Athari za Marafiki katika Mahusiano ya Kimapenzi

Nicas Mtei

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2010
Posts
11,556
Reaction score
7,106
black-couple-arguing.jpg

Mu hali gani mabibi na mabwana wa humu MMU? Ni matumaini yangu kuwa wote humu mu wazima wa afya. Kwa mara nyingine leo nimeona bora tuzungumzie suala zima la athari za marafiki katika mahusiano...

Katika mahusiano ya mapenzi yoyote kuna watu wanaitwa MARAFIKI. Kabla sijaendelea sana ni vizuri kujiuliza kuna umuhimu gani wa kuwashirikisha marafiki katika mahusiano yako? Mahusiano mangapi yamevunjika kwa sababu ya marafiki ingawa kuna mahusiano yaliyojengwa na marafiki japokuwa ni machache kuliko yale yanayovunjika.

Kuna baadhi ya watu hawawezi kufanya kitu chochote na mpenzi wake bila kumshirikisha rafiki lakini swali la kujiuliza, mwisho wa mazungumzo yenu anakusaidia nini?

Ndio hatukatai kuwa katika group la marafiki huwa kuna story za aina mbalimbali lakini si vema kuongea mambo ya ndani ya kwako na mwenza wako kwa rafiki kwasababu dunia ya sasa kumpata rafiki wa kweli ni vigumu sana tena sana.

Naongea hivyo kutokana na baadhi ya suhuda nyingi ambazo nimekuwa nikikutana nazo kutoka kwa watu tofauti tofauti, kuwa marafiki wamekuwa ni chanzo kikubwa cha mahusiano kuvunjika ama kwa kutengeneza uongo kutoka pande moja kwenda pande nyingine, au kwa kumchukua kabisa mpenzi wa mwenzake na hii inategemea na mazingira au msimamo mliojiwekea nyinyi wapenzi.

Kuna baadhi ya mahusiano huwa yanakuwa imara sana kutokana na misimamo ya wahusika, mtu huwezi kusikia jambo linalomhusu mwenzi wako halafu ukachukua hatua moja kwa moja au kununa au kupoteza kabisa mawasiliano.

Mtafute umuulize au chunguza kwanza. Nimewahi kushuhudia rafiki wa karibu akijaribu kuharibu penzi la rafiki yake eti tu kwa sababu anaona anapata mafanikio au kwa sababu nyingine ambazo anazijua yeye. Anataka amtafute mtu wa pembeni, ampe namba ya mpenzi wa rafiki yake halafu amtukane na amwambie aachane na rafiki mtu.

Hivi hii yote ili iweje? Sana sana unakuwa unajishusha. Naamini siku zote wivu unaotakiwa ni ule wa maendeleo lakini siku hizi marafiki wana vitu vya ajabu ajabu huo unaitwa urafiki wa KICHINA.

Fanya mambo yako wewe kama wewe marafiki ndio wapo, lakini sio wa kuongea nao kitu chochote kuhusu mahusiano yako au hata matarajio ya maendeleo yako wengine wakiona unafaidi/unafanikiwa sana wanaweza kufanya njia yoyote kukufunga hata kwenda kwa waganga wa kienyeji kwa wenye imani hizo ili tu uharibikiwe hiyo ndo furaha yao.

KUWA MAKINI NA MARAFIKI HASA KWENYE MAHUSIANO.

Si lazima umshirikishe katika kila jambo, siku hizi marafiki wa kweli ni wachache sana....

Nawatakia sabato na Week end njema

Naona unakuja kwa kasi unataka kumpiku mzee Mtambuzi..
Asante kwa mada..na washahili wanasema kikulacho ki nguoni mwako.
 
Last edited by a moderator:

hahhahaha.... Mzee Mtambuzi yeye nimemwachia uchambuzi wa kesi na mikasa ya kimaisha.... mimi najikita kwenye ushauri wa kimapenzi kwa sasa....
kuwa makini na marafiki zako
 
Well said.. Kwa ushuhuda wangu hii inatokea zaidi kwa kina'SHE', na huwa wanapinduana kweli.. Hilo la kuendeana kwa waganga kuna bidada mmoja namfaham kidogo angekua 'ndondocha', maombi ndo yalimsaidia..
 
Nadhani huu ujumbe utawasaidia sana wanawake, asilimia kubwa ya wadada mahusiano yao huendeshwa na marafiki zao.
Mathalani, wataalam wa sanaa ya utongozaji huwa wanasema katika kundi la wanawake marafiki, kama mwanaume anayo nia ya "kumtokea" mdada mmojawapo basi lazima ahakikishe ameiteka mioyo ya marafiki zake pia hususani yule kiongozi wa kikundi.
 
