #14
  Jan 31, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,908
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Huyo dada anayejifanya kutaka asome hiyo albadiri angejisomea mwenyewe ili ajue alichokikosa mpenziwe kwake mpaka akamfuata mrembo wetu Bi. Anti..
   
 15. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #15
  Jan 31, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  hivi kwa mfano kasomewa albadir , harafu kavimba tumbo, harafu kapelekwa UFUFUO NA UZIMA kaombewa kwa jina la yule aliye kinyume na mashetani na mapepo yaani YESU, hara akapona, sasa hapa naomba mnijuze si ina maana albadir itakuwa ni nini?
  si mnajua mtu aombewavyo ee? kwa jina la Yesu ewe pepo nakuamuru tooka!!!!
   
 16. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #16
  Jan 31, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  huyu atakuwa anaabudu mapeppo, maana hayana maarifa
   
 17. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #17
  Jan 31, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana nawe mzeee wangu, ingekuwa ni kitu hatari kama "nyuklia" nadani Taifa la wana wa Islael ambalo lipo katika kati ya Watalamu wa hivyo visomo lingekwisha tetekea kabisa. Na watu kama G.W. Bush sijui kama angekuwepo katika hii dunia!.


  Ebu enyi wana adamu muishio kwa na kuamini kutegemea hivyo visomo tufunulieni wengine haya makuuu, enendeni mkamsomee huyu anayeifanya nchi yetu yenye kila aina ya utajiri izidi kuwa maskini kila kukicha.


  Mkawasomeeni majambazi wanaoua na kuiba mali za raia wema waliojitafutia kwa jasho mali zao; wasomeeni mafisadi na wala rushwa wacahche wanaoishi maisha tambalale na kula bata kwa jasho la wengi;


  Enendeni mkawasomee kisomo hiki hawa wanaotuibia hela zetu kupitia makanisa ya ufunuo na upako na kuongeza umasikini kwenye jamii; mkamsomee yule anayeifanya nchi hii ya kilimo iendelee kutegemea mvua kila siku; muwasomee RICHMOND, IPTL, DOWANS, na vizazi vyao ambao wameliingiza taifa katika mkenge, Muwasomee wanaotaka kuvuruga Muungano kwa maslahi binafsi, Muwasomee na dereva wazembe wanaosababisha ajali za hovyo barabarani na kusababisha maisha wa wasio na hatia kupotea; muwasomee wanaobakaji na wanaoambukiza wenzao UKIMWI kwa makusudi.

  Naomba kuwasilisha haya maombi yangu kwa kuanzia!
   
 18. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #18
  Feb 1, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Unaweza mpata kwa email yake : auntezekiel12009@yahoo.com, usiache kuniPM na kunipa thanks!
   
 19. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #19
  Feb 1, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Masanilo,.aaaaakha!

  Kutoka kwenye "addiction" ya "chinywaji" sasa upo kwenye viwango vya "kuhamasisha" maambukizi mapya kwa vijana wetu kwa kuachia hewani mawasiliano ya warembo?, duh siamini!
   
 20. Natty Bongoman

  Natty Bongoman JF-Expert Member

  #20
  Feb 1, 2010
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hahaaa
   
Loading...