Atayaweza majukumu huyu kweli?

Atayaweza majukumu huyu kweli?

utani huu, kwamba jamaa alikua anakula ugali tu na kuondoka?

Inawezekana si alikua anaenda mikono mitupo alafu wahehe wa zamani wakikua na kuburi sana

Sema jamaa anaweza kuwa alikula ahata mara tatu hapa wanawake hawahesabu kama wameliwa..
Angalau angekula mara15 hivi kwenye kumbukumbu angekuwepo
 
Habari zenu wanaMMU. Nina mpenzi wangu ambae nnategemea kuwa atakuwa baba watoto ila ana tatizo (mimi naliita tatizo). Ni kwamba yeye ni mfanyakazi wa kampuni moja binafsi,ni kawaida yake huwa anakuja kwangu mara nyingi nampikia chakula.

Anaweza akatoka kazini anapitia kwangu anakula then anaenda kwake.

Hakuna siku utamsikia anasema dia hela hii hapa kanunue mchele au hata yeye mwenyewe kwamba anapokuja abebe walau maji ya uhai, hana muda huo kabisa. Gharama zote nazijua mimi. Tena anaweza kudiriki hata kusema chakula nlichopika ye hakipendi.

Sasa nauliza eti huyu mtu majukumu anayajua? Hata tukiingia ndoani si atanitwisha majukumu yote huyu? Au labda nyie wenzangu mnaonaje tabia hii, ni ya kawaida?
Pole huyo marioo mwanaume yoyote lazma ajue majukumu yake chakula cha mtoto wa kike raha utoe pesa wewe unatuna huku unauliza mboga mbona chumvi ndogo sio unaenda na pumbu tu kama umekuta kimepikwa unakula halafu unaacha pesa ya mboga...n.b...mwanaume kumtunza mwanamke sio ombi wala msaada ni wajibu...sio mtu huyo piga chini mzigo huo
 
Umemdekeza ndo mana.. Siku nyingine pika ugali na kachumbali... Akilalamika sema hukua na hela uluchelewa kununua mboga uone kama atajiongeza... Au mwambie nunua vitu nikupikue kwako.
 
Pole ndugu, kwa kwel hizo si tabia za kiume kabisa si kwa mpenzi hata kwa rafiki wa kawaida wa kike, itakuwa mbaya zaidi kama ni mtu anayependa kulelewa, kiuhalisia wanaume wanaopenda kulelewa huwa hawahelewi kitu na huwa na tabia zote ambazo unaweza usizipende, jitahidi msomane kama hana mkwamo wowote kiuchumi jitahidi kuwa makini zaidi ni huruma sana kwa mdada kutendwa na mtu anayemlea🙂🙂🙂 tutafurahi pia kupata mrejesho kabdilika🙂🙂🙂. Tchao, kaka muuza nyanya
 
Sasa Hajakuoa Matumizi ya nini? Anafidia kwanza ale vya kutosha kabla Hujaanza Kula Vyake..
 
Duuhh...pole sana mamii umejua kumvumilia kweli hili li dubwana, vp ulivyomuacha hajakutafuta tena..?
ni afadhali umtose sasa hivi maana huyo ni dezo style. ki ufupi hawezi badilika hata mkioana. mie mchuchu niliyempiga kibuti alikuwa ana hiyo tabia, ni msomi na kazi ya mshahara mzuri tu sana. tena anatoa order tu mara oo nitengenezee mbuzi wa ku-roast, mara leo natamani maini ya kukaanga etc. kwa mwezi nilikuwa na-spend kama laki 2 na zaidi kumpikia tu yeye, kabla ya hapo matumizi ya misosi ya home yalikuwa elfu 50 tu kwa mwezi. hakuna hata siku moja alikuwa anapitia juisi wala soda wala nini. tena siku akikuta hujapika atanisimanga au akute nimepika ma-beans nitaambiwa hicho ni chakula cha ndege. tukienda out kula nalipa mimi, miaka miwili ikakatika hivi hivi, nikasema mimi siyo mama yake wala shangazi yake....i kicked his cheap a*** to ze left!
 
Mkuu naomba unifafanulie kidogo, maana kuna sister namfaham nae mwanaume aliyekua nae ni hivi sasa mshkaji kambwaga kaenda kwa mwingine. Huyo kaka anasema yule demu hana mvuto yaan dad's face.
We dada naona una inferiority complex,labda kwa sababu ya umri,au maumbile yako,au sijui nini.

Nakumbuka nikiwa form 5&6,Bado niliweza kumgharamia gfriend kwa pesa ya wazazi.je iweje kwa mgfanyakazi ashindwe! hapo ----- ni wewe sio yeye.pole
 
Habari zenu wanaMMU. Nina mpenzi wangu ambae nnategemea kuwa atakuwa baba watoto ila ana tatizo (mimi naliita tatizo). Ni kwamba yeye ni mfanyakazi wa kampuni moja binafsi,ni kawaida yake huwa anakuja kwangu mara nyingi nampikia chakula.

Anaweza akatoka kazini anapitia kwangu anakula then anaenda kwake.

Hakuna siku utamsikia anasema dia hela hii hapa kanunue mchele au hata yeye mwenyewe kwamba anapokuja abebe walau maji ya uhai, hana muda huo kabisa. Gharama zote nazijua mimi. Tena anaweza kudiriki hata kusema chakula nlichopika ye hakipendi.

Sasa nauliza eti huyu mtu majukumu anayajua? Hata tukiingia ndoani si atanitwisha majukumu yote huyu? Au labda nyie wenzangu mnaonaje tabia hii, ni ya kawaida?
Akija anakula nini, hujafafanua,
 
Back
Top Bottom