Askofu Niwemugizi: Jamii imejaa uasi

johnmashilatu

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
718
703
Askofu wa jimbo katoliki la Rulenge Ngara, Mhashamu Severine Niwemugizi amesema jamii imejaa uasi kutokana na kuongezeka kwa maovu yanayotekelezwa na baadh ya wanajamii.

Akiongea katika ibada ya Upadrisho wa Padre Baraka Rusesa, inayofanyika leo katika kanisa la Mtakatifu Fransinsko wa Asiz jimbo la Rulenge Ngara, Mhashamu Niwemugizi amesema, viongozi wa dini wanapaswa kukemea bila kuchoka hata kama kwa kufanya hivyo watakutana na changamoto hasa kutoka kwa wenye mamlaka.

"Kuna Ukatili na vitendo vya uasi katika jamii yetu, hivi sasa tumekuwa tukisikia vitendo vya maasi ambapo mke au mume humuua mwenza wake kwa silaha mbalimbali kama vile risasi na baadaye naye kukimbia na kwenda kujitoa uhai... huu ni uasi unaoendelea katika jamii" alisema Askofu Niwemugizi.

Amesema taarifa zinazosikika maeneo mbalimbali, zinaonyesha kuwawepokwa vitendo vingi vya uasi, hivyo kiongozi wa kiroho anapaswa kutambua kuwa anafanya kazi katika maeneo ya aina gani ili atimize kazi anayotakiwa kuitekeleza.

Katika Ibada hiyo inayotangazwa moja kwa moja na na Radio wizera, amesema binafsi amekuwa akikema maovu na baadhi ya watu wakimkemea lakini hachoki kwani amekuwa akikemea, anakemewa naye anaendelea kukemea kwa kuwa jamii inapaswa kutekeleza kazi yaliyo mema.

Mhashamu Niwemugizi amemtahadharisha kiongozi huyo mpya wa kiroho kuwa katika kutekeleza kazi hiyo atarushiwa madongo ya aina mbalimbali... umetumwa kufanya kazi ya mungu hakua sababu ya kuongopa na pia hapaswi kutekwa na malimwengu.
 
Back
Top Bottom