Milonji
Senior Member
- May 26, 2022
- 153
- 494
Salaam wapendwa.
Dk. Tulia Ackson Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sasa, aliwahi Kufanya kosa la KIIMANI akiwa katika harakati za kutafuta Ubunge.
Dk. Tulia aliwahi Kutumia Jeneza na MSALABA kama Ishara ya kuizika CHADEMA kwa Mkoa wa Mbeya.
Watu walipopiga kelele kwenye Mitandao ya Kijamii Dkt. Tulia hakujali kitu na akanyamaza kimya kama vile ni sawa na ni haki yake.
Majuzi mashabiki wa Simba wakarudia kitu kile kile tena kwa kuweka na Vionjo vya aina ya Mavazi vinavyofana na yale yanayotumika katika Misa na au Ibada Takatifu.
Watu wakiwamo na Viongozi wa Dini wakajitokeza hadharani kukemea dhihaka iliyofanywa na Mashabiki wa Simba.
Ukimya wa Dkt. Tulia kwa kosa lile la KIIMANI alilofanya inawezekana lilisababisha Washabiki wa Simba waone ni kitu cha kawaida wakaingia mkenge kwa kuiga na kuongeza vionjo vyenye makwazo zaidi. Inawezekana kabisa kama Dk. Tulia asinge shupava shingo yake wakati kwa kuomba Msamaha Simba wasingefanya Jambo lile. Dhihaka ndogo imetengeneza Dhihaka kubwa.
Simba waungwana wamechutama na Wameomba Msamaha. Naamini KIIMANI Wamesamehewa.
Dkt. Tulia ni wakati wako wa kuonyesha uungwana. Chutama na uombe Msamaha kwa kitendo kile ulichokuwa umefanya ili Jamii ijue kwamba lilikuwa Jambo baya na wasije Kufanya kama wewe.
Hili ni ombi langu kwako Dkt. Tulia Ackson popote ulipo.