ATCL bado sana kwenye Safari za anga

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,039
Rais JPM anajitahidi kufufua shirika letu la ndege lakini namna linavyojiendesha ni tatizo. Tusipopiga kelele litakufa tena na juhudi za kulifufua zitakuwa zimehujumiwa.

Muhula wa masomo China umemalizika. Wanafunzi waliohitimu wanarudi makwao. Nchi nyingi zinachukua wanafunzi wake kwa ndege zao or any other chattered flights.

Serikali yetu imeamua kuchukua watu wake kwa ndege yetu ya Dreamliner ambayo imeondoka leo saa kumi jioni (one way, kutoka Guanzhou mpaka JNIA, Dar)
_
Lakini zoezi hili limekuwa na kasoro nyingi. Moja ni gharama kuwa juu karibu mara mbili kulinganisha na mashirika mengine. Lakini wamelazimika kulipa kwa sababu serikali imezuia kurudi kwa ndege nyingine isipokua ATCL kwa kile kinachoitwa Uzalendo.

Pili, mwezi mmoja uliopita wahitimu walitakiwa kutuma nakala za passport zao ili waandaliwe tiketi. Wakatuma na wakawa wanasubiri itinerary ili kupewa tiketi.

Juzi wakapokea ujumbe kutoka Ubalozi wetu China, kwamba ATCL imefanya makosa mengi kwenye tiketi. Wamekosea spelling, Lulu Kicheere ameitwa Lulu Kicheche. Wamekosea jinsia, John kaandikwa Female na Prisca Male. Wamekosea tarehe za kuzaliwa. Kuna waliozaliwa 1890 kabla ya vita vya Majimaji. Wamekosea mpangilio wa majina na makosa mengine mengi.

ATCL walipotakiwa kufanya marekebisho walidai muda uliobaki usingetosha kurekebisha makosa yote. Kama walipewa mwezi mzima wakafanya makosa mengi hivi, wangewezaje kurekebisha kwa siku mbili.

Kwahiyo ubalozi wetu China ikabidi uandae orodha ya majina itakayotumiwa na wasafiri. Jana Ubalozi umesema ticket za ATCL hazitatumika kama kigezo pekee cha kusafiri bali abiria watahakikiwa kupitia orodha ya majina iliyoandaliwa na ubalozi huo.

Jiulize, hivi tupo serious na biashara ya usafiri wa anga? Kama mwezi mzima ATCL wameshindwa kuandaa tiketi, tena kwa safari moja, je safari zikiwa kila siku itakuaje? Tumebaki kusifu idadi ya ndege, kumbe hatuna uwezo hata wa kuandaa tiketi? Leo watu wanapanda ndege kama daladala? Hakuna hata boarding pass, unakaa siti yoyote iliyo wazi kama mabasi ya Bukene Nzega. Aibu gani hii?

Kumbuka Nyerere aliacha shirika likiwa na ndege nyingi sana, lakini likafilisika kwa sababu ya management mbovu. Sasa tunarudi kulekule?

Malisa GJ
 
Inafaa muda mwingine kunyamaza. Sio kila kitu kinaweza kuwa ni makosa au ni kosa la kuzungumziwa sababu wote tunamapungufu kama alivyo mtu mwingine yeyote including the president Magu.

Tatizo mnamsimanga lakini katika mengi aliyofanya Magu kwa muda mchache nyie wenywe hamuwezi kufanya.

Magufuli, anayo speed, anataka speed na anaenda kwa speed.

Mnasubiri siku ndio mmkumbuke au afe ndio mmkumbuke. Hata Mkapa mlisema sana. Amekufa ndio mnasema alikuwa genius sijui nini.

Atcl haitakufa labda mfe nyinyi. Mungu ataendelea kubariki kazi za muheshimiwa RAisi Magufuli na utawala wake katika kuinua Tanzania na watanzania walio maskini.

Nyinyi ndio moja ya wale mijitu inasubiri Magufuli aondoke muendlee kufanya yenu. Kuiba, ufisadi ndio mnavyoviwaza.
 
Tumeweza lipi? Hata huyo Nyerere wako unaemsifia nchi aliifikisha wapi su ulikuwa hujazaliwa kwa mdomo tu alikuwa malengo lakini mwisho wake watendaji ambao ni mimi na WEWE tulishindwa kama washindwavyo waafrika wengine
 
Inafaa muda mwingine kunyamaza. Sio kila kitu kinaweza kuwa ni makosa au ni kosa la kuzungumziwa sababu wote tunamapungufu kama alivyo mtu mwingine yeyote including the president Magu.
Tatizo mnamsimanga lakini katika mengi aliyofanya Magu kwa muda mchache nyie wenywe hamuwezi kufanya.
Magufuli, anayo speed, anataka speed na anaenda kwa speed.
Mnasubiri siku ndio mmkumbuke au afe ndio mmkumbuke. Hata Mkapa mlisema sana. Amekufa ndio mnasema alikuwa genius sijui nini.

