Atc kuiokoa kifanyike nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Atc kuiokoa kifanyike nini?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Netanyahu, Feb 14, 2009.

 1. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #1
  Feb 14, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa mawazo yangu nashauri vitu vifuatavyo vingine wengine mtajazia
  ili kuliokoa shirika letu la ndege.

  1.ATC wanabwata kuwa wanahitaji ndege nyingi zaidi (quantity) Swala si uwingi wa ndege kama wanavyodai bali ni uhakika wa HUDUMA hizo ndege (quality) bila kujali ni moja au nyingi.Mfano precision AIR walianza na ndege moja ikawa inaenda kwa wiki mara mbili bukoba kama sikosei lakini walikuwa waaminifu sana na hizo safari zao mbili kwa wiki.Serikali isiwape mabilioni wanayotaka kuomba kwanza.Ni heri waruke hata mara moja kwa mwezi lakini wawe reliable na quality za huduma zao ziwe nzuri.Watu wataanza kuwaheshimu na kuwaamini.Wapunguze wafanyakazi,routes,na gharama za uendeshaji na waweke menejimenti ndogo ya watu wachache wenye akili sana na wajuao kutumia hizo akili kuendesha shirika kwa faida.Inaelekea ATC kumejaa wajinga wengi kuanzia bodi,manajimenti hadi kwa wafanyakazi wa kawaida ndiyo maana haliendi vizuri.Kama haiwezekani serikali iajiri menejimenti yenye uwezo kutoka nje iendeshe kwa muda au iombe Ethiopian Airline watuazime baadhi ya watu wao waje watusaidie kwa posho kidogo Kwenye menejimenti.Kikwete aongee na Raisi wa Ethiopia ni mtu mzuri nadhani aweza msaidia.

  2.Wawe makini kuchagua routes zenye faida ndani na nje ya nchi.Sasa hivi inaonyesha wanaruka tu kama vichaa.Kuna njia ATC haiwezi kushindana kabisa,Njia kama ya kwenda Johansburg wameshindwa kabisa wala huhitaji mtaalamu wa safari za anga kuwaeleza kuwa imewashinda.

  3.Wawe na uhusiano mzuri na serikali na ma-ajents wa kukata tikiti.Serikali mara nyingi huwa na watumishi wanaosafiri mara kwa mara kikazi n.k ndege za ATC zikiwa za kuaminika na wakawa na uhusiano mzuri na serikali serikali ingaliweza kuwa inawapa tenda nyingi na ingeamuru wafanyakazi wake kuwa lazima wasafiri na ATC unless labda hiyo route ATC iwe haiendi.Lakini naona hata serikali inaogopa maana ATC wengine hupenda kuiita ANY TIME CANCELLATION AIRLINE .Uhusiano wa kuaminika na maajenti wakata tikiti ni muhimu mno.Kuna maajenti ukienda wakitaka kukukatia tikiti wanaanza kwanza kukutajia ndege zingine na siyo ATC.ATC nadhani kichwani mwao huwa haipo kabisa wanaanza kwanza mashirika mengine lakini siyo ATC kwa nini nadhani ATC wanalo jibu la kwa nini maajenti wa kukata tikiti hawawapi kipaumbele.
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,350
  Likes Received: 5,653
  Trophy Points: 280
  2.Wawe makini kuchagua routes zenye faida ndani na nje ya nchi.Sasa hivi inaonyesha wanaruka tu kama vichaa.Kuna njia ATC haiwezi kushindana kabisa,Njia kama ya kwenda Johansburg wameshindwa kabisa wala huhitaji mtaalamu wa safari za anga kuwaeleza kuwa imewashinda

  mkuu akuna alieandikiwa kwenda jnb m napingana na wwewe kidogo hapo,,siku zote rte yoyote kinachotakiwa kwanza kaka uwe stable kwenye marketing...na comm
  nini maanna yake,viongozi wa atcl wamekuwa wakiamua wanachojua wao liwalo na liwe bila kuangalia vitu vya maana..mfano halisi rais alihimiza wapewe hela waanze kuruka mara moja,,hata kama ni mfalme ameagiza ,,wamekuwa chini kwa miezi miwili...ok,na baad aya hapo hakuna alieamua kuitangaza mpaka watu tunaruka na ndege zao tunawaambia fanyeni marketing.,,kuna mbinu nyingi hata wangeanza na special fair kuwa attract abiri hao punguani wao wa liokalia viti uko marketing hawana ata akili...hiyo RTE mkuu inauzika wacha....m nakumbuka nilishawahi kusafiri TCLA IKO FULL MARA T KWENDA S.africa,so tatizo ni kufwata principle,,,kinachofanyika sasa hizi hata schedule maalum natumain hawana...wewe utaweza kuttoka ata mkipewa billion 500 za mwana kjkj
  luv u tz
   
 3. N

  Namnauka Member

  #3
  Feb 16, 2009
  Joined: Jan 12, 2008
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo katika ATCL ni ubunifu wa biashara. Tunajua kampuni imekuwa na matatizo ya muda mrefu sana hata baada ya kuungana na SAA hakukuwa na matunda yeyote.
  Kinachotakiwa kufanyika sasa ni uongozi kujipanga upya na kuangalia sifa za watendaji wake wote ili kuona ni maeneo gani yanahitaji wataalamu lakini yanakaliwa na watu wenye sifa zisizokidhi matakwa ya nafasi husika.

  Aggressive Marketing inahitajika sana kuiweka tena ATCL mioyoni na midomoni mwa wananchi.
  Customer care ya hali ya juu inatakiwa kuanzia reception mpaka kwa sales personel. Iondoke ile tabia ya unapiga simu kuulizia huduma unajibiwa "Haloo Shirika la ndege hapa..!"...Duu kwa wataalamu wanajua receptionist anatakiwa kujibu nini ili mteja ajue kuwa anaongea na ATCL na kwamba shida zake zitafanyiwa kazi. (First Impression).

  Lakini muhimu katika operesheni ni kuhakikisha kuwa ndege zote zinakuwa katika hali nzuri muda wote. Kusiwe na excuse za "kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu ndege haitaruka leo..." na hiyo excuse unaitolea uwanja wa ndege muda wa kuruka ndege.

  Yapo mengi sana lakini bila kusahau staff motivation...iwe katika salary, masomo, warsha, kusikilizwa mawazo yao, kutatuliwa shida ndogondogo. Yaani mfanyakazi afikie mahali aone shirika kama sehemu ya mwili wake.
   
Loading...