Sajenti
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 3,651
- 416
Habari za kuaminika ni kuwa shirika la ndege ATC limeshindwa kufanya safari zake kutokea Dar kwenda Kigoma tangu tarehe 10 May 2010.
Kwa mujibu wa mtu mmoja wa karibu aliyetakiwa kusafiri na ndege hiyo siku ya Jumatatu tarehe 10 kwenda kigoma, walifahamishwa kuwa ndege hiyo imefutwa bila ya kupewa maelezo yoyote ya maana. Baada ya sintofahamu ya muda mrefu ilikuja kubainika kuwa ndege iliyotakiwa kuruka siku hiyo kwenda kigoma kutoka Dar imevunjika kioo chake kimoja na kuwa ATC iko katika harakati za kuagiza kioo hicho kutoka nje. Hadi leo kioo hicho hakijapatikana na abiria waliotakiwa kusafiri kwa ndege hiyo kwa pande zote mbili baadhi walirudishiwa pesa zao ili wafanye mipango mingine wale wasio na haraka wanaendelea kusubiri na wengine walisafiri kwa Precision Air mpaka Mwanza na Shinyanga....Ndio ATC hiyo kuna mtu aliwahi kuniambia ATC ni kirefu cha Any Time Cancellation...