Askofu Shao amfananisha Rais Magufuli na Robert Mugabe wa Zimbabwe... ataka watanzania tumuunge mkono!

Huyu askofu shoo anajua arusha kuna biashara ya kununua watu kama biadhaa?
Au anazungumzia rushwa gani?
 
Nimekusikia ukimfananisha Rais Magufuli wa Tanzania na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe. Nimekusikia ukiwataka wananchi wamuunge mkono Rais Magufuli. Dunia nzima inajua kuwa Rais Mugabe wa Zimbabwe ni dikteta. Anakandamiza upinzani. Anang'ang'ania madaraka kwa namna yoyote ile na kadhalika.

Je, kwa matendo na maneno ya Rais Magufuli na Rais Mugabe, wanafanana? Kwahiyo Rais Magufuli naye ni dikteta? Nani amekwambia Baba Askofu kuwa wananchi hawamuungi mkono Rais Magufuli? Kwanini inatumika nguvu kubwa kuomba wananchi wamuunge mkono Rais wao waliomchagua kwa kumuamini?

Rais atapendwa kwa maneno na matendo yake. Hakuna maajabu mengine!

Bunduki za nini tena jamani katika kujenga hoja!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Mombasa, Kenya)
Mshindi wa uchaguzi anapoomba aungwe mkono
 
Mhasham Askofu Zimbabwe siyo mfano sahihi. Huko wana taabu kweli. Hata hela yao haipo tena. Nafikiri uliongea kifilisofia na natumai atakuelewa.
 
Ukiona ofisi ya rais inaamua kutoa taarifa hii ya askofu kuunga mkono juhudu za JPJM ujue kama ni matusi rais ameyafurahia sana. Na huwezi kutegemea la tofauti toka kwa MTU ambaye anafurahia sana kusifiwa.

Hata hivyo siamini kama huyo askofu anaifahamu Zimbabwe vizuri kwa sababu mtu anayeifahamu Zimbabwe hawezi kuomba Tanzania iwe kama Zimbabwe. Hawezi!
Take it from me, Askofu anaifahamu Zimbabwe vizuri sana. Pili, haya matamshi alivyoyatoa siyo kwa bahati mbaya, ndivyo alivyotaka ujumbe ufike.
 
Dah.... Sasa hii mbona imegeuka juu chini? Au askofu atakuja tena kukanusha?
 
Ni kweli kabisa bila hata Chembe ya unafiki Mh.Lowasa anaipenda Nchi yake na kila kitu kilichomo anatamani kiwe chake yy na mke wake
 
Back
Top Bottom