Askofu Shao amfananisha Rais Magufuli na Robert Mugabe wa Zimbabwe... ataka watanzania tumuunge mkono!

Kama mtanzania sikubali rais wangu kufananishwa na Mugabe. Huyo Askofu amwombe radhi Rais wetu mpendwa na sisi watanzania. Kule kwa Mugabe hakuna demokrasia, huyo Mugabe ana zaidi ya miaka 30 madarakani. Na anataka kurithisha watu wake urais. Jamani, jamani huyo askofu hajui kinachoendelea duniani? Hivi tunavyoongea Zimbabwe si shwari kabisa. Sasa hii Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu ina maana gani kwa taarifa hii?
 
Au kwa vile ni mkatoliki mwenzake? Waendelee tu kumwekea mikono kama kawaida yao.
 
Pengo njoo huku ukanushe, kipenzi chako kimefananishwa na "nduli" wa Zimbabwe.
 
Jana nilikuwa nasikiliza habari za Mugabe BBC nikakumbuka hii thread.

Nikasema, ina maana Magufulinaye kipira kitanuka ama vipi?

Maana hawa watu wa "Mungu" wengine wanaoneshwa "maono".

Tehe tehe tehe.
 
Mugabe kafanya mengi ya kizalendo,tatizo kutojitambua anga'tuke madarakani, mbaya zaidi shetani via mkewe akajiinua sana kwa kiburi na fedhuli.
 
29a49d629149afb1ae065243c4cc7a50.jpg



Kwa kweli tunamwunga Askofu mkono hajakosea, hawa jamaa wanafanana....tusubiri kuona Jenerali Chiwenga wa huku atakavyofanya
 
Askofu huyu kweli ni mwanateolojia, yani anakutukana huku unachekelea.

Si sawa mtu akufananishe na Elton John wewe unaona ujiko kumbe Elton John ni shoga.

Hawa wasomi wa kikatoliki ni hatari sana ndio maana maaskofu wao sijawahi kuona wakipandishwa mahakamani.
 
Askofu Shao na Ikulu itapendeza zaidi wakitoa tena tamko sasa baada ya Mugabe kupinduliwa kwa kumtaka huyu ajiudhuru ,ama wamtafute dikteta mwingine wa kumfananisha nae maana nashangaa hawakumuona raisi mwingine hata Keneth Kaunda hadi wamfananishe na dikteta aliyetaka atawale milele yeye na mkewe hadi wafie Ikulu?!!
 
hawa maaskofu wangu wa Katoliki watakuwa wamerogwa hawa si bure. wanatutia aibu Wakatoliki wote kwa kweli!

Pengo anasifia mambo ya ajabu ajabu, sasa huyu Sh ao naye loh!!
 
Back
Top Bottom