Askofu Steven Munga: Tulia Ackson ameizika CHADEMA mazishi ya Kikristo

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,273
Kauli ya Baba Askofu Rev.Dr.Stephen Munga (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, baada ya Naibu Spika kushiriki igizo la kuizika Chadema.
______________
Naibu Spika (Dr.Tulia Ackson) ameizika Chadema mazishi ya Kikristo. Tunamshukuru kwa kuudhihaki msalaba.

Mungu amrehemu!

1569256755426.jpeg
 
Maombi yangu kwa MUNGU ni aniondolee ubatili na uongo; Asinipe umaskini wala utajiri; Anilishe chakula kilicho kadiri yangu.

nisidhibe nikakufuru Nikasema, MUNGU ni nani? Wala nisiwe maskini sana nikaiba, Na kulitaja bure jina la Mungu wangu.
Na kufanya matendo kama ya bibi Tulia
 
Naibu spika msomi wa PhD, kufanya ujinga kama ule Si aibu kwake tu, bali kwa taifa, bunge na watu waliokaribu naye.
Ph.D za wabongo wengi, hususan za miaka ya karibuni, hazizingatii viwango hata vya heshima za kawaida tu.

Ndiyo maana hata rais ana Ph.D lakini ni msema ovyo.

Ni matokeo ya kulazimisha tamaduni za watu za usomi wa kupimwa kwa Ph.D katika mfumo wetu ambao umekaa kienyeji zaidi.

We mtu kalelewa kwa kubwengwabwengwa miaka yote, kasoma ukubwani kapata Ph D, wazo lake la kwanza anaona na yeye zamu yake kubwenga wenzie.

Huyo Spika inawezekana tamaduni zao zinaruhusu utani wa jadi wa kuonekana wa ajabu kwa mtu msomi. Najua kuna makabila Tanzania ukiwa na msiba, watani wa kikabila wanakuja kushikilia maiti mpaka uwape hela.

Sasa hapo anaweza kuwa anachanganya siasa, utamaduni, utani na usomi.

Lazima atoke na bomu la maangamizi ya halaiki, kama si nyukilia kabisa.
 
PhD za karne hii zina shida sana. Huyu msomi anatumia kodi zetu kusafiri mpk Mbeya kwenda kudhihaki ukristo jumla jumla hivi.

Askofu, Mungu amekwisha mrehemu huyo mweshimiwa maana inasemekana kati ya wale walioshiriki mazishi hayo ya kuukebehi ukristo wawili wamekuwa marehemu kweli kutokana na ajali waliyoipata wakitoka kuizika Chadema.
 
Dr. Munga uko sahihi sana kwakua ndivyo jinsi mafundisho yanavyotaka. KUTOUDHIHAKI MSALABA lakini mzee wangu hiyo ya maziko ni angle ndogo msalaba unadhalilishwa sehemu nyingi sana.

1. Kufungisha ndoa kwenye nyimbo SCENE. Hawa unakuta katika wimbo huo huo unamambo ya ajabu katika SCENE nyingine.

2. Mzee wangu watu wa makanisa wanapo tembea na watoto na wake za watu.

3. Mzee wangu hata wale wavuta unga kule amerika na kolombia huvaa misalaba wakiwa wanakula unga na bangi na miili yao ikiwa imejaa tatuu za mazombi.

NB
Double standard ni kitu kibaya sana, tafadhali Mzee wangu mulika na upande huu mwingine ili tuulinde msalaba Kama alama yetu kuu ya imani.
 
Back
Top Bottom