Augustino Ramadhani: Chaguo la system

Augustino Ramadhani: Chaguo la system

Rutunga M

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2009
Posts
1,769
Reaction score
1,393
agustino_ramadhani.jpg

Sisi wengine tunajitokezaga kipindi kama hiki tu.
Augustino Ramadhani ndiye chaguo la system.taarifa kutoka kabatini ndo hizo.
Kigezo kilichotumika ni issue ya udini na mfumo wa muungano kuanzia kwa nyerere ghadi jk.
Bara imetoa rais vipindi vitatu kati ya vinne.Zamu hii ni ya Zanzibar.

Ni ngumu kumeza lakini taarifa ndo hiyo.

Pole sana baadhi yenu.

UPDATES:
January Makamba na Benard Membe wamepatikana na hatia ya kosa la kufanya kampeni kabla ya muda kinyume cha taratibu na kanuni za CCM.

Ngeleja na Lowassa wamekutwa na makosa matatu kila mmoja ambayo ni uadilifu, kutoa rushwa na kufanya kampeni kabla ya muda.

Lowassa ameonekana kuwa na utovu mkubwa wa nidhamu kwani amedaiwa kusambaza fomu as udhamini kabla ya muda huku akihonga watu kuchukua kadi mpya za chama maeneo ya Zanzibar kinyume cha sheria.

Pia Lowassa na Membe wamedaiwa kukigawa vibaya chama pamoja na vyombo vya habari hali iliyotafsiriwa kuwa ni makosa kulingana na miiko ya CCM.

Kwa maana hiyo mashitaka yote yanapelekwa kamati kuu ya CCM kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi.

Leo usiku hatima ya hawa wote itajulikana. Sisi tutakuwepo kumulika kwa macho kama paka

=======
UPDATE 1:


UPDATE 2:




Mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Jaji mstaafu Augustino Ramadhani amewataka Watanzania kuendelea kumwombea ili mapenzi ya Mungu ya kumfanya kuwa kiongozi wa Taifa yatimie.

Jaji Ramadhani alisema hayo jana wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Dayosisi ya Dar es Salaam. Katika sherehe hizo, mgombea huyo alikuwa mgeni rasmi akiambatana na Dk Mwele Malecela ambaye pia anawania nafasi hiyo.

Jaji Ramadhani, ambaye ni mchungaji wa kanisa hilo alisema haikuwa mapenzi yake kutangaza nia ya kugombea urais, bali alipata msukumo kutoka kwa Mungu mwenyewe.

"Kila siku watu wananipongeza kwa kujitokeza kuwania urais. Ninawaambia safari bado ni ndefu, wazidi kuniombea ili mapenzi ya Mungu yatimie," alisema.

Azungumzia rushwa

Kiongozi huyo alisema rushwa imekuwa tatizo kubwa nchini na kubainisha kuwa yeye anachukia na hata Mungu pia haipendi.

Alisema CCM imekuwa ikipambana na rushwa chini ya msemo wake ‘rushwa ni adui wa haki' na kuwataka wananchi wabadilike na kuepuka rushwa.

Awali akimkaribisha Jaji Ramadhani, Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk Valentino Mokiwa alimpongeza kwa kujitokeza kuwania urais, akisema kati ya waliojitokeza, yeye ameonekana kuwa na karama nyingi.

Alisema Jaji Ramadhani amekuwa ni Kasisi wa Kanisa la Anglikana, aliwahi kuwa Brigedia Jenerali, alikuwa Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu na pia ni Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu.

"Tuko nyuma yako, tunakuombea kwa Mungu ushinde nafasi ya urais ili utende haki na kupambana na rushwa," alisema Askofu Mokiwa.

Askofu Mokiwa alisisitiza kuwa wala rushwa wote wafungwe bila huruma ili kuondoa tatizo hilo.

Alipoulizwa kuhusu Jaji Ramadhan kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo licha ya kuwa yeye ni kasisi tu wa kanisa hilo, mjumbe wa kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo, Mchungaji John Kamoyo alisema uamuzi huo unatokana na uhusiano kati ya Jaji Ramadhani na Askofu Mokiwa.

"Majibu ya swali hilo ni mengi, lakini nadhani ni uhusiano tu kati ya Askofu Mokiwa na Jaji Ramadhani. Kuna mambo mengi lakini nisingependa kueleza hapa," alisema Mchungaji Kamoyo.

Source: Mwananchi
 
nani atatusaidia kumuuza mtu mwenyewe hatumfaamu,
poleni wazee wa ccm mliompendekeza mwaka ccm mkimpitisha mtu asiyefaamika au mwizi kazi mnayo.
 
Atauweza mfupa alioushindwa fisi?Namuonea huruma tu.Maana zigo la kichaa wanamwachia pole zake.
 