Marafiki katika jamii ndio sisi wenyewe wana jamii. Wana faida na hasara zake... Na yote hutegemea wewe uliye katika mahusiano wawachukulia vipi, umewapa nafasi ipi na umuhimu upi katika mahusiano yako.

Marafiki siku zote lolote lile analokuwambia kuhusu mtu wako chukua hizo habari changanya na zako. Kuna wakati huwa ni watu wazuri sana kwa "your well being" na kuna wakati hawafai na ni nyoka kabisa kwa mahusiano hayo hayo. Yote hiyo ikitokana na kwamba level za kirafiki baina ya watu kumepishana... Kwani kuna marafiki ambao ni wa dhati na niya njema juu yako na wale ambao ni huwa na wivu juu yako bila wewe kujua ama kwa kujua.

Faida za Marafiki katika mahusiano.

Mara nyingi ndiye mtu ambae anakuwa nakujua vema, na tokana na tabia za wanadamu wengi za ku confide kwa watu wao kwa karibu inakuwa rahisi kwa yeye kujua kila kitu kuhusiana na mahusiano hayo. Kwa hiyo ukibahatika ukapata rafiki wa kweli mwenye kukupenda kwa dhati; inamfanya kuwa protective hasa katika kuhakikisha kuwa hauumizwi kwenye mahusiano hayo kwa njia hizi (tegemeana na nguvu na uhodari wa rafiki huyo);

  • Atahakikisha kuwa anamuangalia kwa karibu mpenzi wako na kumuonya hasa katika sehemu ambazo huyo mpenzi wako anaonyesha kutaka kutereza.
  • Yeye hayuko blinded na feelings za mtu wako... Hilo linamfanya kwa kiasi kikubwa kuona ukweli kuliko wewe rafiki yake. Kuwa huyo mtu anakufaa na kuwa labda hakufai hivo taratibu kuanza namna ya kukunasua katika huo mtego.
  • Mara nyingi ndiyo mshenga wa kutuma ujumbe, kutoa taarifa hasa katika masuala ya dharula kama magonjwa, msiba, matatizo n.k. Anakuwa ndiye anajua mtu wako ampate vipi.
  • Kama mtu wako ni mtu mwema na anakufaa, atajitahidi kwa kila namna kuhakikisha unadumu nae, ndiye atakae kurudisha ukiwa na hasira, ndiye atakae kukumbusha mema ya mpenzi huyo. Ndie atakae kuonyesha jinsi gani maybe you are being selfish and all.
  • Rafiki ndie ambae ni rahsi kumlilia begani pale mahusiano yako yamekoma kwa kupenda ama bila kupenda... Sababu una uwezo wa kusema lolote baya, zuri, tusi juu ya ex wako na akakuelewa kwa rahisi zaidi ya yeyote. Bila kujalisha huyo ex ni looser ama siyo.

Hasara za Marafiki katika Mahusiano;

  • Anakujua vema... Mabaya na mazuri yote. Yeye kama ana niya mahusiano yako yasifanikiwe, kwa kiasi kikubwa hayawezi fanikiwa. Yeye kama rafiki yako wa karibu (pengine hata huwa unamuambia mpenzi wako hakunaga rafiki kama huyu); akipeleka habari ya kusukwa (au ya kweli but damaging) yoyote ile kwa mpenzi wako mahusiano yaweza kuwa yawalakini. Ni wapenzi wachache watathubutu kukuambia aliloambiwa...
  • Yeye ndiye huwa unamuambia sifa zote za Mpenzi wako... Nini anapenda, nini anachukia, vipi anaridhishwa, vipi alivyo na masifa mengine kem kem. Sifa hizo mara nyingi humjengea njia ya moja kwa moja kujenga ukaribu na mpenzi wako huku akileta habari na maongezi ambayo anajua fika ndiyo anapenda kusikia mtu wako. Mwisho wa siku mtu wako anaanza kutafakari pengine s/he chose the wrong person wa kuwa nae na huyo rafikiyo ndiyo alistahili.

Ukweli unabaki... Marafiki ni muhimu katika mahusiano ila wasiwe wao ndio waamuzi wa what is right and wrong for you. Hakikisha kuwa daima unafuata nini unataka, hakikisha kuwa their is a line ya nini ajue na nini asijue na hakikisha kuwa siyo lazima awe too close na mtu wako. Mara nyingi ni inappropriate. Hayo ndiyo mawazo yangu.

