Chanya.
Muungano ukivunjika kila nchi na kila mwananchi, kila mtu atarudi katika uhalisia wa siasa, uhalisia wa maisha.
Kwa wa "visiwani" kama hii unamaanisha Zanzibar hao wabunge watakaorudi kwao wanaweza kuchaguliwa kuwa mabalozi wa Zanzibar nje ya nchi au UN au katika regional bodies nyengine kwa wale wenye sifa na uwezo wa kazi...lakini wanaweza kuamua kuchukua uraia wa Tanganyika.
Kama speaker post #3 alivyosema Tanganyika inarudi na siasa za "kujivua magamba" itabidi zikome, siasa za usanii, janja na mazingaombwe na sababu za "kiintelijensia" zitakuwa zimepatiwa dawa.
Lakini la faida kuu ni kwa wananchi wa nchi mbili, nchi ya Tanganyika kujua nani wa kumkabili, wa kumshushia ghadhabu zao, kwani viongozi watakuwa ni viongozi wa Tanganyika na sio kama sasa kujifanya wao ni viongozi wa Tanzania, nchi ya kufikirika tu kitu kinachowafanya kutokuwa na uchungu na nchi na maliasili zake.
Na wananchi wa Zanzibar nao hawatapewa tena sababu za "muungano unaibana Zanzibar". Viongozi wa huko wasipowajibika watakumbana na ghadhabu ya wananchi, huenda wakatiwa moto kama vibaka.
Chanya, Muungano ukivunjika itakuwa hakuna tena shamba la bibi .Tanganyika itakuwa na wenyewe,wananchi wa nchi ya kikweli Tanganyika.
Kufufuka kwa Tanganyika itakwenda sambamba na kuwa na katiba mpya ya Tanganyika ambayo katika kuandikwa kake itahakikisha kiongozi mzembe anawajibishwa anaposhindwa kujiwajibisha. Sheria ya upokeaji rushwa na ufisadi itakuwa kama hukumu ya China.
Mimi naona unachelewa mbona kuvunjika?