Atcl haitakufa labda mfe nyinyi. Mungu ataendelea kubariki kazi za muheshimiwa RAisi Magufuli na utawala wake katika kuinua Tanzania na watanzania walio maskini.

Nyinyi ndio moja ya wale mijitu inasubiri Magufuli aondoke muendlee kufanya yenu. Kuiba, ufisadi ndio mnavyoviwaza.
Ni ukweli usiopingika kuwa wafanyakazi weengi wa serikali hawapo business oriented. Ni wazembe, wavivu kufanya kazi na kufikiri.

Juzi imenichukua wiki 2 kupata birth certificate wakati ni kitu cha dakika 10-20, nikajiuliza hivi hawa wana KPI?

KPI zao zina vigezo gani?

Maana nnapofanya kazi nina strict daily KPI
 
Bei Imepanda Mara Mbili Zaidi, Bila Shaka Iwapo Huu Ni Ukweli
Acha Tumzike Mzee Mkapa Halafu Utaona Cheche.
Yaani Hiyo Haiwezekani Ufanye Jambo Tofauti Na Wenzako
Matumaini Ya Kufanya Vema Sokoni Yanahujumiwa!!!!

Stay Tuned!!
Nawaangalia Halafu Nasema Hii Bhaghoshaa!!!
 
Mkuu ndiyo matatizo ya kutaka kufanya mambo KIENYEJI kwa kulazimisha tu bila kusikiliza maoni ya wengi.

Tangu mwanzo wengi tulisema biashara ya ndege ni ngumu sana na mashirika mengi duniani yanapata hasara kubwa sana mengine HUFA na mengine huamua kuingia kwenye partnership na mashirika mengine.

Pia tukasema kwamba kutokana na vipato vidogo vya Watanzania wengi basi wenye uwezo wa kusafiri na ndege hawezi 5% ya Watanzania wote.

Ukiweka na haya madudu mengine kama alivyoandika Malisa basi unaona tulichokisema kinakuwa kweli. ATCL inaendeshwa kwa hasara kubwa sana ya mabilioni na hiyo ruzuku wanayopewa na Serikali haina return yoyote kwa walipa kodi.

Ni mpaka lini ATCL itaendelea kutumia billions za walipa kodi huku ikiendelea kuingiza hasara kila quarter tena ya mabilioni?
Na hivi ni mtu asiyependa kushindwa na anajua aibu yote ya atcl ni yake yeye, ataendelea kuwachotea hela tu..

Dawa yake huyu ni October 28 kumpiga termination tu..

Rais ameingia jana Mkuu.
 
Inafaa muda mwingine kunyamaza. Sio kila kitu kinaweza kuwa ni makosa au ni kosa la kuzungumziwa sababu wote tunamapungufu kama alivyo mtu mwingine yeyote including the president Magu.
Tatizo mnamsimanga lakini katika mengi aliyofanya Magu kwa muda mchache nyie wenywe hamuwezi kufanya.
Magufuli, anayo speed, anataka speed na anaenda kwa speed.
Mnasubiri siku ndio mmkumbuke au afe ndio mmkumbuke. Hata Mkapa mlisema sana. Amekufa ndio mnasema alikuwa genius sijui nini.

Atcl haitakufa labda mfe nyinyi. Mungu ataendelea kubariki kazi za muheshimiwa RAisi Magufuli na utawala wake katika kuinua Tanzania na watanzania walio maskini.

Nyinyi ndio moja ya wale mijitu inasubiri Magufuli aondoke muendlee kufanya yenu. Kuiba, ufisadi ndio mnavyoviwaza.
Ishiiiiiiii! Hivi una akili kweli? Hizo irregularities zote alizoandika Malisa umeona hazifai kuandikwa kwenye hii platform? Yaani Negligence of that degree🤔🤔🤔 unakosea majina bado unapga mikwara mbuzi kwa passengers,wakati nauli yenyewe sio ya kiushindani,tunawasema ili wajirekebishe wewe unazuia!!!!!!! Mara Mkapa mara sijui Nini,ulisikia wapi marehemu anasemwa vibaya? KWANI LAZMA U COMMENT?
 
Inafaa muda mwingine kunyamaza. Sio kila kitu kinaweza kuwa ni makosa au ni kosa la kuzungumziwa sababu wote tunamapungufu kama alivyo mtu mwingine yeyote including the president Magu.
Tatizo mnamsimanga lakini katika mengi aliyofanya Magu kwa muda mchache nyie wenywe hamuwezi kufanya.
Magufuli, anayo speed, anataka speed na anaenda kwa speed.
Mnasubiri siku ndio mmkumbuke au afe ndio mmkumbuke. Hata Mkapa mlisema sana. Amekufa ndio mnasema alikuwa genius sijui nini.

Atcl haitakufa labda mfe nyinyi. Mungu ataendelea kubariki kazi za muheshimiwa RAisi Magufuli na utawala wake katika kuinua Tanzania na watanzania walio maskini.

