Aua mkewe baada ya kumfumania

Aua mkewe baada ya kumfumania

Luggy

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2012
Posts
4,166
Reaction score
4,092
Mkazi mmoja wa Kijiji cha Idubula, katika Kata ya Karitu ,wilayani Nzega, Tabora, amemuua mkewe kwa kumkatakata kwa mapanga baada ya kumfumania.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Antony Lutta, alisema tukio hilo lilitokea usiku wa mkesha wa Sikukuu ya Pasaka.

Lutta alisema mtuhumiwa alimfumania mke wake Veronica Maganga (20) akiwa chumbani kwake na mwanamume mwingine .

Kwa mujibu wa kamanda huyo, mwanamume huyo alifanikiwa kukimbia.
Alisema hasira za mtuhumiwa katika tukio hilo ziliishia kwa kumtakata mke kwa panga hadi alipokufa.

Kamanda Lutta aliwataka wananchi kutojichukulia sheria mikononi mwao na badala yake, waviachie vyombo vya dola kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa.
“Watu wamekuwa na tabia ya kujichukulia sheria mikononi kwa kuwahukumu watuhumiwa, huo ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za nchi na tunawasihi waache,” alisema kamanda huyo.

Alisema mtuhumiwa wa tukio hilo atafikishwa mahakamani mara baada ya kukamilika kwa upelelezi.

Aua mkewe baada ya kumfumania - Habari - mwananchi.co.tz
 
haya na iwe fundisho mke wa mtu mtu sumu
 
Kabinti kaa 20yrs?mhh damu changa inachemka haviridhiki,tamaa mbele kisa atanunuliwa simu tecno
 
Mapenzi yaua ...................................!:A S 39:
 
Si ungi mono hata kidogo mauaji ya aina hii, huu ni ukatiri uliopitiliza.

Hapa lazima panamapungufu makubwa sana kwa huyu jamaaa kujichukulia sheria mkononi na kutoa adhabu ya kikatiri namna hii kwa mkewe.

Kuna maswali mengi ya kujiuliza hapa maana mwanamke ameshakufa na hatujui kama ni kweli alikutwa live kwani hata nafasi ya kujieleza hajapewa yeye hukumu yake ilikuwa kifo.

So sad,
JE kama alibakwa na huyo mwanaume?
Na ni kweli walikuwa wanafanyangono? inasikitisha sana
Na serikali ihakikishe inachukuwa hatua kali kabisa kwa huyu mwanaume ili liwe fundisho kwa wanaume makatiri kama yeye!
 
Ni ukatili tu na kutokua na Huruma,

Huyo Bwana Yeye ni msafi sana kwenye hiyo ndoa??????????????????
 
Hata ingekuwa ww mwanasheria mku au general mkuu lazima usingekubali. Simlaumu
 
Safi sana na iwe fundisho kwa wazinzi wengine na wazazi wanaowapa watoto wao malezi mabaya.Ningependa kama hata huyo waliyekuwa nae angekatwakatwa ili nayo iwe fundisho kwa wanaume wanaochukua wake za watu na kuzini nao.
 
Kaua mke hategemei kukutana naye tena maishani mwake. Yeye anakwenda jela mgoni wake anaendelea kudunda mtaani mwenye faida ni yeye au mwenzie. Hasira hasara.
 
Back
Top Bottom