Nicas, mada nzuri. Asante.
 
Nicas Mtei,safi

Marafiki wakiruhusiwa kuingia deep sana katika maisha yako wanaweza kuwa tatizo na inategemea pia aina ya Marafiki ulio nao.binadamu huwa wanabadilika.Jambo la muhimu ni kutowaruhusu sana waingie hadi kwenye mambo ambayo ni too senstive kwako na patna wako
AshaDii umefanya tathmini nzuri
 
Last edited by a moderator:
Ukweli unabaki... Marafiki ni muhimu katika mahusiano ila wasiwe wao ndio waamuzi wa what is right and
wrong for you. Hakikisha kuwa
daima unafuata nini unataka,
hakikisha kuwa their is a line ya nini ajue na nini asijue na hakikisha kuwa siyo lazima awe too close na mtu wako. Mara nyingi ni inappropriate. Hayo ndiyo mawazo yangu.

Dada Ashadii nashukuru kwa mchanganuo wako. Umeandika mambo muhmu sana na yanayofunza. Nimepapenda hapopa blue.
 
Nicas Mtei,safi

Marafiki wakiruhusiwa kuingia deep sana katika maisha yako wanaweza kuwa tatizo na inategemea pia aina ya Marafiki ulio nao.binadamu huwa wanabadilika.Jambo la muhimu ni kutowaruhusu sana waingie hadi kwenye mambo ambayo ni too senstive kwako na patna wako
AshaDii umefanya tathmini nzuri

Asante Ben... Nakubaliana pia na muono wako. Kuwa na weekend njema.
 
Nicas Mtei,safi

Marafiki wakiruhusiwa kuingia deep sana katika maisha yako wanaweza kuwa tatizo na inategemea pia aina ya Marafiki ulio nao.binadamu huwa wanabadilika.Jambo la muhimu ni kutowaruhusu sana waingie hadi kwenye mambo ambayo ni too senstive kwako na patna wako
AshaDii umefanya tathmini nzuri

Kweli kaka. Ni vyema kuweka mipaka katika urafiki. Kinyume na hapo waweza lia.
 
Last edited by a moderator:
Marafiki katika jamii ndio sisi wenyewe wana jamii. Wana faida na hasara zake... Na yote hutegemea wewe uliye katika mahusiano wawachukulia vipi, umewapa nafasi ipi na umuhimu upi katika mahusiano yako.

Marafiki siku zote lolote lile analokuwambia kuhusu mtu wako chukua hizo habari changanya na zako. Kuna wakati huwa ni watu wazuri sana kwa "your well being" na kuna wakati hawafai na ni nyoka kabisa kwa mahusiano hayo hayo. Yote hiyo ikitokana na kwamba level za kirafiki baina ya watu kumepishana... Kwani kuna marafiki ambao ni wa dhati na niya njema juu yako na wale ambao ni huwa na wivu juu yako bila wewe kujua ama kwa kujua.

Faida za Marafiki katika mahusiano.

Mara nyingi ndiye mtu ambae anakuwa nakujua vema, na tokana na tabia za wanadamu wengi za ku confide kwa watu wao kwa karibu inakuwa rahisi kwa yeye kujua kila kitu kuhusiana na mahusiano hayo. Kwa hiyo ukibahatika ukapata rafiki wa kweli mwenye kukupenda kwa dhati; inamfanya kuwa protective hasa katika kuhakikisha kuwa hauumizwi kwenye mahusiano hayo kwa njia hizi (tegemeana na nguvu na uhodari wa rafiki huyo);

  • Atahakikisha kuwa anamuangalia kwa karibu mpenzi wako na kumuonya hasa katika sehemu ambazo huyo mpenzi wako anaonyesha kutaka kutereza.
  • Yeye hayuko blinded na feelings za mtu wako... Hilo linamfanya kwa kiasi kikubwa kuona ukweli kuliko wewe rafiki yake. Kuwa huyo mtu anakufaa na kuwa labda hakufai hivo taratibu kuanza namna ya kukunasua katika huo mtego.
  • Mara nyingi ndiyo mshenga wa kutuma ujumbe, kutoa taarifa hasa katika masuala ya dharula kama magonjwa, msiba, matatizo n.k. Anakuwa ndiye anajua mtu wako ampate vipi.
  • Kama mtu wako ni mtu mwema na anakufaa, atajitahidi kwa kila namna kuhakikisha unadumu nae, ndiye atakae kurudisha ukiwa na hasira, ndiye atakae kukumbusha mema ya mpenzi huyo. Ndie atakae kuonyesha jinsi gani maybe you are being selfish and all.
  • Rafiki ndie ambae ni rahsi kumlilia begani pale mahusiano yako yamekoma kwa kupenda ama bila kupenda... Sababu una uwezo wa kusema lolote baya, zuri, tusi juu ya ex wako na akakuelewa kwa rahisi zaidi ya yeyote. Bila kujalisha huyo ex ni looser ama siyo.

