ATM & Cards Statistics in Tanzania

PeterMimi00

New Member
Oct 31, 2007
2
0
Wapendwa jee kuna mtu anayeweza kunipatia taarifa zifuuatazo kuhusiana na ATM, Cards na Services za ATM au Cards zinazotolewa na mabenki hapa nchini. Nipo katika kufanya research yangu ya shule hivyo ningependa kama yoyote yule mwenyewe information yoyote ile inahusiana na kichwa cha habari hapo juu naomba anipatie hata kama ni ya benki moja moja.

1. Je BANK (Jina la Benki) ina ATM ngapi
2. Je BANK (Jina la Benki) ina wateja wangapi wa Kadi za ATM ngapi
3. Je BANK (Jina la Benki) ina service zipi za ATM ngapi, kwa mfano VISA, MasterCard, Kulipia Bili, Kulipia Vocha n.k

Ntashukuru sana nikipata taarifa hizo,
Asante sana.


Majina ya Mabenki
1. Access Bank Tanzania Ltd.
2. Akiba Commercial Bank Ltd
3. Azania Bancorp
4. BancABC
5. Bank M (T) Ltd
6. Bank of Africa
7. Bank of Baroda (T) Ltd
8. Bank of India Tanzania Ltd
9. Barclays Bank (T) Ltd
10. BOA
11. CF Union Bank ltd
12. Citi Bank
13. Commercial Bank of Africa
14. CRDB Bank Ltd
15. Dar-es-Salaam Community Bank
16. Diamond Trust Bank
17. Exim Bank (T)Ltd
18. FBME
19. Habib African Bank Ltd
20. International Commercial Bank (T) Ltd
21. Kenya Commercial Bank Ltd
22. National Bank of Commerce Ltd
23. NMB
24. Savings and Finance Commercial Bank Ltd
25. Stanbic Bank
26. Standard Chartered Bank (T) Ltd
27. Tanzania Investment Bank
28. Tanzania Postal Bank
29. The Peoples' Bank of Zanzibar Ltd
30. Twiga Bancorp
31. United Bank for Africa
 
Mkuu hizo data utapata lakini inaweza kuhitaji uunguze sori ya kiatu kidogo ukawapate wahusika huko huko kwenye benki. Kimsingi utapata data za uhakika kuliko humu jamvini.
 
Kupata hizi data kunawezekana sema tatizo ni ushindani wa kibiashara uliopo baina ya mabenki yenyewe. Nilishawahi kuulizia kwa benki moja wakaniambia hizo habari hawatoi kwa hofu ya kuwapa mwanya wapinzani wao wakajua nguvu zao. Ila kwa jumla ya idadi ya ATM nchini ni kama 663 hivi (hii ni data za karibuni kabisa). sijui kama nimesaidia kidogo...
 
Hizo ni changamoto za kufanya utafiti na kukusanya takwimu pia. Takwimu unazoomba ndugu yangu ni nyeti hakuna anayeweza kukupa zote kama unavyopenda katika mtandao huu. takwimu hizi ukizipata unaweza ukazitumia katika mambo mengi sana. Nakushauri nenda katika benki husika na barua rasmi wanaweza kukusaidia. Nadhani pengine itabidi wakusainishe mkataba wa kutoziuza au kuzisambaza. Kama unavyojua suala la ushindani kama walivyo andika wachangiaji wengine. Nakutakia kila raheri katika utafiti wako.
 
Back
Top Bottom