Elections 2010 Atagombea wapi?

Anaweza asigombee, akawa mbunge mteuliwa kwani raisi anayo nafasi ya kuteuwa wabunge kumi.
 
Huyu kijana kaingia kwa moto kwenye siasa akifuata staili ya baba yake ya makundi na mitandao. sizani kama atadumu ninachokiona mbele ni wingu zito baada ya baba yake kuondoka. Kwa sasa anaweza kupewa chuuo chochote anachotaka kwa sasabu hakuna wa kumzuia.
 
Mwanakijiji

You are too fast..Yes even January atapata unaibu waziri katika wizara Nyeti..Yes we Know..Nadhani Ridhwani atateuliwa,kugombea ni kumpa kazi kubwa sana
 
Mzee mwenzangu Gembe, atagombea (somewhere in Pwani....i guess) ili apate legitimacy ya kupewa unaibu. Kuteuliwa itakuwa ni kubebwa kulikotukuka. Lakini ndiyo demokrasia ndani ya CCM.
 
Anaweza asigombee, akawa mbunge mteuliwa kwani raisi anayo nafasi ya kuteuwa wabunge kumi.
Japo JK is not genius, he is not this cracy to do such a thing!. Anaweza kuwateuwa watoto wa rafiki zake kama alivyofanya kwa yule kijana, lakini hawezi kumteua mwanaye mwenyewe.

Ila kija, ana uhuru wa kugombea na kuchaguliwa kama walivyo Watanzania wengine, ila JK hawezi kumteau katika wadhifa wowote, not while on power, bali anachoweza kufanya JK ni kumkabidhi kwa Membe ili kwenye awamu ijayo ndipo aukwae na kuendelea kupanda juu, ndivyo alivyofanya Mwinyi, baada ya kuondoka, kijana akaingia, na ndivyo atakavyofanya Karume, Ali atapewa uwaziri fulani, na ndivyo atakavyofanya JK, kumkabidhi kwenye mikono salama.
 
Anaweza asigombee, akawa mbunge mteuliwa kwani raisi anayo nafasi ya kuteuwa wabunge kumi.
Jamani JK is not that crazy!.
Ningekuwa mshauri wa first family, ningemshauuri kijana akapige LL.M Havard au Yale, akirudi akatingishe kidogo mahakamani kujenga jina kitaaluma, 2015 aingie ulingoni na unaibu, 2020 Waziri kamili, 2025 atakuwa ameshaiva kiasi na kubisha hodi kuingia sebuleni.

Lazima tufike mahali tuanze kukubali, kuna baadhi ya familia nyota ya siasa na uongozi, zinawang'aria kama kina Kenedys, Bush etc, hapo Kenya kuna kina Kenyata na Odinga, Tanzania tulikuwa na kina Nyerere na Kawawa, enzi zao ndio hizo zinayoyoma na nyota mpya ya kina JK ndiyo inayong'ara kwa sasa.
 
Japo JK is not genius, he is not this cracy to do such a thing!. Anaweza kuwateuwa watoto wa rafiki zake kama alivyofanya kwa yule kijana, lakini hawezi kumteua mwanaye mwenyewe.

Ila kija, ana uhuru wa kugombea na kuchaguliwa kama walivyo Watanzania wengine, ila JK hawezi kumteau katika wadhifa wowote, not while on power, bali anachoweza kufanya JK ni kumkabidhi kwa Membe ili kwenye awamu ijayo ndipo aukwae na kuendelea kupanda juu, ndivyo alivyofanya Mwinyi, baada ya kuondoka, kijana akaingia, na ndivyo atakavyofanya Karume, Ali atapewa uwaziri fulani, na ndivyo atakavyofanya JK, kumkabidhi kwenye mikono salama.

