Assad akiwatembelea wanajeshi wake

Assad akiwatembelea wanajeshi wake

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
21,765
Reaction score
71,801
Wasalaam ndugu zangu,
Hii video nimeiangalia na kuna vitu vimenifanya niwaze sana.
Watu wanasema Assad ni dikteta na hata kama kweli yuko hivyo ni viongozi wachache wanaweza kupendwa hivi na raia wake wakati nchi iko kwenye lindi zito la vita vya wenyewe kwa wenyewe tokea mwaka 2011. Ameenda kuwatembelea wanajeshi kwenye uwanja wa mapigano na hata ukiona jinsi walivyompokea utahisi kabisa wanampenda kiongozi wao.

Kikubwa zaidi amejishusha na kukaa kula nao bila hofu yoyote,
Kiongozi ambaye hajiamini hata chakula tu angeogopa kula kwasababu anajua madhambi yake,
mfano mzuri tu hapa Afrika hata kwenda kuwona Madaktari wetu katika hospitali ni mbinde sana.
Tuachane na udikteta na mengine yote lakini Assad anapendwa na kuheshimika sana, maana asingefika leo. Kikubwa ni kwamba wanajeshi hawaasi na kila siku raia wanajitolea kujiunga na jeshi la Syria.

CC: Consigliere , Bukyanagandi , Richard , MSEZA MKULU
 
Hakuna mtu anaechukuwa wala anaependwa,
Ninachojua ni kwamba wapo wanakupenda na wapo wanakuchukia sema asilimia zinatofautiana kuchukiwa na kupendwa, endapo wanaokuchukia wakiwa 50.5% na wanao kupenda wakiwa 49.5% basi watu husema anachukuwa.
 
Kushindwa kumuondoa madarakani Assad hadi leo kuna dhihirisha nguvu ya Iran katika ukanda huo.. Nchi za Magharibi ziliwaondoa kirahisi Viongozi wa Sunni katika nchi zao kama Gaddafi, Mubarak, Rais wa Tunisia, Saddam lakini washia kwa umoja wao chini ya nguvu ya Iran walikataa Assad kuondoka hadi leo..mbali ya America kupenyeza ISSIS
 
Mimi kuna video nimetizama watu wanamlaani Assad vibaya sana mpaka vitoto vinamlaani

Mkuu siku zote jeshi ni tiifu kwa amiri jeshi mkuu sababu wao hulipwa mshahara na rais ,huwezi kusema Assad anapendwa kisa jeshi linamheshimu.

Na waovu siku zote hupendwa na jeshi sabb ya $$

Chukua sample ya wananchi

Syria asilimia 80 wanamchukia Assad tena hv ss chuki dhidi ya Assad ndio imezidi wanaamini yeye ndiye ameua watu wengi kwa drones zake

Na natabiri japo urusi kamsaidia sana ila bado rising zitakuwepo nyingi.
 
Hakuna mtu anaechukuwa wala anaependwa,
Ninachojua ni kwamba wapo wanakupenda na wapo wanakuchukia sema asilimia zinatofautiana kuchukiwa na kupendwa, endapo wanaokuchukia wakiwa 50.5% na wanao kupenda wakiwa 49.5% basi watu husema anachukuwa.

Nimekuelewa mkuu,
Upendo siku hizi siyo Abstract Idea tena umekuwa Tangible hadi unaweza Quantify kwa kutumia hesabu za alimia,
Naomba nikupe hongera zangu za dhati kwa kugundua mbinu mpya ya kupima Abstract Ideas kama Upendo,
Wewe ni mtu wa kipekee sana.
 
Mimi kuna video nimetizama watu wanamlaani Assad vibaya sana mpaka vitoto vinamlaani

Mkuu siku zote jeshi ni tiifu kwa amiri jeshi mkuu sababu wao hulipwa mshahara na rais ,huwezi kusema Assad anapendwa kisa jeshi linamheshimu.

Na waovu siku zote hupendwa na jeshi sabb ya $$

Chukua sample ya wananchi

Syria asilimia 80 wanamchukia Assad tena hv ss chuki dhidi ya Assad ndio imezidi wanaamini yeye ndiye ameua watu wengi kwa drones zake

Na natabiri japo urusi kamsaidia sana ila bado rising zitakuwepo nyingi.

Hongera sana mkuu,
Kwa kuamini kwamba vitoto vina utashi wa kuweza kutambua mema na mabaya yanayoendelea Syria.
Lakini hata mimi pia nilishawahi kuona video ya CNN, FOX NEWS,CBS, zikisema zaidi ya asilimia 80% ya Wamarekani wanampenda Hillary Clinton na Angeshinda kwa asilimia 55% dhidi ya Trump.

Hapa chini nimekuwekea Video nyingine ya vitoto vya Kimarekani,
Vinamlaani Donald Trump.
 
Sasa aleppo ishachukuliwa na assad bado idlib

nasubiria mvua za bunker buster, cluster bombs, phosphorus bomb, napalm, precised guided missile zote zianze kunyesha palymira usiku na mchana kama gharika la siku za nuhu
 
Mimi kuna video nimetizama watu wanamlaani Assad vibaya sana mpaka vitoto vinamlaani

Mkuu siku zote jeshi ni tiifu kwa amiri jeshi mkuu sababu wao hulipwa mshahara na rais ,huwezi kusema Assad anapendwa kisa jeshi linamheshimu.

Na waovu siku zote hupendwa na jeshi sabb ya $$

Chukua sample ya wananchi

Syria asilimia 80 wanamchukia Assad tena hv ss chuki dhidi ya Assad ndio imezidi wanaamini yeye ndiye ameua watu wengi kwa drones zake

Na natabiri japo urusi kamsaidia sana ila bado rising zitakuwepo nyingi.
Mimi pia kuna mkanda nimeangalia yaani Assad mpaka anabebwa na vitoto vya chekechea na vikagoma asiondoke!!
 
Mimi pia kuna mkanda nimeangalia yaani Assad mpaka anabebwa na vitoto vya chekechea na vikagoma asiondoke!!
Unajua free Syrian army ni wa Syria wazawa kwanini wapo maalfu na maalfu wanamkataa Assad vitoto,vikongwe,vijana

Hakuna kitu cha namna hicho ,magorofa yote yaliyogeuka kuwa magofu ni sababu ya ndege za Assad na maalfu ya watu wamekufa kwa drones..watu wengi hawajaondoka allepo sabb ya waasi,sabb iliyowaondoa ni makombora,ndege za Assad

Kubali au kataa wa Syria wengi wana maumivu na grudge kwa Assad
 
Mimi amenifurahisha tu kuwagomea Marekani na washirika wake kwenye hili sakata! Bahati yao kwa Gadaffi; Putin alichelewa kidogo tu kumwunga mkono naamini angekuwapo mpaka leo hii!
 
Hata Idd Amin alikua anapendwa na wanajeshi wake na raia mkuu.

Hapo jirani Nkuruzinza anapendwa na jeshi lake vizuri tu.

Lakini ukiangalia kwa jicho la 3 utaona ni maigizo tu.

Hata Pogba wetu si anapendwa au

[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Back
Top Bottom