Atatamani awe wako

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
371,109
Reaction score
859,333
Kupenda ni sanaa
Kupenda ni hisia
Kupenda ni pepo, lakini kuhodhi moyo wa mtu ni kipaji.
Usitafute tu nafasi kwenye macho yake,
tafuta mizizi kwenye fikra zake.
Mfanye akukumbuke sio kwa sababu upo karibu,
bali kwa sababu ladha ya uwepo wako haipatikani kwingine kote.

Mnusanishe harufu ya upendo wa dhati,
mtazame kwa macho yanayosoma siri za nafsi yake,
na mpe tabasamu litakalobaki kama picha isiyofutika akilini mwake.

Ukigusa hisia zake kwa usahihi, hatatamani tu kuwa na wewe—atafanya kila uwezalo kuwa wako.
 
Kumpata sasa,
 
Kupendwa raha, ila usipendwe na mnafiki
 
 

Attachments

Huko Verona, mji wa kale nchini Italia, kulikuwa na koo mbili zilizochukiana kwa miaka mingi: Capulet na Montague.

Uhasama wao ulikuwa mkubwa kiasi kwamba kila walipokutana barabarani, mapanga yalichomolewa na damu ilimwagika. Katika mji huu uliogawanyika, hakuna mtu aliyeamini kuwa kuna kitu kizuri kingeweza kuzaliwa kutoka kwenye chuki hiyo, hadi usiku mmoja wa karamu ya siri.Romeo, kijana mtanashati kutoka ukoo wa Montague, aliingia kwa siri kwenye sherehe ya wakubwa wa ukoo wa Capulet.

Humo, macho yake yaligongana na ya Juliet, binti mrembo wa nyumba hiyo. Katika sekunde hiyo hiyo, chuki ya koo zao ilitoweka akilini mwao; ulikuwa upendo wa mara ya kwanza.
Baada ya sherehe, Romeo alipenya hadi kwenye bustani ya Juliet na kumkuta binti huyo kwenye balcony akilia kwa sauti kwa nini mpenzi wake lazima awe adui wa familia yake.

Romeo alijitokeza, na usiku huo, chini ya mwanga wa mwezi, walila kiapo cha kupendana milele.Wakijua kuwa familia zao zisingekubali kamwe, walimwomba Padri Lawrence uwafungishe ndoa ya siri siku iliyofuata.
Padri alikubali, akitumaini kuwa ndoa hiyo ingekuwa daraja la kuleta amani Verona. Hata hivyo, hatma ilikuwa na mipango mingine. Muda mfupi baada ya ndoa yao, ugomvi ulizuka mjini; Tybalt, binamu wa Juliet, alimuua Mercutio, rafiki wa karibu wa Romeo. Kwa hasira na uchungu, Romeo alilipa kisasi na kumuua Tybalt, kitendo kilichomfanya mkuu wa mji kumfukuza Verona moja kwa moja.Wakati Romeo akiwa uhamishoni, maafa mengine yalifuata. Baba yake Juliet aliamuru binti yake aolewe haraka na tajiri mmoja aitwaye Paris. Akiwa amekata tamaa, Juliet alikimbilia kwa Padri Lawrence ambaye alimpa dawa ya kumpoteza fahamu kwa masaa 42, ili aonekane amekufa na kuepuka ndoa hiyo, huku akituma mjumbe amwite Romeo watoroke wote.

Kwa bahati mbaya, mjumbe huyo alichelewa kwa sababu ya ugonjwa uliokuwa umezuia watu kusafiri. Romeo alipata habari kutoka kwa mtu mwingine kwamba Juliet amefariki na kuzikwa.Akiwa na majonzi mazito, Romeo alinunua sumu kali na kukimbilia kwenye kaburi la Capulet. Alimkuta Juliet amelala akionekana kama amekufa, akamshika mkono, akanywa sumu hiyo na kufa pembeni yake.

Dakika chache baadaye, Juliet alizinduka kutoka kwenye usingizi wa ile dawa na kumkuta Romeo akiwa tayari amekata roho. Dunia yake ilinyooka; bila kusita, alichukua kisu cha Romeo na kujidunga kifuani.
Miili ya wapendanao hao ililala pamoja milele, na kifo chao kikafungua macho ya koo zote mbili, ambao waliamua kuweka chini silaha na kumaliza uadui wao kwa machozi ya majonzi.
Kama penzi la Romeo na Juliet by William Shakespeare

Ila sasa hivi bila sapampa huwa hisia zao zinakuwa deactivated

Ijapokuwa katikati ya udongo na uchafu mwingi dhahabu inaweza kupatikana
 
Ausio saivi wanadeal na kipato,,ukichanganya na vikoba,mpeano ndio kabisaaa hawana hisia wamepagawa hata uwe na ueledi kiasi gani ngoma inadunda tu
 
Hakika walikuwa na mapenzi ya kweli wapendwa hawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…