Athari ya demokrasia kupitia maandamano yasiyo na ukomo

Unaujua ukweli, ila unataka kujifanya hujui.....
Sio vizuri kuwarudisha waTz kwenye siasa za mazoea....
Usitamani nyakati hizi (ambapo watu wanaandamana kwa amani) ziishe au zizimwe bila mabadiliko yanayoliliwa.
 
Uendeshaji wa vyama kupitia maandamano unaficha mambo mengi ambayo ni vyema watanzania tujiulize. Je miaka 2010 hadi 2015 tutegemee maandamano wa mji hadi mji? Ndio demokrasia ya vyama inavyojengwa? Je tunatoa nafasi kwa chama kilichoshinda kutekeleza mipango yake?


Je upinzani unapinga nafasi ya uwekezaji wa nje kama njia muhimu ya kujenga uchumi na kujenga nafasi mpya za ajira? Je, ni sera ya upinzani kuwa wawekazaji katika sera ya madini waondoke na upinzani unafahamu athari za utaifishaji?

Maandamano hayatoi nafasi ya kuwauliza viongozi wa “Vyama-maandamano” kama wangependa waliowekeza SONGAS waondoke sasa hivi. Je tunao uwezo wa kununua mitambo ya kuchimba madili na kuchota gesi asilia kutoka ardhini bila kutegemea uwekezaji kutoka nje?

Je “Vyama-maandamano” vitatumia mbinu gani kuwashawishi wawekezaji wawekeze fedha nyingi za kigeni lakini sisi ndio tuvune matunda yetu? Watanzania ni bora tukumbuke kuwa tuna rasilmali nyingi sana ardhini lakini hii rasilmali sio yetu peke yetu kwa kuwa hatuna uwezo wa kifedha, kuitaalamu na kiufundi wa kuivuna.

Utamu wa maandamano ni nafasi ya kulaumu na kuahidi watanzania kuwa hali ya maisha ya watanzania yatabadilika endapo walio upinzani watachukua dhamana ya kuongoza nchi.

Maandamano zenye ahadi tamu tamu hayatoi nafasi kwa wananchi kujiuliza msimamo wa vyama-maandamano kuhusu sera zao na watatoa wapi rasilmali ya kubadili maisha ya watanzania kwa muda mfupi kama wanavyoahidi.

Bei ya petrol, dizeli na vyakula huko Kenya ni kubwa zaidi ya Tanzania. Mtikisiko wa uchumi wa dunia ulipo sasa, machafuko katika nchi zinazozalisha mafuta na kadhalika haitokani na chama kilichopo madarakani Tanzania.

Mimi nafahamu kuwa wengi katika Jamii forum, hawapendi kuwauliza “Vyama-maandamano” maswali magumu. Wengi tunapenda kusikia maneno matamu ya kulaumu, na kutoa ahadi kuwa ufumbuzi wa matatizo ya Tanzania ni kupitia “maandamano.” Kwa bahati mbaya pia, wengi hatupendi kujitafutia taarifa sisi wenyewe. Tunasubiri kuwa Fulani tunayempenda akishasema sisi tunakubali na pia tunawazomea kwa nguvu sana wale ambao wataonyesha dalili za kupingana au kuhoji. Hiyo ndio demokrasia ijayo Tanzania. Mungu Ibariki Tanzania.


na bado.. kama unafaidika na upuuzi unaofanywa na hao unaowatetea jipange sasa wakati bado una muda, siku yaja
 
Huyu mtoa mada nadhani yuko kazini na alitaka kujua tutasema nini . Kesha jibiwa nadhani atatia akili . Huyu kaleta mawazo ya akina Mukama , Nape, Tambwe , na wajinga kibao wa CCM.Hivi kweli una amini kwamba Tanzania itaendelea kwa wawekezaji hawa wanao pelekea watu kuawa na serikali kuwaita wahalifu the same time wanapeleka pesa za msaada kuwazika ?Nenda huko Ulaya uone uwekezaji ulivyo na jinsi wanavyo gawana hakuna ujinga kama huo wa Songas wako . Uwekezaji huo uko muda sasa zile ajira za milioni zimesha fika au unasema tu kwa kuwa una access ya kuandika JF ? Hivi mzozo huu ukipelekwa Bungeni Makinda na wengi wape watakubali hoja zijadiliwe hadharani na kupatiwa majibu ?
 