I real dont know if it has something to do na ugenius? It think .....has something to do with something else!!!?? Museveni na mkewe!!!! Omar Bongo na mwanaye...Mubarak na mwanaye au hawa wapo kwenye usultani? nadhani nao wana domokrasia hii hii ya Viama vingi etc
mix with yours
 
Bongo kila kitu urithi......Anaweza asigombee ila akaandaliwa mahala pake pazuri koz the guy ni advocate sasa.....within these five yrs MAY be ataukwaa UJAJI....Who Knows????
 
Aende JKT apate uzalendo kidogo wa nchi,then atakuwa bomba kwenye politics.
 
Kwa JK hakuna kisichowezekana, hana haya, anaweza kumteua kuwa mbunge, wala sishangai! Baba mkuu wa nyumba, mama mjumbe wa mkutano mkuu wa nyumba, mwana mjumbe wa nyumba. Uliona wapi kwingine zaidi ya TZ?
 
I mean Ridhiwani. Maana anaweza akaukwaa Unaibu Waziri fulani hivi... I know you think I'm crazy..

Si Unaibu waziri tu, anaweza akawa waziri kamili n a hata kuwa Rais baadaye.
LAANA KUBWA WALIO NAYO VIONGOZI WENGI NI HII YA KUWARIDHISHA WATOTO WAO UONGOZI HATA KAMA HAWNA UWEZO WA KUONGOZA, na mbaya zaidi wanawaridhisha na tabia za wizi/ufisadi na mambo mengine ambayo kwa mzazi mwenye hekima hasingemridhisha mtoto wake.
 
I mean Ridhiwani. Maana anaweza akaukwaa Unaibu Waziri fulani hivi... I know you think I'm crazy..

Anaweza kuwa mbunge wa kuteuliwa, rais ana nafasi 10 kikatiba na hakuna wa kuuliza kigezo alichotumia kuteua huyo mbunge. Mwanakijiji you are not crazy and i wouldnt be surprised in Tanzania the unexpected always occures and the expected never happens.
 
Si LAANA KUBWA WALIO NAYO VIONGOZI WENGI NI HII YA KUWARIDHISHA WATOTO WAO UONGOZI HATA KAMA HAWNA UWEZO WA KUONGOZA, na mbaya zaidi wanawaridhisha na tabia za wizi/ufisadi na mambo mengine ambayo kwa mzazi mwenye hekima hasingemridhisha mtoto wake.
.
Ulimbo, tuweke na mipaka basi ili isije onekana ni chuki binafsi dhidi ya watoto wa viongozi. Uongozi haurithishwi, ni ama kipaji mtu anazaliwa nacho (born leader) kama kina Nyerere au na maandalizi, groomed leaders (man made) kama kina JK .

Hao vijana wanauwezo wao binafsi waliozaliwa nao, ndio maana wanafuata nyayo za wazazi wao. Issue iwe ni uwezo wa uongozi ndio uwe msingi wa mjadala na sio ni mtoto wa nani. Mimi binafsi nawakubali baadhi ya vijana wote wenye uwezo na kuamua kutangaza nia, hata kama majina yao ya ubini ni mtaji.

Kwa mfano, binafsi namkubali sana huyu kijana Nape, amesimama independently kuhesabiwa na sio kwa mgongo wa baba, japo katika harakati za Ubungo, nina side na JJ.Myika.

Kuna issue ya kuwa na kipaji cha uongozi, kijana Riz alikuwa kiongozi pale UDSM, wakati huo baba hajaingia Magogoni, kama ana interest, na ana uwezo, kwanini asigombee?!. Yaani apoteze haki yake ya kuchagua ama kuchaguliwa eti kwa sababu tuu baba ni fulani?. No way!,

Mbona Vita yuko mjengoni?, nenda Riz nenda Janu pia nenda, Nape nae aende, kama Fred ana interest pia aingie, William pia aingie, Kina Steve na Niko pia kama wana interest nao waacheni waingie. Tuwahukumu hawa vijana with their own merits na sio kutokana na majina yao ya ubini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom