Atafia mikononi mwangu

Atafia mikononi mwangu

Muuee tuu coz akipona ataua wengne wengi,nakuomba na nakusihi dokta nakuomba sana muue huyo jamaa,me ucpomuua utaniboa sn,plizpliz kill him au kama unashnda niite nmuue me mwenyewe
 
acha use nge, mtibu huko
Kisasi kinalipwa kwa mtu anayejiweza, unakuwa coward wa kufa mtu.

In my life, siwezi lipa kisasi kwa siri, nikilipa nitataka ujue ni mimi, ili kama unamashambulizi uyaelekeze sehemu muafaka.
 
Usifanye hivyo, usichukuwe sheria mikononi mwako.

Wewe ni Daktari na msomi unaweza kutumia njia nyingine za kisheria huko mbele ya safari. Kwa kuwa ni vigumu wewe kumtibu kama mgonjwa mwingine yeyote yule call in sick ukapumzike uwaachie wengine wamshughulikie.

Kumbuka, kama kifo cha rafiki yako kimekutesa basi cha wewe kuuwa kwa makusudi kitakutesa zaidi.

Don't do it.
 
Usiue usiue usiue usiue namuomba Mungu sauti hii ikusumbue mpaka uache hicho unachofikiria. Kumbuka hakuna mwenye haki ya kuutoa uhai wa mtu mwingine au kulipiza kisasi. Huyo rafiki yako alipoamua kufanya biashara haramu je unajua ni wangapi walidhurika/kufa kwa sababy ya yeye kukubali kuingia kwenye dili. Kumbuka ziko njia nyingi zionekanazo nzuri machoni pa mtu lkn mwisho wake ni mauti. Pia elewa kuwa ukiingia chama cha wachawi huwa hawatokagi , kama utatoka basi adhabu yako ni kifo na ndicho kilichomtokea rafiki yako. Ni heri ukafanya sehemu yako kama dr na Mungu atakulipa. Hebu jiulize utalipa visasi vingapi chini ya jua hili. Uko udhalimu mwingi mno pengine hata hao uwaonao wema machoni pako ukifunuliwa watendayo sirini hutaamini na utasema kama ndio hivi basi vitu vyote ni ubatili.
 
Ni bora kuokoa maisha ya vijana wetu maalfu kwa kuondoa huyo mmoja

in fact utakua hujaua, utakua umekamilisha tu safari yake maana tayari keshaisha....

hakikisha kabla hajafa rasmi unamfanya ajue kuwa aliua na ni muuaji wa vijana through madawa ya kulevya

tunalea sana ujinga
 
Usifanye hivyo, usichukuwe sheria mikononi mwako.

Wewe ni Daktari na msomi unaweza kutumia njia nyingine za kisheria huko mbele ya safari. Kwa kuwa ni vigumu wewe kumtibu kama mgonjwa mwingine yeyote yule call in sick ukapumzike uwaachie wengine wamshughulikie.

Kumbuka, kama kifo cha rafiki yako kimekutesa basi cha wewe kuuwa kwa makusudi kitakutesa zaidi.

Don't do it.

hawa watu (maawa ya kulevya) wameshashinda mamlaka karibia zote dawa yao ni elimination tu

kama dini zilienezwa kwa upanga, ubinadamu gani huu tulionao wa kulea wauza madawa ya kulevya tena wauwaji wakubwa??

hii ni hypocrisy ya hali ya juu

DR. USIUE HUYO MGONJWA, MSAIDIE TU AISHIE... UTAKUA HUJAUA ILA TECHNICALLY UTAKUA UMEFANYA MEDICATION ERROR
 
Hata ukimuua rafikiyo hatarudi na kifo chake hakita undo yaliyokupata maishani.
Msamehe tu umtibu,hukumu yake atakutana nayo kwa aliyemuumba.
USIHUKUMU
MNAWAZA HUYO RAFIKI TU.... HIVI MNAJUA WATU WANGAPI WANATEKETEA KWA MADAWA YA KULEVYA??? mnajua huyo jamaa kaua wangapi?? na si ajabu ni mfadhili wa wanasiasa

he deserves to die
 
Usifanye hivyo, usichukuwe sheria mikononi mwako.

Wewe ni Daktari na msomi unaweza kutumia njia nyingine za kisheria huko mbele ya safari. Kwa kuwa ni vigumu wewe kumtibu kama mgonjwa mwingine yeyote yule call in sick ukapumzike uwaachie wengine wamshughulikie.

Kumbuka, kama kifo cha rafiki yako kimekutesa basi cha wewe kuuwa kwa makusudi kitakutesa zaidi.

Don't do it.

Ni busara kubwa sana hii mama mzazi!
 
MNAWAZA HUYO RAFIKI TU.... HIVI MNAJUA WATU WANGAPI WANATEKETEA KWA MADAWA YA KULEVYA??? mnajua huyo jamaa kaua wangapi?? na si ajabu ni mfadhili wa wanasiasa

he deserves to die
Na unafikiri kumuua huyu kutaua huo mtandao wa madawa?
Madawa ni janga ila kumuua huyu si dawa ya kutokomeza janga hili.
Akimuua huyu hatopata amani kamwe!!!
 
USIUE PLZ USIUE DR.
acha kabisa shetani hilo la kuua likutoke uakuja kuumia sana rohoni na itakutesa

pole sana omba dr mwingine amwagalie na kumtibu
 
Mimi ni Daktari wa hospitali moja kubwa binafsi hapa Dar es salaam mzaliwa wa kanda ya ziwa na huu ni mwaka wangu wa pili kazini. Nilikua na rafiki yangu sana ambae sasa ni marehemu. Huyu rafiki yangu tulipendana sana kwa vile tulikua majirani na hata wazazi wetu walikua marafiki pia. Tulisoma wote shule ya msingi hadi A level mkoani Mtwara.

Baada ya kumaliza kidato cha sita sote tulifaulu vizuri na kubahatika kujiunga na masomo ya elimu ya juu hapa hapa Dar kusomea udaktari. Tukiwa mwaka wa kwanza rafiki yangu alibadilika sana na alinishtua sana aliponiambia kua ameamua kuhairisha masomo amepata kazi kwenye kampuni ya kuuza magari. Nilimshauri na kumsihi aendelee na masomo lakini hakubadilisha uamuzi wake.

Alianza kusafiri sana nje ya nchi, mara Afrika kusini, India, China, Brazil, Marekani n.k. Nilienda kuishi nae kwake baada ya kupanga nyumba nzima. Alinipeleka chuo kwa gari lake na kunirejesha kila alipopata nafasi. Niliishi maisha mazuri kiasi ingawa ilikua siri nyumbani hawakujua kama rafiki yangu alisitisha masomo. Skuwahi kupajua anapofanya kazi, kila nilipomwambia anipeleke hakukubali.

Sku moja usiku wa manane nikiwa mezani najisomea na yeye akiwa chumbani kwake alipigiwa sim na mtu ambae walijibizana sana huku kaka akisistiza kua amechoka kusafirisha dawa za kulevya anaacha. Niliogopa sana, niliondoka taratibu na kwenda kulala chumbani kwangu ili asigundue kua namsikiliza. Skupata usingizi kabisa. Asbuhi alionekana mwenye mawazo na hasira nyingi tofauti na siku zote. Nilimuuliza kulikoni akanambia ana mgogoro na bosi wake, nilmuuliza kwani huyo bosi anaishi hapa nchini akasema ndio na kunionesha picha yake kwenye sim.

Kama kawaida alinipeleka hadi chuo, aliponishusha na kuondoka nikachkua taksi na kuanza kulifuata gari lake kwa nyuma, Nilidhamiria kupajua anapofanyia hizo kazi zake. Sku hiyo ndio siku niliposhuhudia rafki yangu akipigwa risasi na mtu aliyekua amepakizwa kwenye pikipiki (Ni yule nilooneshwa na rafki yangu kwenye picha), na kufariki hapohapo. Baada ya kifo cha rafiki yangu yalitokea mambo mengi sana ikiwa ni pamoja na mimi kuachishwa masomo kutokana na kua sehemu ya washukiwa, kuparaganyika kwa familia zetu n.k.

Usiku wa kuamkia leo hapa hospitalin ameletwa mtu yuleyule aliyemuua rafiki yangu na kusababisha misukosuko mingi katika maisha yangu akiwa hoi kwa presha ya kupnda. Sijawahi kufikiria kuua katika maisha yangu ila kwa sasa dhamira inanituma nimchome sindano ya sumu, nimtundike dripu ya glucose, nimuoverdose au ninyonge kabisa.

Najua bdo una machungu bdo lkn ukumbuke hatujapewa hyo hukumu ya kuua xo kazi kwako umtibu or kill him de decision iz in ur hand bro
 
Ni hadithi au? Nyway,mungu pekee ndo mwenye kutoa hukumu utapata dhambi za bure muhudumie tu kama wagonjwa wengine.
 
Najua bdo una machungu bt ukumbuke hatujapewa hyo hukumu xo ur decision iz in ur hand kumtibu or kill him
 
Hongera kwa kushirikisha jukwaa,mungu ana hekma na wewe.Mungu ndo hakimu wa haki.
 
Ni bora kuokoa maisha ya vijana wetu maalfu kwa kuondoa huyo mmoja

in fact utakua hujaua, utakua umekamilisha tu safari yake maana tayari keshaisha....

hakikisha kabla hajafa rasmi unamfanya ajue kuwa aliua na ni muuaji wa vijana through madawa ya kulevya

tunalea sana ujinga

Unachosema kina mantik lakini asijichukulie sheria mkononi akiwa kazini kwake.
 

Mkuu,
Utampigaje mtama mtu ambaye tayari ameanguka chini?

Kutoa uhai wa mtu makusudi pasi kuwa na mihadarati kichwani yahitaji moyo.

Nafsi ya hatia itakuandama Sana maana hata hao majambazi na wachawi Kuna pilika hufanyika baada ya kutoa uhai wa mtu.

If you're ready for that then go ahead!!
 
Najua how u feel, kuona maisha ya rafiki yako yanakatishwa hivi hivi. Na bado kwa kuwepo hai kwake maelf elf ya maisha ya vibaya yanaharibiwa kama siyo kufa kabisa. Huyo rafiki yako likuwa punda, kaleta sana mizigo ambao imeangamiza vijana wengi sanaa

Nakushauri, kwa imani yako kwa muumba wako, muombe akupe njia sahihi huku ukijua yeye ndiye mtoa hukumu mkuu!
 
Back
Top Bottom