Stavros Myles
JF-Expert Member
- Jun 7, 2020
- 350
- 390
Natoa Hai kwa wanajukwaa was Jf. Ni matumaini yangu ya kwamba muwazima wa aftya tele.
Natoa shukurani zangu nyingi kwa muumba mbingu,dunia na vitu vyote vinavyouzunguka ulimwengu ambaye ni Mungu. Shukurani nyingine zimuendee muanzilishi wa forum hii bw. Maxence Melo
Baada ya maneno machache ya utangulizi ningependa nizungumzie suala ambalo limenisukuma kutoa mawazo yango kulihusu. Hapa nazungumzia athari za mitandao ya kijamii kwa jamii.
Kwa hivi karibuni dunia imeshuhudia maelfu ya apps zinachowekwa App store,Playstore na sehemu nyingine nyingi za kusambazia Apps hizo. Miongoni mwa Apps pendwa ni apps za mitandao ya kijamii kama Facebook,Twitter,Snapchat, Instagram n.k.
Wimbi kubwa limejikuta likitumbukia kwenye matumizi ya mitandao hiyo ya kijamii, shida sio idadi ya watu wanaotumia mitandao husika bali ni athari wanazozipata kupitia mitandao husika.
Kabla ya yote ninakiri ya kwamba wanaotumia mitandao ya kijamii wengi hawana hata elimu ya jinsi ya utumiaji sahihi wa mitandao hiyo. Kuna mfano hai ambao nimewahi kukumbana nao yapata miezi miwili iliyopita, mmoja wa aliyekuwa rafiki wa dada yangu alikuwa ametuma picha yake akiwa amekaa juu ya kitanda chake, alikaa pozi la hasara hasara tu na hata skirt fupi aliyoivaa ilikuwa inayakimbia magoti na kukifuata kiuno. Picha hiyo aliituma facebook mwaka 2014 na mpaka hivi leo bado inatumika na wahuni wanaotapeli watu wakiwadai wamtafute (wanatumia picha kuwahadaha watu) huko WhatsApp. Sijui kama mhusika alifanya ivyo (ku 'post') akijua ya kwamba kitu kikiingia mtandaoni kutoka ni jambo la kusahau.
Ngoja tuachane na huyo dada, inawezekana ulipokuwa unapitia mfano wa dada huyo ulijiona upo salama kabisa, lakini nataka nikutaadharishe na kukuambia bado endelea kusoma.
Kama wewe ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii unaweza kuwa tayari umekumbwa na athari hizi au ndo unaianza safari ya kukumbana na athari hizi nitakazoziandika hapa chini.
1.Kutumia muda mwingi mtandaoni.
Inawezekana unapoanza kufungua 'notification' yoyote ya mtandao husika wa kijamii unajiapiza kuwa utaangalia hiyo 'notification' na kuendelea na mambo yako mengine. Lakini hali inakuwa tofauti baada ya kufungua tu App na kuangalia 'notification' husika unajikuta tu licha ya kutoona ujumbe wowote uliotumiwa unafungua sehemu ya 'message' ,unahamia upande wa 'newsfeed' na kwingineko kwingi. Baada ya muda unajikuta tayari upo kuitazama video iliyopita kwenye macho yako.
2.Msongo wa mawazo.
Mitandao ni kama bomu la nyuklia ambalo linatafuta sehemu ya kulipukia, bomu hili kubwa lipo tu na utayari wake wa kulipuka ndio unaotia mashaka. Inawezekana hata sasa wewe ndiye unayelipukiwa na bomu hili.
Kila mtu yeyote anapo 'post' kitu chochote iwe picha, faili, maneno ,status au hata video anatarajia kupata idadi kubwa ya watu watakaotazama vitu vyake, na hii inapelekea kila baada ya dakika kadhaa mhusika (aliye 'post') kufungua mtandao husika (app) na kutazama na kujua amepata shares, comments au likes (+reactions) kiasi gani (idadi).
Mambo yanakuwa mabaya haswa pale ambapo mhusika anapokhja kugundua ya kwamba ni watu wanne tu ndio walio 'like' kitu alichokuwa ameki 'post'. Kuna hali ga kuanza kujiuliza je kuna nini ambacho akikiposti kitapelekea apate likes nyingi. Wengine hujikuta wanaanza kupoteza hata furaha, nuru katika nyuso zao inapotea kabisa. Na hali kama itaendelea inaweza kumsababishia mhusika kuwa na msongo wa mawazo.
3.Utamaduni wa ovyo kusambaa.
Kuna video mbalimbali zinazopandishwa katika mitandao ya kijamii. Na kutokana na malezi ya ovyo au hata kuwa na access ya vitu vingi vya mtandaoni kwa watoto hata ambao hawana uwezo wa kuchuja tabia fulani fulani wanazoiona kwenye apps au tovuti za mitandao ya kijamii, dimbwi kubwa linawameza watoto hao na mwisho wa siku wanaiga tamaduni za ovyo ovyo.
Hali hii inasambaa hata kwa watu wazima ambao wamejikuta wakishadadia mambo ya ovyo, lakini sababu ya msingi imekuwa ni kwamba aliona msanii fulani kutoka marekani amefanya naye anafanya.
Kuna mabinti wengi wamejikuta wakijiingiza kwenye shughuli za ngono ilimradi wawezw kukidhi matamanio yao ya kuvaa kama Rihanna,Beyonce, Lily Kim na wengineo wengi. Hata kwa upande wa wanaume mambo ni mabaya mno, kuna idadi kubwa ya wanaume wanaojikuta wanatamani kufanya mapenzi kinyume na maumbile.
Si kwamba hawajui wanachofanya ni kitu cha ovyo, ila baada tu ya kuona jamii ya mashoga huko Insta au hata mitandao mingine wanajipa moyo na kujizamisha mazima kwenye uchafu huo.
4.Kupoteza pesa
Kwa wafanya biashara wengi ambao wanataka jumbe au matangazo yao yasomwe na wengi wamejikuta wakitumia njia ya kufanya matangazo katika apps au sites hizo za kijamii (sponsored Ads). Wote wanafanya ivyo ili kujipatia traffic. Lakini hali ni mbaya zaidi kwa upande wa watu wa kawaida ambao hata hawana jambo la msingi wanalotuma mitandaoni, unakuta ni sikukuu ya sherehe ya kuzaliwa lakini mtu analipia mpaka pesa atume tangazo la posti yake hiyo (sponsored Ads) ili iwafikie watu wengi, sasa unajiuliza waki 'like' wafu 10 elfu posti yangu nita achieve nini? unakuta hauna jibu lolote sahihi.
Kuna wengine wengi ambao wao wako radhi waunge bando ili wawepo mitandaoni bila hata ya kuwa na issue ya msingi. Yaani mtu anakubali awe anachoma 3000/= kwa wiki ili aweze kutazama insta stories za public figures na posti za umbea ,,,
Kwa leo naishia hapa kama una mchango wako kuhusu athari nyingine nyingi ambazo unazifikiri tafadhari ziandike at least watu wajifunze.
Duarte