Ataka serikali imkabidhi viwanda vyote Kilimanjaro

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
babu%20viberiti%20.jpg


Caption Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Viberiti cha Kibo Match Group Ltd, cha mjini Moshi, Sheriff Babu akitoa taarifa kwa mbunge wa viti maalumu kupitia Chadema Lucy Owenya, ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Viwanda, Biashara na Masoko aliyetembelea kiwanda hicho. (Picha na Daniel Mjema)

Daniel Mjema, Moshi
RAIA wa India, Sheriff Babu ameshangazwa na hatua ya viwanda vilivyojengwa kwa mabilioni ya dola za Marekani mkoani Kilimanjaro kufa wakati utafiti alioufanya unaonyesha vinaweza kufufuliwa na kuchangia uchumi wa nchi.

Babu ambaye ni Meneja wa Kiwanda pekee cha viberiti nchini cha Kibo Match Group, cha mjini Moshi alitoa somo kwa serikali namna ya kuviwezesha viwanda hivyo kufufuliwa kama wawekezaji waliouziwa wana dhamira ya dhati ya kuvifufua.

Raia huyo wa kigeni alisema kama atakabidhiwa viwanda hivyo ana uwezo wa kuvifufua na kuanza uzalishaji ndani ya mwaka mmoja ili mradi tu serikali ikubali nayo kubeba jukumu lake la kujenga mazingira mazuri ya uwekezaji.

Moja ya mambo ambayo raia huyo wa India alitaka serikali ifanye ni kubadili sera ya uwekezaji ili msamaha wa kodi wa miaka mitano (tax holiday) wanaopewa wawekezaji wapya nchini ili uwanufaishe pia wale wanaotaka kufufua viwanda.

"Kwa viwanda hivi vya mkoani Kilimanjaro, wala sihitaji msamaha wa kodi wa miaka mitano wanipe miaka miwili tu, viwanda vyote hivi vilivyokufa vitafufuka, nchi imelalia mabilioni ya dola hapa Kilimanjaro,"alisema kwa uchungu raia huyo wa India.
Sharti lingine ni kwa serikali kutoa mtaji wa uanzishaji uzalishaji na kubeba mzigo wa madeni yote ya nyuma ya viwanda hivyo ikiwamo michango ya NSSF na mafao ya watumishi ili viweze kuanza upya katika mazingira ya sasa.

Babu alikuwa akitoa taarifa ya changamoto zinazokikabili kiwanda cha viberiti cha Kibo Match kwa Waziri kivuli wa Viwanda, Biashara na Masoko, Lucy Owenya aliyetembelea viwanda kabla ya Bunge la bajeti mwezi ujao.

Mbali na mapendekezo yake hayo, Babu alisema kama serikali haitakuwa na uwezo wa kutoa mtaji basi, iwezeshe kupitia Benki ya Rasilimali (TIB) viwanda vikopeshwe mkopo wenye masharti nafuu utakaolipwa kwa muda mrefu.

Miongoni mwa viwanda alivyosema vinaweza kuanza uzalishaji sasa ni Interchem Pharm Limited (IPL) ambacho kina uwezo wa kuzalisha asilimia 60 ya mahitaji yote ya dawa nchini ambacho sasa kimefilisika na kimetangazwa kuuzwa kwa zabuni.

Viwanda vingine ni Kilimanjaro Machine Tools (KMT), Pestside Industries na Kiwanda cha Magunia (TBC) ambacho baadhi ya mitambo yake imeondolewa kiwandani.
 
Jamaa anaonekana kuwa na kibri kweli dhidi ya Serikali yetu "Mjinga".... Haya Bana!!
 
Nafikiri jamaa yuko sahihi kabisa. Kufufua viwanda vyetu tunaweza, ila inatokana na baadhi ya urasimu uliopo kwenye vyombo husika unashindwa ku-facilitate zoezi zima la ufufuaji wa hivi viwanda. Huwezi kuniambia kwamba Billioni 11 serikali ilizotenga zilishindwa kufufua kiwanza cha General tyre pale Arusha. Lakini kibaya zaidi hata haijulikani zitumikaje. Kuna haja ya serikali kuweka mikakati maalumu ya kufufua viwanda vyetu ikiwa ni pamoja kuweka mipango madhubuti ya kuvisimamia...
 
Jamaa kasema kweli kabisa kwamba viwanda vile vinaweza kufufuliwa. Suala la yy kufufua si baya kama inavyoonekana, cha msingi alichotoa ni kwamba hakuna nia ya dhati kwa serikali yetu kufufua viwanda.
 
Jamani,huyu mdosi ni mgeni na systems zetu za urasimu.
kiwanda kinapigwa zengwe na mawaziri ilii kife,then wao wakipige bei wapate 10 % zao,mfano hai ni jinsi kiwanda cha sungura textiles pale gongo la mboto,shirika letu la ndege ATC aliyekuwa waziri mwenye dhamana ndio huyo huyo aliyekuwa na hisa nyingi tu ndani ya precision.Tuangalie kwa nini TTCL mobile inazorota nyuma ya akina vodacom ,simple shareholders wa vodacom ndio viongozi wa chama na serikali.

wazo langu:Huyu mdosi wa india yuko sahihi na anao uchungu wa mali inavyopotea,asichokijua ni kuwa InJi hii ilimshinda Mrema Lyatonga enzi za siku7,nothing will happen mpaka wakulu wapate Ten parcent zao
 
kila kitu kinawezekana ikiwa tutakuwa na maamzi mazuri mwaka 2015 kwenye sanduku la kura
 
Jamaa anaonekana kuwa na kibri kweli dhidi ya Serikali yetu "Mjinga".... Haya Bana!!
Inawezekana ana kibri lakini pia ameonesha udhaifu wa serikali yetu katika kufufua viwanda.

Lakini ni vyema kuangalia perfomance ya hicho kiwanda cha Kibo kilichopo chini yake..kama kinafanyakazi vizuri na kimetoa ajira kwa wananchi basi tuichukulie kauli yake kama ni uamsho badala ya kibri.

Serikali haina kipaumbele cha kuwawezesha wazawa kuwekeza katika viwanda,inapendelea wageni.
Kama ameweza kwa Kibo basi ataweza kwa vyengine..lakini mbinu au masharti aliyoyatoa yanaweza kuisaidia serikali katika kuwawezesha wazawa ili viwanda hivyo vifufuliwe na hatimae kutoa ajira kwa watanzania na kusaidia katika ustawi wa mtanzania na Tanzania.
 
Hivi viwanda vimekufa kutoka na watu wachache wanataka tuendelee kuwa dump.

Hilo wazo lake la mitaji au mikopo kila nikikumbuka Rites,Chavda and the like naishiwa nguvu.
 
Back
Top Bottom