Atheists tulionekana wa ajabu sana!

Atheists tulionekana wa ajabu sana!

Wakuu salama, Kwanza kabisa nianze kwa kusema Elimu pekee ndio itakayomkomboa Mwanadamu katika sayari hii, Uwezo wa kutatua changamoto upo ndani yake mwenyewe, Hakuna Msaada wowote utakaotokea anga za juu kuja kusaidia hapa Dunia Hivyo Binadamu ni Mungu tosha kabisa ni Maarifa na yanazidi kupanuka na kukiweka Huru kiumbe Hichi.

Miaka kadhaa nyuma Baadhi ya sisi atheists humu tulionekana watu wa ajabu kwa imani Yetu kuwa Hakuna Mungu, Mkuu Kiranga ana thread moja imefikisha almost 3K Comments za Believers wakimshambuliwa kwa matusi nae akiwajibu kwa hoja.

Taswira ya JamiiForums sasa iko tofauti kabisa Watu kiukweli wametoka kwenye vifungo na kwa sasa wengi ni Free thinker ata kama Anaamini katika Mungu ila yuko tayari kusikiliza sera za wasio amini na kuchambua kidogo.

Tuliwahi ongea apa kwamba Mungu huyu tunaemsoma makanisani au Misikitini Hawezi kuwepo hata kwa bahati mbaya mana sifa tunazomjaza hayuko nazo hata punje. Nakaribisha mijadala zaidi.

Cc Free ideas Doyi Kiranga nusuhela @Areta ludovick Kifyatu
Moja ya mada zisizo na tija.Je ukishasema Mungu hayupo unafaidika na nini?
 
Aliyekuambia Mungu lazima kuabudiwa ni nani? Kuabudu kwako kunamuongezea nini Mungu au kumpunguzia kipi?
Nilichosema ni kwamba kila pale panapotumika neno Mungu basi kuna kuabudu na kuomba,sasa ukisema Mungu maana yake ni chanzo tu,ndio maana nikauliza kumetumika vigezo gani hadi ikapatikana tafsiri ya Mungu ni chanzo?
 
Ili uweze kuthibitisha lazima uwe na huo uthibitisho,mfano mie naweza kukuona wewe ukiiba ila nikijakuambiwa kuthibitisha nikashindwa kwa kukosa uthibitisho japo ni kweli nimeshuhudia ukiiba.
Sasa si utathibitisha kwa kile nilichoiba...
 
Nilichosema ni kwamba kila pale panapotumika neno Mungu basi kuna kuabudu na kuomba,sasa ukisema Mungu maana yake ni chanzo tu,ndio maana nikauliza kumetumika vigezo gani hadi ikapatikana tafsiri ya Mungu ni chanzo?
Ndio maana nimekuuliza ni nani aliyekuambia kuwa lazima likitumika neno Mungu lazima abudiwe? Na nimekuuliza huko kuabudu kunamuongezea kipi Mungu na kinampunguzia kipi Mungu? Kufanywa jambo na watu hakuhalalishi kuwa kifanywacho ndio uhalisia.
 
Nabado mtaonekana wa AJABU mpk dunia itakapo the end.
 
Mimi ninaamini katika mungu wa kikiristo (Mungu wa Israel),lakini nakiri mijadala ya kina Kiranga kuna hoja za msingi huwa nazinusa ,tena nyingi sana
 
Ndio maana nimekuuliza ni nani aliyekuambia kuwa lazima likitumika neno Mungu lazima abudiwe? Na nimekuuliza huko kuabudu kunamuongezea kipi Mungu na kinampunguzia kipi Mungu? Kufanywa jambo na watu hakuhalalishi kuwa kifanywacho ndio uhalisia.
Kila neno lina maana yake na matumizi yake,bila ya hivyo basi tunaweza kutumia neno lolote popote kwa tendo lolote. Ndiyo maana nikasema kila panapotumika neno Mungu basi kunafuata kuabudu na kuomba,wewe unayesema Mungu maana yake ni "chanzo" sijakubishia ila nimeuliza hiyo maana umetumia vigezo gani?

Mungu hafaidiki wala hapati hasara kwa kumuabudu au kutomuabudu.
 
Mbona unashindwa kunijubu nakuuliza ni nani aliyekuambia kuwa Mungu anahitaji abudiwe?
 
Mbona unashindwa kunijubu nakuuliza ni nani aliyekuambia kuwa Mungu anahitaji abudiwe?
Mungu sio muhitaji wa kuabudiwa,nimesema kabisa kuwa kutomuabudu hapati hasara navwala kumuabudu hapati faida.

