Atheist wengi hawajui wanachokitafuta

Ameshakuwekea njia ya kupita ya kwenda peponi na nyingine ya motoni, yes ukichagua ya kwenda motoni basi anataka akakuchome.

Kwanini mungu kaweka moto kwaiyo mungu hataki watu wote waende peponi??

Mungu alishindwa kuwafanya wote waingie peponi bila kuweka kizuizi cha moto??
 
Amekwambia ukiasi utaenda motoni, na amekwambia ukitii utaenda peponi. Sasa wewe unataka kufanya lipi?

mungu kaumba kiumbe dhaifu huku akijua kua udhsifu wa kiumbe hicho kinaweza kufanya mambo yaliyo kinyume na yeye, amejua kua hicho kiumbe hakina uwezo wa kujibadili kisiwe dhaifu mpaka yeye apende lakini hajapenda.

Maana yake karuhusu binadamu aweze kufanya yaliyokinyume naye. Hicho kiumbe kimefanya vile vile kama alivyotaka ( asingetaka angerekebisha kwasababu alijua madhara ya udhaifu na effect zake zikoje)

badala ya mungu kuridhika na matendo ya huyo kiumbe ya kukosea, ambacho alikiumba kikiwa na uwezo wa kukosea alioutaka yeye uwe yeye anakiadhibu kwasababu zipi??

Kwamba hapendi makosa yaliyofanywa na kiumbe wake?? Hapana ni lazima apende kwasababu alitaka kiumbe huyo akosee maana alimuumba akiwa na udhaifu wenye kusababisha kiumbe huyo kukosea

Kwamba anamuadibu huyo kiumbe kwasababu kiumbe amekuwa tofauti na mungu alivyotegemea??? Lakini hapana maana huyu mungu alijua kila kitu kitacho fanyika kabla hakija fanyika

Au alijua hilo ila hakuwa na uwezo wakufanya jambo hilo liende kama atakavyo?? Lakini pia ni muweza wa yote alikua na uwezo wa kufanya jambo hili liende kwa namna ambavyo anataka

Bila shaka jambo hili limetokea kama alivyotaka, sasa point ya kuadhibu kiumbe chake inamashiko gani?? Huyu mungu anajitekenya halafu anacheka mwenyewe
 
Kwa ufupi ni hivi; elimu ya Mungu, ujuzi wake na maarifa yake ni tofauti na sisi binadamu.

unajuaje kwamba ujuzi wake ni tofauti na binadamu na sio kwamba ni tofauti kwasababu hayupo na ndio maana hathibitishiki nje ya hadithi???

ndiyo nakubali huwezi ukajua itavyokua kwasababu ni kitu kipya kwako

Lakini kwa Mungu hiyo siyo case! Kwa sababu maarifa yake, ujuzi wake na elimu yake unao uwezo wa kuona hayo yote!

hapa sijaelewa, unamzungumzia mungu au mtu?

Hatua kwa hatua na jinsi mwanzo utakavyokuwa na jinsi mwenendo wa kitu utakavyokua na hatma yake itakuwa ni ipi.

hapa bado sijaelewa anayezungumziwa kati ya mtu na mungu

Mwanadamu amepewa uhuru wa kufanya mambo na katika hilo Mungu hamuingilii binadamu

uhuru huo katika mambo gani?

ana muacha binadamu afanye atakavyo. Kama binadamu A akiingia motoni na binadamu B akaingia peponi lawama usimrushie Mungu kwa vile tayari ameshaandika A ni wa motoni na B wa peponi.

mungu ameandika A ni wamotoni inamaana tayari huyu A hana uhuru wakuchagua aende peponi alikoenda B


kwa maana hiyo mungu akijua kesho nitatenda dhambi nina uhuru wakubadili nisitende dhambi??

Tunachofeli ni kwamba God's thinking tunaiweka daraja moja na human's thinking pasipo kujua kwamba binadamu hawezi Ku' think kama Mungu. Kwa sababu binadamu tupo kwenye specific spot in time. Tunachogundua sisi ni kwa kupitia tuliyoyapitia.
Kwa kusema tu "tunafeli" kunathibitisha kua mungu mjuzi wa yote muweza wa yote na mwenye upendo wote hayupo. Angekuwepo kufeli kusingekuwepo wala hata kuhojika na wote tungeweza kufanya mambo bila kufeli.

Maana katika ulimwengu wenye huyo mungu hakutakiwi kua na imperfection yeyote kama kufeli.

Lakini Mungu yupo nje ya time. Anaona mwanzo utakuaje, na anaona na mwisho utakuaje. That's why tayari ameshaandika kila kitu na hatma ya hivyo vitu vitakuaje.
thibitisha mungu yupo
 
Ndio maana nikasema nyie mnaangaika bureee maana kila kitu Mungu alishakiandika kuwa utakula tumba ngapi za mchele utake au usitake uwezi zidisha wala punguza tumba hizo za mchele, hivyo hivyo ata uruke uruke vipi kama Mungu kaandika wa motoni hakuna wa kukupeleka peponi , hivyo huwezi badili chochote
 
Unauliza maswali ya kitoto sana. Mola wetu anajua hata kile ambacho hakipo laiti kingekuwepo anajua vipi kingekuwa.

