Augustino Ramadhani: Chaguo la system

Augustino Ramadhani: Chaguo la system

Nilishasemaga hapa kwamba hili zigo wanataka kumrithisha Jaji maana ni mpole na cartel hawa wakina jk na wenzake watamwambia nini afanye.

Kikwete anapenda sana watu wadhaifu.
Jaji ramadhani sio dhaifu sema mpole na hata kuwa na maamuzi
 
Mmeshaanza Majungu Yenu. Watanzania Sijui Tupoje. Hivi Na Wewe Mathalan Baba Yako Angekuwa Ndiyo Rais Wetu Usinge Feel Proud? Tutafutieni Basi Rais Tasa Mridhike!

Ni mtazamo tu mkuu usijenge chuki,hata rizone mwaka 2003/4/5 alikuwa kachoka tu lakini baada ya mshua kuchukua nchi na yeye ni bilionea.
 
Ni mtazamo tu mkuu usijenge chuki,hata rizone mwaka 2003/4/5 alikuwa kachoka tu lakini baada ya mshua kuchukua nchi na yeye ni bilionea.

Mmmmmmmmh! Lakini Hili Nalo Neno Kwani Nakumbuka Miaka Ya 88 Hadi 92 Nikiwa Skonga Hapo Jirani Na Kanisa La Mtakatifu Petro Obey Tukiwa Tunatoka Shule Na Kupiga Misele Hadi Maeneo Ya Drive In Enzi Hizo Ambako Ni Karibu Na Kwao Pale Kwa Chini Ulikuwa Unakuta Lile Deli La Ice Cream Kwa Nje Na Tukiwa Tukitaka Kununua Ice Cream Basi Dogo Rizimoko Alikuwa Anatoka Baru Kutoka Ndani Na Kuja Kutuuzia Na Leo Dogo Kaula Kimaisha. Anyway King Kong III Nimekuelewa Mkuu!
 
Wakimleta huyo tunachukua kura zetu Ukawa kwasababu nilimpenda Makongoro huko CCM ..hili zee pelekeni kwao Zanzibar na wala hata mvuto hana. Atakuwa ana uchu sana Wa madaraka huyu mara jaji, Mara mchungaji mara brigedia mara raisi, hatukubali kamwe kwasababu kwanza umri wa kustaafu kashatimiza na zaidi ..upuuuzi huu.
 
Tuendelee kuhabarishana.
Mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Jaji mstaafu Augustino Ramadhani amewataka Watanzania kuendelea kumwombea ili mapenzi ya Mungu ya kumfanya kuwa kiongozi wa Taifa yatimie.

Jaji Ramadhani alisema hayo jana wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Dayosisi ya Dar es Salaam. Katika sherehe hizo, mgombea huyo alikuwa mgeni rasmi akiambatana na Dk Mwele Malecela ambaye pia anawania nafasi hiyo.

Jaji Ramadhani, ambaye ni mchungaji wa kanisa hilo alisema haikuwa mapenzi yake kutangaza nia ya kugombea urais, bali alipata msukumo kutoka kwa Mungu mwenyewe.

“Kila siku watu wananipongeza kwa kujitokeza kuwania urais. Ninawaambia safari bado ni ndefu, wazidi kuniombea ili mapenzi ya Mungu yatimie,” alisema.

Azungumzia rushwa

Kiongozi huyo alisema rushwa imekuwa tatizo kubwa nchini na kubainisha kuwa yeye anachukia na hata Mungu pia haipendi.

Alisema CCM imekuwa ikipambana na rushwa chini ya msemo wake ‘rushwa ni adui wa haki’ na kuwataka wananchi wabadilike na kuepuka rushwa.

Awali akimkaribisha Jaji Ramadhani, Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk Valentino Mokiwa alimpongeza kwa kujitokeza kuwania urais, akisema kati ya waliojitokeza, yeye ameonekana kuwa na karama nyingi.

Alisema Jaji Ramadhani amekuwa ni Kasisi wa Kanisa la Anglikana, aliwahi kuwa Brigedia Jenerali, alikuwa Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu na pia ni Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu.

“Tuko nyuma yako, tunakuombea kwa Mungu ushinde nafasi ya urais ili utende haki na kupambana na rushwa,” alisema Askofu Mokiwa.

Askofu Mokiwa alisisitiza kuwa wala rushwa wote wafungwe bila huruma ili kuondoa tatizo hilo.

Alipoulizwa kuhusu Jaji Ramadhan kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo licha ya kuwa yeye ni kasisi tu wa kanisa hilo, mjumbe wa kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo, Mchungaji John Kamoyo alisema uamuzi huo unatokana na uhusiano kati ya Jaji Ramadhani na Askofu Mokiwa.

“Majibu ya swali hilo ni mengi, lakini nadhani ni uhusiano tu kati ya Askofu Mokiwa na Jaji Ramadhani. Kuna mambo mengi lakini nisingependa kueleza hapa,” alisema Mchungaji Kamoyo.

Source: Mwananchi
 
UPDATES leo july 9,2015

January Makamba na Benard Membe wamepatikana na hatia ya kosa la kufanya kampeni kabla ya muda kinyume cha taratibu na kanuni za CCM.

Ngeleja na Lowassa wamekutwa na makosa matatu kila mmoja ambayo ni uadilifu, kutoa rushwa na kufanya kampeni kabla ya muda.

Lowassa ameonekana kuwa na utovu mkubwa wa nidhamu kwani amedaiwa kusambaza fomu as udhamini kabla ya muda huku akihonga watu kuchukua kadi mpya za chama maeneo ya Zanzibar kinyume cha sheria.

Pia Lowassa na Membe wamedaiwa kukigawa vibaya chama pamoja na vyombo vya habari hali iliyotafsiriwa kuwa ni makosa kulingana na miiko ya CCM.

Kwa maana hiyo mashitaka yote yanapelekwa kamati kuu ya CCM kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi.

Leo usiku hatima ya hawa wote itajulikana. Sisi tutakuwepo kumulika kwa macho kama paka

=======
UPDATE 1:


UPDATE 2:
 
Back
Top Bottom