Askofu Stephen Munga: Hatuwezi Kufungwa Midomo Kisa Maendeleo

Askofu Stephen Munga: Hatuwezi Kufungwa Midomo Kisa Maendeleo

IMG_20191122_183537.jpg
 
Askofu mkuu wa kanisa la kkkt dayosisi ya kaskazini mashariki amesema kuwa watanzania hatuwezi Kufungwa midomo ya kutetea haki za binadamu, demokrasia na utawala bora, kisa kuna mtu anasema analeta maendeleo. Ameyasema hayo katika sherehe za kutimiza miaka ishirini ya kituo cha sheria na haki za binadamu nchini. Ambapo ripoti ya hali ya haki za binadamu nchini ilijadiliwa. Bila woga wala kupepesa macho askofu Munga katoa maoni yake hayo ili hali hivi sasa viongozi wengi wa dini wamefunga midomo yao. Napenda nimpongeze baba askofu kwa kusimamia ukweli, Mungu ambariki sana.

Kazi ya dini ni tofauti na kazi ya uongozi wa Serikali. Sasa huyu askofu anatakiwa ku-concetrate na jukumu lake la dini kwa waumini wake. Swala la kuongoza awaachie wengine, yeye hana utaalam wa kuongoza Serikali na anaposema hakuna demokrasia au utawala bora anatumia vigezo gani? Je, anasikiliza majungu? Kama anao ushahidi aweke hadharani. Kuna viongozi wa dini tunafahamu wanachotewa mabulungutu ili tu waseme. Tanzania chini ya awamu hii utawala bora imeimarishwa vile vile democracy ya hali ya juu na haki za binadamu zinafuatwa. Wengi wanaolalamika ni wachumia matumbo yao. Yaani kila Dick, Tom and Harry wakipayuka kuna a bunch of imbiciles wanasheherekea. Wivu tu unawasumbua.
 
Huo ndiyo uhuru wa kutoa maoni; askofu amaweza kuongea anayodhani ni sahihi, na kwa maana hiyo ametumia haki yake ya kutoa maoni. Ni vema pia akatambua kuwa na wengine wanayo haki hiyo kusema wanachodhani ni sahihi, hivyo aache tabia ya kushambulia wengine wakitoa maoni bali kuheshimu maoni yao hata kama hakubaliani na maoni hayo.

Nilimsikia akisema kuwa, mtu akiropoka basi maoni yake yanapuuzwa; hivyo hata yeye ajue yake yakipuuzwa ameropoka.

Aidha sivyema sana kuwa unatoa maoni yako kwa uhuru, na katika jukwaa hilohilo unasema unazuiliwa kutoa maoni.
 
Back
Top Bottom