Yeye ndio anaumba na yeye ndio analea,ujuzi wake ni kamilifu.
kila kitu Mungu wenu alishaandika yeye vip amilazimishe mswali mara mtubu , wakati mwisho wa watu hao anaujua ? huku ni kujitekenya kisha kucheka mwenyewe
 
Kwani mbona wewe unatokwa mishipa humu kusema hakuna Mungu kwani kama kitu hakipo si hakipo na kila mtu anaona kiwa kweli hakipo sasa kuna haja gani wewe kutwa kubishana na watu kuwa hakuna Mungu?
Nabishana na watu kwa sababu uwezo wao naumudu lakini Mungu wako muweza wa yote vip asijitokeze yeye kila siku anamitoa nyinyi chambo mpaka mnatia huruma humu
 
Nilichokiona ni unaandika ili uandike; yaani unabetua betua maneno.

Nilichokifafanua ni kuhusu pre destiny! Na ndiyo sababu iliyonifanya nikoti comment yako. As kama kawaida ukabetua maneno ukarukia kwenye tawi jengine.

Umenitaka nithibitishe kama Mungu yupo? Ili nikujibu swali lako nithibitishie wewe kwanza kama Mungu hayupo.
 
kila kitu Mungu wenu alishaandika yeye vip amilazimishe mswali mara mtubu , wakati mwisho wa watu hao anaujua ? huku ni kujitekenya kisha kucheka mwenyewe
Ujinga kweli ni giza.

Ni lazima utii na utubu kwa yule ambae amemuamini na kuamua kumtii,ila wewe kama hujamuamini hizi amri hazikuhusu mzee.

Mola wetu usipomjua huwezi kumuelezea,yaani hapa unachokiuliza ni ujinga ambao hata mtoto hawezi kuuwaza na maswali yako yanaonyesha ni kwa jinsi gani humjui.

Kitu ambacho hukijui ni kuwa kujua kwa ni katika elimu na utendaji yaani kujua kuliko kamilika na kujua kule hakumzuii mwanadamu kufanya alitakalo.
 
Nimekuuliza swali nataka majibu kama huwezi kili kwamba umeshindwa kuthibitisha mungu yupo ili nami nikuthibishie kua hayupo
 
Badala ya kujibu swali unaanza maelezo wala yasiyo takiwa
1 . Swali ni hili , vip Mungu wenu amiambie mtubu mara mswali wakati anafahamu kabisa kuwa ni wakina nani wataingia peponi na wakina nani wataingia motoni ? wewe uoni kuwa Mungu wako anafanya utoto
 
Soma vizuri jibu humo na hukufundishwa kusoma huku unatafakari hilo ni tatizo lako na wakubwa zako.

Tuendelee...!
 
Na hapo ndipo unapokosea! Yaani laiti ungelitumia akili kidogo tu ungelinielewa.

Binadamu yupo ndani ya uzio unaoitwa muda. Hakuna chochote atakachokijua zaidi ya experience aliyopitia.

Hatua ya utungaji mimba kwa binadamu upo ndani ya muda! Hatua ya ukuaji wa binadamu tangu kuwa mtoto mpaka mtu mzima yapo ndani ya muda.

Hiyo hali/hatua ya matukio juu ya matukio ambayo kwa ujumla yanachukua mwenendo wa maisha ya binadamu yapo ndani ya muda.

Hayo yoooote unayoyaandika sijui utakula pumba ngapi za mchele yapo ndani ya muda.

Mungu yupo nje ya ring/circle ya muda! Hiyo inamfanya haoni mambo hatua kwa hatua au kipindi kwa kipindi au tukio baada ya tukio. Mungu kwake kuyaona hayo matukio baada ya matukio yaliyobeba mwenendo mzima wa maisha ya binadamu, Mungu anayaona kwa wakati mmoja tu! Kwa sababu yupo nje ya muda!

Kwa hiyo mwenendo wako woooote wa maisha, utakachofanya na ambacho hutokifanya tayari Mungu alishaona kiona. Kwa hiyo pre destiny yako yote Mungu anayo.

Kwa hiyo Mungu kuijua pre destiny yako haimaanishi kwamba ameshakuhukumu, hapana! Bali alishakuona kabla mwenendo wako wa maisha utakavyokua.
 
Nimekuuliza swali nataka majibu kama huwezi kili kwamba umeshindwa kuthibitisha mungu yupo ili nami nikuthibishie kua hayupo
Na mimi nimekuuliza swali nataka majibu. Kama huwezi kiri kwamba umeshindwa kuthibitisha Mungu hayupo ili nami nikuthibitishie kua yupo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…