Aslay ana tatizo gani, mbona simuelewi?

sangujoseph

Senior Member
Nov 30, 2015
164
183
Hivi mnamuelewa Aslay, labda nianze kuwauliza ndugu zangu, maana nilishafikiria Sana mpaka nimeona niwasharikishe na nyinyi.

Aslay ni Moja ya Wasanii Wazuri Sana Bongo na wanakipaji cha Hali ya juu Sana, na waswahili wa Mtaani wanamuelewa sanasana nadhani Kwa sababu wanamjua Mswahili mwenzao kama ambavyo Mimi nilipata bahati ya kusoma naye pale Tandika Sekondari (Hapo nimejipa minyama mngejuaje sasa kama nimesoma na Star ).

Tuachane na hayo Kwanini nasema simuelewi Aslay naona kama bado anajitafuta wakati nadhani kuna hatua Fulani ambayo alikuwa kashaifikia kwenye muziki kiasi Kwamba alikuwa namba 3 yaani ukimtoa Mondi na Kiba anayefuata ni yeye, sijui hapa Kati ikawaje lakini nikaona graph yake ikiwa imestack na sielewi anachofanya kwenye muziki.

Nimefuatilia nimegundua tangu Mwaka huu uanze nadhani anatoa Ngoma kila mwezi ambapo kwa sasa anangoma karibia 5 Kwa 2020 sio mbaya kwa sababu hata Harmonize naye anafanya hasa baada ya kutoa Album ya Afro East.

Siikumbuki mara ya mwisho nimesikia interview yake kwenye Radio, TV, Blog ukitacha wakati alipotoa Ngoma yake na Alikiba ya Bembea na alipofanya Homa TVE.

Ngoma ya mwisho kutoa Aslay ilikua mchepuko ni Kali lakini ilipita kimya kimya sio hiyo tu ni nyingi ambazo akishatoa mnaweza msisikie chochote. Moyo Kiburi Mateka Kilanga Komo Rudi Darasani Mchepuko

Sijui tatizo ni nini kama nilivyosema simuelewi Japo nilijaribu kuwauliza baadhi ya wadau wa muziki walinijibu Kwamba Mwana anadai amekuwa Mkubwa hafanyi Interview na media yeyote na Ngoma wazifuate YouTube, kama ni kweli nadhani Aslay bado anaamini yeye ni namba 3 kwenye muziki

Kama anaamini hivyo anakosea sana Kwa sababu zamani nilikuwa nikisikia Sana Ngoma zake kwenye Bodaboda, vibanda vya simu Ila now sizisikii tena na hata huko YouTube anapotegemea mara nyingi huwa hazikai Trending Kwa muda mrefu, pia akumbuke game hapakati imechange sana kuna mtu anaitwa Konde Boy Mjeshi MARIOO wanahasira sana wanapiga interview hata na sisimizi, na wanafanya poa kila Kona.

Nadhani Aslay anahitaji kunielewesha kwenye hili bila hivyo, siuoni Ubora wake tena kwenye muziki au labda kama ameamua kubadilisha biashara na si muziki tena.

Insta : FB : Twit : Sangu Joseph

 
Hivi kumbe bado anaimba ? Nina siku sijaskia nyimbo zake, ukishuka wenzio wanapanda, yule Enock ndo kawa mjasilia mali mazima simsikii tena ata kiki za harmorapa
 
Lawama watapewa WCB mng,lkn mwanzo alivyokuwa anang'aa sifa alikuwa anapewa meneja Maneno.Aslay Kafeli kwenye management huwezi kutoa hit song 14 ndani ya mwaka mmoja,kama angekuwa anatoa tatu kali na mbili za kawaida kila mwaka Aslay mpaka sasa angekuwa bado wa moto.

Wenzake wana rekodi nyimbo nyingi alafu unachanganya kali na za kawaida wakati wa kutoa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom