Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Bara la africa limezindua rasmi cheti chake cha kusafiria.
Madhumuni ya umoja wa africa (AU) kuzindua cheti hicho ni kuvunja mipaka iliyowekwa na mkoloni alipoigawa Africa ili kuitawala katika karne iliyopita.
Viongozi wa africa wamezindua cheti hicho maalum mjini Kigali Rwanda katika kongamano la viongozi wa africa.
Wakwanza kupewa cheti hicho watakuwa ni viongozi wenye hadhi ya kupewa vyeti vya kidiplomasia.
Mwenyeji wa kongamano hilo Rais Paul Kagame atakuwa wa kwanza kupewa cheti hicho na mwenzake Rais wa Chad Idris Deby.
Marais wote wakiohudhuria kongomani hilo watapewa cheti hicho cha (AU) kabla ya kukamilika kwa mkutano huo.
Mawaziri wa maswala ya kigeni na viongozi wakuu katika umoja wa africa pia wanatarajiwa kufaidi cheti hicho cha kusafiria.
Umoja wa Africa unatarajia kuwa mataifa ya kiafrika yataanza kutoa vyeti hivyo vipya vya usafiri kufikia mwaka wa 2018.
Chanzo: BBC