1,Rais Mgufuli
makamu ramadhani
au
2 Rais mwandosya
makamu-ramadhani

kwa miundo hiyo watapona ccm nje ya hapo kazi wanayo,
 
Huyu ni Mtu Kutoka Nchi Jilani au Marafiki Zetu Wazanzibar Kwa Maana Zanzibar ni Nchi Huru iliyokamilika. CCM wakimleta Huyo Waandike Maumivu Kwa Maana Huyu ni Mzanzibar na Zanzibar ni Nchi Kama ilivyo Burudi au Rwanda.

Rais wa Tanganyika Hapigiwi Mizinga Zanzibar Kama Tulivyoona kwenye Sherehe za Uhuru wa Zanzibar. Hapana Ndani ya CCM leteni Mtaganyika na UKAWA Wataleata Mtanganya.
 
Duh! Unajua hata haisound kuitamka just imagine "AKizindua mradi huo Rais Agustino Ramadhani alisema......"yaani nakosa radha kabisa jina lake litatamkikaje,listen nahsi jaji anakwenda kupewa jumba bovu,though atashinda general election ila kwa shida sana,ile CCM angepewa Makongoro ndio ingenyooka!
 
Huyu ni mtu safi ambaye ndiye anaweza kumaliza makundi kwa sasa ndani ya CCM

kweli je watu vijijini wanamfaamu ambako ndo wapinga kura waliko,mimi nawashauri wafanye kama kwa kikwete,
1,magufuli-rais
2,ramadhani-makamu

hii timu itashinda kwa kishindo na inakubalika na itasaidia wabunge wa ccm,ia tutapata baraza la mawazri bora.
 
Duh! Unajua hata haisound kuitamka just imagine "AKizindua mradi huo Rais Agustino Ramadhani alisema......"yaani nakosa radha kabisa jina lake litatamkikaje,listen nahsi jaji anakwenda kupewa jumba bovu,though atashinda general election ila kwa shida sana,ile CCM angepewa Makongoro ndio ingenyooka!

kwa hali ilinyo ccm kumsimamisha ramadhani kama rais na ubora wake ni kazi kushinda maana ccm hawajamuanda ,itakuwa ni kazi kubwa wala hatawasaidia wabunge wa ccm
so,
awe makamu wa rais kati ya magufuli au makongoro basi,
 
Atauzika kirahisi sana

utamuuza wapi na siasa zilinyo ? wakati wenzao wanaombakura ccm watakuwa wanaangaika kumuuza mpaka watu wamjue siku ya kupiga kura imefika,lakini pia sisaa pedwa za sasa hivi anaziweza ?,
 
Huyu ni Mtu Kutoka Nchi Jilani au Marafiki Zetu Wazanzibar Kwa Maana Zanzibar ni Nchi. CCM wakimleta Huyo Waandike Maumivu Kwa Maana Huyu ni Mzanzibar na Zanzibar ni Nchi Kama ilivyo Burudi au Rwanda.

Rais wa Tanganyika Hapigiwi Mizinga Zanzibar Kama Tulivyoona kwenye Sherehe za Uhuru wa Zanzibar. Hapana Ndani ya CCM leteni Mtaganyika na UKAWA Wataleata Mtanganya.

milion 5 kuongoza milion 43,sijui
 
votes must decides

MNATAKA KUTUPANDIKIZIA MTU !!!

ILI IWE SIMPLE KUENDELEZA UMWINYI!!!
 
Huyu ni Mtu Kutoka Nchi Jilani au Marafiki Zetu Wazanzibar Kwa Maana Zanzibar ni Nchi. CCM wakimleta Huyo Waandike Maumivu Kwa Maana Huyu ni Mzanzibar na Zanzibar ni Nchi Kama ilivyo Burudi au Rwanda.

Rais wa Tanganyika Hapigiwi Mizinga Zanzibar Kama Tulivyoona kwenye Sherehe za Uhuru wa Zanzibar. Hapana Ndani ya CCM leteni Mtaganyika na UKAWA Wataleata Mtanganya.

wazee wa NEC waisome hii itawasaidia kufanya maamuzi sahihi ili kuendelea kuongoza dora,
 
Huu utaratibu wa ovyo kweli.

Ngoja CUF ishinde Zenji ndo mwisho wa huu muungano.
 
hivi sifa hizi anazo tunazotaka atakayeitishwa na ccm ili kumuuza vizuri kwa wananchi?
1,mkali
2,mchapa kazi
3,kwa umri wake kuna kitu amekifanya ktk nchi hii ambacho aswa vijijini amboko ndo kunawapiga kura kuwa kunaweza kumsaidia kuomba kura?
4,uwezo wa kusimamia serikali,maana namuona kama alikuwa nye ya system,
5, uwezo wa kufanya maamuzi mangu yapo aliyoyafanay yatamsaidia kutuaminisha kuwa anaweza ?
6,namuona mpole vile
7 siasa za sasa za vijana anaziweza?
 
rais wa tanzania mzanzibar
rais wa zanzibar mzanzibar

kweli!! ebu lione hili ccm
 
Rutunga M

Umetoka jela? Wenzako hii sio tena habari mpya bali ni historia. Pole sana kama ndio unajua leo!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom