Atlas Primary School - Madale, Dar

Hili dongo linanihusu maana mie nimeshawishiwa tu Na jamaa Angu kuwa Atlas wapo vizuri,lakini nadhani jamaa Angu aliangalia upande wa Taaluma tu.Sasa nami sikufanya upembuzi yakinifu naona hapa napata Challenge hiyo Bora nifanye Sasa upembuzi yakinifu
 
Aiseee Kiongozi hiyo peace and love wapo vizuri kitaaluma? Aiseee ngoja Jumatatu nikaulizie Aiseee
Kwa maoni yangu wapo vizuri, wanajali watoto na malezi ya watoto ni mazuri sana. Wamesajiliwa si muda mrefu mwakani ndo wanafunzi wao wa kwanza wanafanya mtihani wa kitaifa wa darasa la nne. Kaulize ulete mrejesho kwa faida ya wengine pia.
 
Ni vema uwahamishe tu
Maana sisi wa kwetu huku elimubure wanagombea daladala na hakuna noma yoyote.!
 
Kwa maoni yangu wapo vizuri, wanajali watoto na malezi ya watoto ni mazuri sana. Wamesajiliwa si muda mrefu mwakani ndo wanafunzi wao wa kwanza wanafanya mtihani wa kitaifa wa darasa la nne. Kaulize ulete mrejesho kwa faida ya wengine pia.
Poa mkuu naenda Jumatatu Na nitaleta mrejesho humu
 
Hiyo shule si kuwa ni nzuri sana, basi tu wanakaririsha wanafunzi ili mwakani wapate wengi zaidi.
Mzazi unatakiwa utambue kuwa elimu pekee bila malezi Bora hamsaidii mtoto, mtoto atafaulu ila atafeli maisha
 
Ni kweli lakini, jamani hiyo shule ina watoto wengi sijapata kuona, hilo naona ndilo linalompa jeuri. Halafu kama ile ya Ubungo mazingira ni hivyo tu hata viwanja vya kucheza watoto hakuna. Watoto wanavushwa barabara kwenda kwenye viwanja vya hosteli za Udsm pale Mabibo. Ukiwaona utawaonea huruma. Mazingira mabovu, ila wanafanya vizuri kwenye mitihani na ada ni nafuu sana ukilinganisha na shule nyingi. Mmiliki analitambua hilo ndio maana anawajibu atakavyo anaamini hamuwezi kuhama na vyuma hivi vilivyokaza.
 
Unakuta mtoto anakaa mbagala..eti anaenda tusiime...unakutana na watoto saa kumi na moja kasoro wako barabaran kusubiri skul bus....aisee huu ni utesaji kwakweli...
Ofcz primary skul sio ya kutumia nguvu hivyoo km sekondary
 
Sio kweli, kimkoa Hazina iko juu, na hiyo ya Madale ndio kabisaa inapitwa na shule kibao kama Lieberman, Rightway etc
 
Vipi kuhusu King's ?
 
ATLAS MADALE KUNGUNI KUNGUNI NI KERO KWA WANAFUNZI WA BWENI.. Hili tatizo hata mwenye shule halijali kwani ktk mkutano na wazazi liliulizwa swali kuhusu kunguni na halikujibiwa kabisa. Kuhamiaha mtoto sio suluhisho. hao wanaobaki kunguni watahama na wao kuwa salama mkuu wa ahule aombe msaada wa kitaalamu kutatua tatizo hili vinginevyo aweke vitanda vya chuma na magodoro ya waliopo yapigwe dawa isiyo dhuru maji ya moto wanayo mwagia vitanda ni suluhisho la siku chache sana.

Sent from my HUAWEI Y330-U11 using JamiiForums mobile app
 
Siyo lazima ila kuna madhara anayopata mtoto kuhama shule moja kwenda nyingine. Loosing friends na kwenda ku adapt mazingira Maya. Nadhani unalitambua hilo
Kwaio ni heri uhatarishe maisha yake kisa atapoteza marafiki? hivi unae mtoto kweli wewe?
 
Tupeane uzoefu wa shule tofauti ili tusifanye makosa ya kupeleka mtoto shule kwa kuambiwa na rafiki/ndugu kumbe kimeo ....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…