Vipi samaki unapata hapo sokoni Kemondo? Sasa hivi watu watakuwa na utapia mlo wa kuzidi.Mkuu niah, huyu kiongozi wa sasa kajikita kwenye shida za kiuchumi, haya maneno eti tunakoelekea ni kubaya yanasikika humu mijini tena mitandaoni tu, mbona huko Kagera, Mbeya, Shinyanga na Pemba hatusikii maneno kama haya yanayosikika yakisemwa na wanaharakati?.
Wanaosema demokrasia imebanwa ni watu wa mijini wenye simu za viganjani na wenye akaunti za twitter, facebook na wenye uwezo wa kununua magazeti kama newsweek na mengine, wale wa vijijini ambao ndio wengi akili zao zipo kwenye utatuzi wa shida zao.
Wanaharakati bado wanayo ile superiority complex, yaani mawazo yao ndio yenye kuwakilisha mustakabili wa wengi, kiburi ambacho jaji Warioba aliwahi kukiongelea, wanadhani kuwa wale watu wa vijijini hawana uwezo wa kiakili wala hawana hekima ya kutambua lipi zuri na lipi baya.