Uendeshaji wa vyama kupitia maandamano unaficha mambo mengi ambayo ni vyema watanzania tujiulize. Je miaka 2010 hadi 2015 tutegemee maandamano wa mji hadi mji? Ndio demokrasia ya vyama inavyojengwa? Je tunatoa nafasi kwa chama kilichoshinda kutekeleza mipango yake?
Je upinzani unapinga nafasi ya uwekezaji wa nje kama njia muhimu ya kujenga uchumi na kujenga nafasi mpya za ajira? Je, ni sera ya upinzani kuwa wawekazaji katika sera ya madini waondoke na upinzani unafahamu athari za utaifishaji?
Maandamano hayatoi nafasi ya kuwauliza viongozi wa Vyama-maandamano kama wangependa waliowekeza SONGAS waondoke sasa hivi. Je tunao uwezo wa kununua mitambo ya kuchimba madili na kuchota gesi asilia kutoka ardhini bila kutegemea uwekezaji kutoka nje?
Je Vyama-maandamano vitatumia mbinu gani kuwashawishi wawekezaji wawekeze fedha nyingi za kigeni lakini sisi ndio tuvune matunda yetu? Watanzania ni bora tukumbuke kuwa tuna rasilmali nyingi sana ardhini lakini hii rasilmali sio yetu peke yetu kwa kuwa hatuna uwezo wa kifedha, kuitaalamu na kiufundi wa kuivuna.
Utamu wa maandamano ni nafasi ya kulaumu na kuahidi watanzania kuwa hali ya maisha ya watanzania yatabadilika endapo walio upinzani watachukua dhamana ya kuongoza nchi.
Maandamano zenye ahadi tamu tamu hayatoi nafasi kwa wananchi kujiuliza msimamo wa vyama-maandamano kuhusu sera zao na watatoa wapi rasilmali ya kubadili maisha ya watanzania kwa muda mfupi kama wanavyoahidi.
Bei ya petrol, dizeli na vyakula huko Kenya ni kubwa zaidi ya Tanzania. Mtikisiko wa uchumi wa dunia ulipo sasa, machafuko katika nchi zinazozalisha mafuta na kadhalika haitokani na chama kilichopo madarakani Tanzania.
Mimi nafahamu kuwa wengi katika Jamii forum, hawapendi kuwauliza Vyama-maandamano maswali magumu. Wengi tunapenda kusikia maneno matamu ya kulaumu, na kutoa ahadi kuwa ufumbuzi wa matatizo ya Tanzania ni kupitia maandamano. Kwa bahati mbaya pia, wengi hatupendi kujitafutia taarifa sisi wenyewe. Tunasubiri kuwa Fulani tunayempenda akishasema sisi tunakubali na pia tunawazomea kwa nguvu sana wale ambao wataonyesha dalili za kupingana au kuhoji. Hiyo ndio demokrasia ijayo Tanzania. Mungu Ibariki Tanzania.