Nyinyi ndio moja ya wale mijitu inasubiri Magufuli aondoke muendlee kufanya yenu. Kuiba, ufisadi ndio mnavyoviwaza.

Nasimama na mleta mada. Pamoja na juhudi kubwa za Mh. Rais za kufufua shirika letu la ndege, kama uongozi na wafanyakazi wa ATCL hawatafanya kazi kwa weledi shirika litakufa. Uzembe ni lazima ukemewe. Tuache kuendekeza uzembe kwa kigezo cha 'mapungufu ya kibinadamu'.
 
Mkuu ndiyo matatizo ya kutaka kufanya mambo KIENYEJI kwa kulazimisha tu bila kusikiliza maoni ya wengi.

Tangu mwanzo wengi tulisema biashara ya ndege ni ngumu sana na mashirika mengi duniani yanapata hasara kubwa sana mengine HUFA na mengine huamua kuingia kwenye partnership na mashirika mengine.

Pia tukasema kwamba kutokana na vipato vidogo vya Watanzania wengi basi wenye uwezo wa kusafiri na ndege hawezi 5% ya Watanzania wote.

Ukiweka na haya madudu mengine kama alivyoandika Malisa basi unaona tulichokisema kinakuwa kweli. ATCL inaendeshwa kwa hasara kubwa sana ya mabilioni na hiyo ruzuku wanayopewa na Serikali haina return yoyote kwa walipa kodi.

Ni mpaka lini ATCL itaendelea kutumia billions za walipa kodi huku ikiendelea kuingiza hasara kila quarter tena ya mabilioni?
Mawazo yako yanadilute uzi. Nampongeza Malisa kwa uzi wa kujenga. Uzi wake lazima ufike kwa Bose wao
 
Matindi asipowafukuza kazi wote waliohusika na hayo makosa basi Jiwe amtumbue yeye. Haya si makosa ya kufumbia macho. Ukicheka na ngedere utavuna mabua.

Zoezi na kukagua vyeti vya elimu vya waajiriwa serikalini lifanywe tena. Bado majipu mengi, na kama alivyosema Jiwe, dawa ya jipu ni kulitumbua.

Tumedharauliwa vya kutosha. It's time to act. Tatizo hapa sio Rais, ni watu wazembe ambao, hatukujua kwamba wameoza kiasi hicho. Maadam sasa uozo umeonekana, ni kusafisha. Enough.
 
Atcl , watumishi wake wanafanya kazi kimazoea sana! Hapa naona ni tabia ya watumishi wengi serikalini uzembe,mapuuza, ujinga, kujiona n.k huku wakiwa hawajali mda.

NB. WAFANYAKAZI WA ATCL JITAHIDINI KUFANYA KAZI KWA WAREDI NA SIO KIMAZOEA. TUTAFIKA MBALI
 
Mkuu ndiyo matatizo ya kutaka kufanya mambo KIENYEJI kwa kulazimisha tu bila kusikiliza maoni ya wengi.

Tangu mwanzo wengi tulisema biashara ya ndege ni ngumu sana na mashirika mengi duniani yanapata hasara kubwa sana mengine HUFA na mengine huamua kuingia kwenye partnership na mashirika mengine.

Pia tukasema kwamba kutokana na vipato vidogo vya Watanzania wengi basi wenye uwezo wa kusafiri na ndege hawezi 5% ya Watanzania wote.

Ukiweka na haya madudu mengine kama alivyoandika Malisa basi unaona tulichokisema kinakuwa kweli. ATCL inaendeshwa kwa hasara kubwa sana ya mabilioni na hiyo ruzuku wanayopewa na Serikali haina return yoyote kwa walipa kodi.

Ni mpaka lini ATCL itaendelea kutumia billions za walipa kodi huku ikiendelea kuingiza hasara kila quarter tena ya mabilioni?
Jiwe ana roho ya uharibifu!
 
Ticket price ya $ 1,219 ni ghali kwa kipindi hiki tena flights hakuna za moja kwa moja Guanzhou to Dar? Ebu acheni maneno ya upuuzi.. Hata kama ni one way, ujue kwenda trip ya China kwani ndege ilitumia maji? Ujue ilitumia gharama ya kwenda na lazima ifidiwe kwenye hiyo nauli.. Yaani rescue flight from China to Tanzania, kwa $ 1,219 mtu anaona ghali? Kweli watu hamjui kabisa mambo ya aviation with respect to certain conditions & time
 
Poleni sana kwa waathirika wa hii incident, Watanzania wenzangu, kwenye mambo ya kitaifa, tutangulize uzalendo kwa ku think positive and concentrate on the positives and not the negatives. ATCL is doing the best, inastahili kuwa encouraged na kutiwa moyo na sio kulaumiwa wakati wote.

Angalia mambo makubwa mazuri haya ya ATCL

P
 
Back
Top Bottom