Dr leader
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 1,065
- 1,412
Kwa nini mambo mabaya mengi huongezeka licha ya kukemewa ?
Kuna mdau ameniuliza swali hili
Pombe ni mbaya, kila siku tunaisema ila wanywaji wanaongezeka?
Mauaji ni mabaya, kwa nini kila siku yanaripotiwa ila hayapungui?
Jibu langu
Akili ya mwanadamu inahifadhi
Unaposema mara kwa mara:
“Usinywe pombe… usinywe pombe… usinywe pombe…”
Akili haisikii “usi-”
Inabeba “pombe.”
Hapa ndio inapoingia ile dhana ya kisaikolojia
Illusory truth effect — jambo likirudiwa mara nyingi, linaanza kuonekana la kawaida… hata kama ni baya.
Tatizo sio kusema — tatizo ni unasema vipi?.
Ukirudia kitu bila mwelekeo wa elimu na maadili, unakipa nguvu.
Ukikiweka hadharani kwa style ya kuvutia, unakitangaza.
Ukikizungumzia bila mipaka, unakifanya kiwe cha kawaida.
👉 “Attention + Repetition = Normalization”
Unachokipa attention, unakikuza.
Unachokirudia, unakijenga ndani ya akili za watu.
Sigara imeandikwa ni hatari kwa afya ila ni moja ya bidhaa zenye soko kubwa
Ndio maana wanazuoni walikuwa makini sana.
Madhambi makubwa hayakutajwa kwa lugha ya kuyafanya yaonekane ya kuvutia…
Bali kwa:
• Lugha ya kufundisha
• Lugha ya kuonya
• Lugha ya kukatisha tamaa
Sio lugha ya “kuchochea udadisi.”
Na ndivyo mafundisho mengi ya kidini yalivyo
Leo hii changamoto
Kuna mambo zamani yalikuwa yanazungumzwa kwa tahadhari…
Lakini leo:
• Yapo kwenye nyimbo
• Yapo kwenye mitandao
• Yapo kwenye TV
• Yapo hadi kwenye katuni
Sio kwa lengo la kufundisha… bali kuvutia.
Matokeo yake?
Watu hawaogopi tena…
Watu wanakuwa na curiosity ya kujaribu.
Ukirudia jambo bila hekima, unaligeuza kuwa wazo.
Ukilipa attention, unaligeuza kuwa hamu.
Ukili-normalize, unaligeuza kuwa tabia.
Hivyo basi:
Sio kila kitu kinahitaji kusemwa sana…
Na sio kila kinachosemwa kinahitaji kusemwa kwa style ya kuvutia.
Kuna mambo ukitaka yapungue,
yafundishe kwa ukali na hekima — sio kuyapa umaarufu.
Abuuabdillah ✍️