Nimekwambia panapotumika neno Mungu basi kuna kuabudu na kuomba,ndio iko hivyo,ajabu unang'ang'ania kuniuliza nani kaniambia.

Ingekuwa vyema kwa wewe kuelezea ni vp umehusisha Mungu na chanzo au kwanini unasema Mungu ndiyo chanzo.
 
Unaposema kuwa panapotumika neno Mungu basi kuna kuabudu na kuomba sasa nimekuuliza ni nani aliyekwambia kuwa lazima Mungu abudiwe ni nani? Mazoea ya watu hakufanyi tukio kuwa ni sahihi. Kuhusu Mungu na chanzo soma post 261
 
Hakuna uwezekano wa kuprove kitu ambacho hakipo... you can't prove negative. Wanaosema yupo ndio wana jukumu la kumuonyesha alipo.... kwasababu tunaosema hayupo inatokana na ninyi kusema yupo while hamna means ya kuthibitisha....

Unasema nahisi kuna gari.. nakuuliza liko wapi, hauna means ya kuthibitisha lilipo... mimi nikisema hakuna gari nakosea nin?
Wanaosema Mungu yupo ushahidi wao eti ni nani aliumba Dunia na Viumbe vyake???? Huyo aliuviumba ndio Mungu
 
Huu ni ujinga uliyo kubuhu taka kichwani..................... Elimu gani unayomaanisha?
Utaalamu gani unafikiria..!!
FYI, hao waliokuwa na utajiri na rasilamali na awanaoongoza katika maendeleo ni watu hata darasa la saba hawakuhitimu!!
Naomba ufungue macho yako na utazame watu waliyekuzunguka wapojee..!!
au nikupe mifano chanya....?
kumwita mwenzako mjinga ni ujinga zaidi kwanini usitumie busara kujibu,au tukubaliane na kauli kwamba kila mtu ni mjinga kwa wakati wake.hata huko kulazimisha uwepo wa Mungu kwa mtoa mada wakati yeye haamini wewe ni mjinga kwake.tuheshimu imani za wenzetu ili ubora wa imani zetu utamalaki.Tusiwe walazimishi.
 
Unapo sema.hapo mwanzo kweli zungumIa hapo mwanzo..

Hapo sisi tulikuwa hatuvai nguo,mababu zetu walikuwa wanatembea uchi
So kuvaa nguo mpaka milegezo yote sio culture yetu

Hapo mwanzo sisi..mababu zetu walikuwa wakiabudu mababu zao chini ya miti nk
Huyo GOD/allah kaletwa na mashua hakuwepo huku

So kubali au kataa,,ila ukweli n kwamba hata hapo mwanzo..tamaduni zishaingiliwa na kupotea hazipo

Wao wameleta,dini,na elimu
Ni wakat wa sisi kuamka na kujitambua
anasema wametuletea milegezo anasahau pia walituletea na dini pia halafu hakumbuki kwamba mababu zetu walitembea uchi lakini hawakutamaniana makalio yao.lakini sasa baada ya dini yakuletwa kutawala makalio yanatamaniwa humo humo surualini na wengine wanayafunua wazi wazi.Tuamke
 
Unaposema kuwa panapotumika neno Mungu basi kuna kuabudu na kuomba sasa nimekuuliza ni nani aliyekwambia kuwa lazima Mungu abudiwe ni nani? Mazoea ya watu hakufanyi tukio kuwa ni sahihi. Kuhusu Mungu na chanzo soma post 261
Katika hiyo post umesema chanzo cha ulimwengu ndiyo Mungu,nachouliza mie kwamba ni kwanini umetumia neno Mungu na si neno lengine? maana matumizi ya hilo neno Mungu ni tofauti na ulichoeleza.

Mfano neno sayansi lina maana yake hivyo matumizi ya neno sayansi yataendana na maana ya hilo neno,sasa mtu akisema sayansi ni uchawi tutauliza kwanini aseme sayansi ni uchawi?

Sasa mimi nakwambia kile kinachoabudiwa huitwa Mungu,wewe unaniuliza nani kasema? kwani wewe hiyo maana ya Mungu ni chanzo cha ulimwengu ni nani kasema?
 
Wa yeye mwenyewe...
Ndiyo maana nikasema yeye ndiye muumbaji maana ili kiwepo kilichoumbwa lazima awepo muumbaji,sasa ikiwa Mungu yeye pekee ndio muumbaji sasa tutasemaje kuna muumbaji mwengine?
 
Back
Top Bottom