Hasara za Marafiki katika Mahusiano;

  • Anakujua vema... Mabaya na mazuri yote. Yeye kama ana niya mahusiano yako yasifanikiwe, kwa kiasi kikubwa hayawezi fanikiwa. Yeye kama rafiki yako wa karibu (pengine hata huwa unamuambia mpenzi wako hakunaga rafiki kama huyu); akipeleka habari ya kusukwa (au ya kweli but damaging) yoyote ile kwa mpenzi wako mahusiano yaweza kuwa yawalakini. Ni wapenzi wachache watathubutu kukuambia aliloambiwa...
  • Yeye ndiye huwa unamuambia sifa zote za Mpenzi wako... Nini anapenda, nini anachukia, vipi anaridhishwa, vipi alivyo na masifa mengine kem kem. Sifa hizo mara nyingi humjengea njia ya moja kwa moja kujenga ukaribu na mpenzi wako huku akileta habari na maongezi ambayo anajua fika ndiyo anapenda kusikia mtu wako. Mwisho wa siku mtu wako anaanza kutafakari pengine s/he chose the wrong person wa kuwa nae na huyo rafikiyo ndiyo alistahili.

Ukweli unabaki... Marafiki ni muhimu katika mahusiano ila wasiwe wao ndio waamuzi wa what is right and wrong for you. Hakikisha kuwa daima unafuata nini unataka, hakikisha kuwa their is a line ya nini ajue na nini asijue na hakikisha kuwa siyo lazima awe too close na mtu wako. Mara nyingi ni inappropriate. Hayo ndiyo mawazo yangu.

Nicas, mada nzuri. Asante.

Mambo yangu ya mahusiano naweza kuhandle mwenyewe, urafiki upo kwangu na wala siyo kwa mpenzi wangu. Huwezi ukawa rafiki yangu halafu ukawa untaka kuwa rafiki wa mke/mpenzi wangu. Siruhusu hicho kitu.
 
Nadhani huu ujumbe utawasaidia sana wanawake, asilimia kubwa ya wadada mahusiano yao huendeshwa na marafiki zao.
Mathalani, wataalam wa sanaa ya utongozaji huwa wanasema katika kundi la wanawake marafiki, kama mwanaume anayo nia ya "kumtokea" mdada mmojawapo basi lazima ahakikishe ameiteka mioyo ya marafiki zake pia hususani yule kiongozi wa kikundi.

Na hiz habari za saluni umbeya zinatuponza..
 
Mambo yangu ya mahusiano naweza kuhandle mwenyewe, urafiki upo kwangu na wala siyo kwa mpenzi wangu. Huwezi ukawa rafiki yangu halafu ukawa untaka kuwa rafiki wa mke/mpenzi wangu. Siruhusu hicho kitu.

Msimamo wako ni sahihi... Na ndio msimamo unaotakiwa kwa kiasi kikubwa. Ubaya ni kuwa tumetofautiana na siyo wote wana msimamo kama wako. Na wahanga wa maelezo yangu hayo mara nyingi ni siye akina mama kuliko wanaume. So unaweza usiruhusu hilo, ila elewa kwa kiasi kikubwa kuna wanao yakuta haya... Iwe kw kupenda ama bahati mbaya.
 
Nicas Mtei, asante sana kwa mada nzuri
mimi ni kati ya watu ambao hatujabahatika kuwa na marafiki wengi. Ila ninachoamini ni kutowahusisha marafiki katika mambo ya mahusiano, hasa mambo yanayohusiana na ugomvi. ni vizuri kuongea kama partners na kuyamaliza nyie wenyewe, marafiki wawaone mkiwa mna-smile tu.
 
Last edited by a moderator:
binafsi si kila rafiki nitamweleza yangu....yale ya ndani nitaenda kuyazungumzia bafuni au chooni mpaka yanitoke.....

Always ni vyema kuchora mstari /mpaka kati ya rafiki na mpenzi mke mume wako......

Na yale ya sirini yabaki kati yenu wenza.....

Kuna limit ya marafiki katika uhusiano.....
 
Back
Top Bottom