ATCL bado sana kwenye Safari za anga

ATCL bado sana kwenye Safari za anga

Mkuu Marashi ,ungepiga picha na kuipeleka kwa Mh. JPM,hakika ungekuwa mzalendo halisi,maana nina imani hatua kali na stahiki zingechukuliwa.
Mimi naamini kabisa kabisa kuwa kama tukiwa na ushahidi wa madudu yanayotokea serikalini na mashirikani,hatua kali zitachukuliwa na wahusika.
Nilihofia kuweka rehani maisha yangu na kibarua. Nilikaa jiran na watu wazito
 
Acha uongo mie nasafiri na pia kuahirisha safari sijawahi kuambiwa miezi sita


Halafu wana sera yao fulani ya "ticket refund". Eti huwezi kupata refund mpaka miezi sita ipite ndiyo uanze kufuatilia hiyo refund yako.
 
Ila si bora ummefika kwenu pamoja na kasoro izo ulizo taja. ? Lkn pia wakati ukidai bei ni kubwa kuliko mashirika mengine, pia kumbuka iyo iyo atcl ilikuwa inakodishwa nq mataifa mengine pia kusafirisha raia wao !
 
Rais JPM anajitahidi kufufua shirika letu la ndege lakini namna linavyojiendesha ni tatizo. Tusipopiga kelele litakufa tena na juhudi za kulifufua zitakuwa zimehujumiwa.

Muhula wa masomo China umemalizika. Wanafunzi waliohitimu wanarudi makwao. Nchi nyingi zinachukua wanafunzi wake kwa ndege zao or any other chattered flights.

Serikali yetu imeamua kuchukua watu wake kwa ndege yetu ya Dreamliner ambayo imeondoka leo saa kumi jioni (one way, kutoka Guanzhou mpaka JNIA, Dar)
_
Lakini zoezi hili limekuwa na kasoro nyingi. Moja ni gharama kuwa juu karibu mara mbili kulinganisha na mashirika mengine. Lakini wamelazimika kulipa kwa sababu serikali imezuia kurudi kwa ndege nyingine isipokua ATCL kwa kile kinachoitwa Uzalendo.

Pili, mwezi mmoja uliopita wahitimu walitakiwa kutuma nakala za passport zao ili waandaliwe tiketi. Wakatuma na wakawa wanasubiri itinerary ili kupewa tiketi.

Juzi wakapokea ujumbe kutoka Ubalozi wetu China, kwamba ATCL imefanya makosa mengi kwenye tiketi. Wamekosea spelling, Lulu Kicheere ameitwa Lulu Kicheche. Wamekosea jinsia, John kaandikwa Female na Prisca Male. Wamekosea tarehe za kuzaliwa. Kuna waliozaliwa 1890 kabla ya vita vya Majimaji. Wamekosea mpangilio wa majina na makosa mengine mengi.

ATCL walipotakiwa kufanya marekebisho walidai muda uliobaki usingetosha kurekebisha makosa yote. Kama walipewa mwezi mzima wakafanya makosa mengi hivi, wangewezaje kurekebisha kwa siku mbili.

Kwahiyo ubalozi wetu China ikabidi uandae orodha ya majina itakayotumiwa na wasafiri. Jana Ubalozi umesema ticket za ATCL hazitatumika kama kigezo pekee cha kusafiri bali abiria watahakikiwa kupitia orodha ya majina iliyoandaliwa na ubalozi huo.

Jiulize, hivi tupo serious na biashara ya usafiri wa anga? Kama mwezi mzima ATCL wameshindwa kuandaa tiketi, tena kwa safari moja, je safari zikiwa kila siku itakuaje? Tumebaki kusifu idadi ya ndege, kumbe hatuna uwezo hata wa kuandaa tiketi? Leo watu wanapanda ndege kama daladala? Hakuna hata boarding pass, unakaa siti yoyote iliyo wazi kama mabasi ya Bukene Nzega. Aibu gani hii?

Kumbuka Nyerere aliacha shirika likiwa na ndege nyingi sana, lakini likafilisika kwa sababu ya management mbovu. Sasa tunarudi kulekule?

Malisa GJ
Daaah, kwani hujui kukosea ndo sehemu ya kujifunza na kwa makosa hayo uliyoelezea hapo yanaua vp shirika? kwani kama ungeandika tu kuwajulisha hao watu wa ATCL juu ya mapungufu yao kwa namna nzuri bila kusema shirika litakufa kuna ubaya gani kuliko kuandika kama ndege imeshindwa kufanya safari kumbe ni majina tu yamekosewa, punguza ujuaji tuwaunge mkono na kuwakosoa ATCL kizalendo watakaa sawa tu, VIVA ATCL, VIVA TANZANIA Twiga ataendelea kuwa angani tu.
 
Ni ukweli usiopingika kuwa wafanyakazi weengi wa serikali hawapo business oriented. Ni wazembe, wavivu kufanya kazi na kufikiri.

Juzi imenichukua wiki 2 kupata birth certificate wakati ni kitu cha dakika 10-20, nikajiuliza hivi hawa wana KPI?

KPI zao zina vigezo gani?

Maana nnapofanya kazi nina strict daily KPI
acha ujinga wewe hauwezi ukapewa cheti cha kuzaliwa kwa dk 10 tu kwa nyaraka muhimu kama hiyo sehemu yoyote duniani.
 
Kuna miaka ya nyuma 2008 baadhi tuliondoka kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine kwa sababu kulikuwa hamna ndege hata moja,
Tulitaka kurudi tukiwa na rating za ndege mbalimbali,wakatuletea fitna wakiogopa kuporwa nyazifa zao huku visingizio kibao,kwa Sasa Kuna mpasuko wa ATCL mpya na na wale wa Zamani Hilo shirika akiondoka Magufuri ataondoka nalo hawajui ushindani.
ndo sababu mnakuwa na chuki na atcl?
 
Sisi wengine huwa hatukurupuki kuandika humu. Tunaangalia pia trend ya biashara hii dunia nzima. Na hii biashara tayari ilikuwa katika hali mbaya hata kabla ya COVID, na hii covid ndiyo kabisa mashirika mengi yameanza kufa na mengi yatakufa au kupunguza wafanyakazi wake kwa asilimia kubwa.

Haingii akilini kuchota hazina trillion 2 kununua ndege huku ukiwa umeshaonywa kwamba ndege si kipaumbele cha Watanzania



Daaah, kwani hujui kukosea ndo sehemu ya kujifunza na kwa makosa hayo uliyoelezea hapo yanaua vp shirika? kwani kama ungeandika tu kuwajulisha hao watu wa ATCL juu ya mapungufu yao kwa namna nzuri bila kusema shirika litakufa kuna ubaya gani kuliko kuandika kama ndege imeshindwa kufanya safari kumbe ni majina tu yamekosewa, punguza ujuaji tuwaunge mkono na kuwakosoa ATCL kizalendo watakaa sawa tu, VIVA ATCL, VIVA TANZANIA Twiga ataendelea kuwa angani tu.
 
Back
Top Bottom