Atheism: Imani nusu na robo

Atheism: Imani nusu na robo

Nitajie wewe hilo baya japo moja ambalo mtu anaweza kutumia kitabu cha kufanya baya hilo.
Lolote utakaloweza kulifikiria.

Kwa nini unataka kunifunga kwenye moja wakati nishakwambia lolote utakaloweza kulifikiria?
 
Sijajibu kvp?

Hujaeleza sababu ya kueleweka aliyokuwa nayo huyo Mungu wako kufanya alichofanya.

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kutokea wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kuwepo?
 
Lolote utakaloweza kulifikiria.

Kwa nini unataka kunifunga kwenye moja wakati nishakwambia lolote utakaloweza kulifikiria?
Mi sijui baya lolote ambalo unaweza kulifanya kwa kutumia kitabu cha dini.
 
Hujaeleza sababu ya kueleweka aliyokuwa nayo huyo Mungu wako kufanya alichofanya.

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kutokea wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kuwepo?
Kufanya alichofanya nini?
 
Mi sijui baya lolote ambalo unaweza kulifanya kwa kutumia kitabu cha dini.
Hata hujaelewa nilichoandika.

Ndiyo maana inakuwa tabu hapa.

Nikichokuambia si kwamba ufikirie baya ambalo unaweza kulifanya kwa kutumia kitabu cha dini.

Nimekwambia baya lolote utakaloweza kulifikiria, unaweza kulifanya kwa kutumia kitabu cha dini.

Ushaelewa?
 
Nini kiliwakuta Mkuu mpaka mkaacha na upadr. Mm niliishi ktk ukristo zaid ya miaka ishirini km mu anglican mwisho nikaachana nao baada ya kuuanza kutafuta elimu zaid niligundua vtu ambavyo nilishindwa kujibiwa

hakika elimu ni kitu muhimu sana

Utafutaji wa facts. Sipendi kuweka assumptions kama sijajua wote wanasema nini. Pia kuna vitu haviungani na shahidi za kisayansi na tafiti za miaka hii. Mfano creation.
 
Nilishasema humu ,"HAKUNA MUNGU NA KAMA YUPO SIO HUYU MUNGU WA WAKRISTO,WAISLAM,BUDHA,HINDUISM ,JEWISH. N.k

I agree with you.

But katika imani hizo za miungu toa Buddhism. Sio imani kuhusu mungu wala miungu. It does not teach anything about God na hakuna concept ya God au creator. Even Buddha himself said he is not a God but a teacher. Na katika mafundisho yake there is nothing about god or who is god.

It is the Agnosticism philosophy.

(Sitetei imani yoyote bali kuweka sawa ujumbe wako usijumuishe kila imani katika paradigm sawa)
 
Kufanya alichofanya nini?

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kutokea wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kuwepo?
 
Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kutokea wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kuwepo?
Kwasababu aliona kuwa kila alichokiumba ni chema, kama wewe unaona kuwa kuna makosa Katika uumbaji basi umeamua kufanya hivyo mwenyewe kwasababu akili yako hushikiwi na mtu, huna uwezo wa kumfanya mtu yeyote aamini kila unacho kiamini wewe.
 
Hata hujaelewa nilichoandika.

Ndiyo maana inakuwa tabu hapa.

Nikichokuambia si kwamba ufikirie baya ambalo unaweza kulifanya kwa kutumia kitabu cha dini.

Nimekwambia baya lolote utakaloweza kulifikiria, unaweza kulifanya kwa kutumia kitabu cha dini.

Ushaelewa?
Ndiyo nikakwambia nitajie japo moja hilo baya ambalo unaweza kulifanya kwa kutumia kitabu cha dini. Mie napingana na wewe kuwa unaweza kufanya jambo baya kwa kutumia kitabu cha dini,labda wewe utakuwa unazungumzia watu kufanya mambo mabaya na kuzingizia vitabu vya dini lakini sio kwamba kitabu cha dini kinampa mtu ruhusa au kumuelekeza MTU kufanya jambo baya. Lakini pia inawezekana tunatofautiana kwenye kujua ni jambo lipi baya.

Muda si mrefu umetoka kusema kusema kuwa kuna watu hawaamini mungu ila bado wapo kwenye dini kwa sababu tu wanaona dini ina umuhimu kwa kuwa ina mafundisho mazuri na kukataza mabaya,sasa tena hapa unasema mtu anaweza kufanya mabaya kwa kutumia vitabu hivyohivyo vya dini na ndiyo maaana nikakwambia unitajie hilo baya japo moja lenye kufanyika kwa kutumia kitabu cha dini.
 
Wewe una tatizo la kusoma na kushindwa kuelewa ulichokisoma.
Yawezekana ikawa kweli endapo utanionesha ni wapi niliposhindwa kuelewa ila vinginevyo yawezakuwa ni muendelezo wa tatizo lako la kusingizia watu mambo.
 
Mi sijui baya lolote ambalo unaweza kulifanya kwa kutumia kitabu cha dini.
Hujaelewa hata tofauti ya "baya lolote unaloweza kulifikiria" na "baya lolote unaloweza kulifanya kwa kutumia kitabu cha dini"

Comprehension please.

Ndiyo maana hatuelewani, huna comprehension.
 
Back
Top Bottom