Athari zake ni chanya kwa kuamsha ufahamu wa haki za raia mtanzania ktk masuala ya kodi wanazotoa kutumika na serikali kuu au serikali za mitaa kuboresha maisha yao kwa huduma bora kama elimu, afya, usafiri, nishati n.k

Pia soma jinsi watoto hawa wa mkoa wa Mara huko Bunda jinsi somo la elimu ya uraia litolewalo na CHADEMA ilivyowaamsha uwezo wao wa kufikiri na kuchambua mambo yaliyo ktk mazingira yao:

Wanafunzi Bunda wamsalimia Mama Kikwete kwa ishara ya vidole viwili

Na Cosmas Mlekani
20th May 2011

Salmaa.jpg

Mke wa Rais, Salma Kikwete akipiga makofi baada ya kuzungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Ushashi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara juzi baada ya sherehe ya kuzindua madarasa matatu yaliyojengwa na Kampuni ya saruji ya Twiga kwa kushirikiana na Kampuni ya Mwanza Huduma.

Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, juzi alipigwa na butwaa baada ya baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Ushashi iliyopo wilayani Bunda mkoani Mara, kumsalimia kwa kumuonyeshea ishara ya vidole viwili.

Mama Kikwete alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi vyumba vitatu vya madarasa na ofisi mbili za walimu na jengo moja vilivyojengwa na kukarabatiwa kwa msaada wa Kampuni ya Saruji ya Twiga kwa kushirikiana na Mwanza Huduma Limited.

Baada ya kukata utepe kama ishara ya kuzindua majengo hayo, Mama Kikwete, alikagua madarasa hayo mapya pamoja na ofisi za walimu kabla ya kukutana na wanafunzi 30 waliotengwa rasmi kukabidhiwa mabegi ya shule na mgeni rasmi huyo.

Na alipofika mbele ya wanafunzi hao, Mama Kikwete, alinyoosha mkono juu kuwasalimia wanafunzi hao, lakini wengi wao walimjibu kwa kumuonyesha ishara ya vidole viwili, kitu ambacho kilimshangaza na kusema: "Huu sio utaratibu." Na kisha akawauliza: Je; walimu wenu wanawafundisha hivyo?.

Hata hivyo, wanafunzi karibu wote walikaa kimya, lakini mmoja wao bila woga alijibu "Ndiyo" na kumfanya Mama Kikwete kumgeukia Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Francis Isack na viongozi wengine na kuwaambia: "Inaelekea watoto hao ndivyo mnavyowafudisha."

Baada ya kukemea kitendo hicho, Mama Kikwete aliendelea na zoezi lake la kuwagawia wanafunzi hao mabegi ya shule kabla ya kwenda katika jukwaa la wageni lililoandaliwa maalum kwa ajili yake na msafara wake. Salamu ya kuonyesha vidole viwili mara nyingi hutumiwa na Chama upinzani cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Kampuni ya Twiga Simenti ilijenga madarasa matatu na ofisi za walimu na kulifanyia ukarabati jengo moja, ambapo walitumia jumla ya Sh. milioni 90.

Sherehe hizo za kukabidhi vyumba hivyo vya madarasa, zilionekana kama ni za Chama cha Mapinduzi (CCM), baada ya nyimbo zilizokuwa zikipigwa ni zile za chama hicho, huku akina mama wengi wakiwa wamevalia fulana na khanga za CCM pia.



CHANZO: NIPASHE http://www.ippmedia.com/
 
Back
Top Bottom