Askofu Mokiwa busara ya hili ni kujitoa boriti

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Hivi karibuni vyombo vya habari viliripoti mgogoro katika kanisa moja la kianglikani lililopo Ukonga Dar es salaam. Mgogoro huo unatokana na waumini kumkataa kiongozi wa kanisa. Ktk jitihada za kujaribu kutafuta muafaka, ilipelekea askofu mkuu wa Anglikan Dr. Valentiono Mokiwa kulifunga kanisa hilo na kuomba ulinzi wa dola kuwazuia waumini kusilitumie.Wakati haya yanafanyika, pengine ifike wakati sasa wa viongozi wa makanisa yetu (hasa yanayoruhusu demokrasia kwa waumini) kuwa tayari kuondoa fikra mgando za kuwaamuria mambo waumini wao hata pale ambapo wanahitaji kufanya maamuzi yenye kujenga. Umetokea mtindo kwa baadhi ya viongozi wa makanisa kuendesha huduma kwa staili ya ubabe na uswahiba.Wapo makasisi/wachungaji ambao wamepungukiwa kabisa maadili lakini wameachwa kwenye huduma kwa kuwa ni maswahiba wa viongozi wakuu wa kanisa. Ukifuatilia kwa makini sana hivi sasa makanisa mengi yanaendeshwa kwa nguvu za waumini kuanzia ujenzi mpaka kuihudumua familia ya mchungaji, lakini chakusikitisha, pale mchungaji husika akiwa mtovu wa nidhamu,waumini wanaonekana kana kwamba hawana mamlaka juu yake.

Kamezuka kamtindo hasa ktk makanisa ya kiprotestanti kwa viongozi wake kupenda makuu, wanataka waishi maisha ghali kwa nguvu ya sadaka na michango ya waumini. Utaratibu huu wa maisha umepelekea makanisa mengi kuongozwa na wazee wa kanisa wenye vipato na ambao hata kasisi hawezi kuwa kemea wanapopotoka, ndio hao wanaosimika hata viongozi wa juu wa kanisa wenye mwelekeo wa kukosa maadili. Hadhi na heshima ya makanisa inapotea, unakuta kasisi anataka kuishi maisha ya bustani ya Eden kwa kuwakamua waumini wake, makasisi hasa vijana wamekuwa mafisadi kiaina kupitia mifuko ya waumini kiasi kwamba wengi hawataki hata kuamishwa toka mitaa au makanisa yenye neema(yenye waumini wenye mioyo ya kujitoa kuchangia maendeleo ya kanisa). Wengine wamekuwa ni mzigo kwa waumini ka kupenda mambo makuu tofauti na uwezo wao na taka taaluma wanayoitumikia (utumishi wa Mungu). Wanapozidi kuyabana makanisa yatoe, bado unakuwa hakuna maendeleo yoyote zaidi ya kuwa neemesha wacache, na hakuna kalipio toka uongozi wa juu kuwataka wachungaji waishi maisha ya kiroho zaidi na sio kupenda makuu kama vile magari ya kifahari, simu kali, posho nyingi nyingi nk.

Uongozi wa kanisa la anglikana nchini uangalie matatatizo ya kule Ukonga na kwngineko kama changamoto na sio kuwazuia waumini wasitumie mahali pa kuabudu kwa kile kinachodaiwa ni vurugu. Zipo kero ni nyingi huko makanisani lakini zimefumbiwa macho.

Pengine kama waumini walijenga kanisa na wanamlipa mishahara mchungaji, ikitokea mchungaji anawavuruga, wao hawaoni kwa nini wasiwe na
mamlaka ya kumwondoa!

Wapinga askofu Dk Mokiwa kulifunga kanisa Ukonga Send to a friendSunday, 15 May 2011 21:11 0diggsdigg

Minael Msuya
MGOGORO wa Kanisa la Anglikana, Mtaa wa Mtakatifu Filipo, lililopo Ukonga Mazizini Dar es Salaam, umeshika kasi baada ya uongozi wa kanisa hilo kuibuka ukipinga uamuzi ya Askofu wake Mkuu, Dk Valentino Mokiwa kulifunga na kueleza kuwa uamuzi huo sio wa kiroho na haukuwatendea haki.

Juzi, Dk Mokiwa alitangaza kulifunga kanisa hilo kutokana na kuwa na mgogoro wa kiutawala kwa muda mrefu na kwamba Dayosisi ya Dar es Salaam imefanya vikao vingi ili kuumaliza utata uliopo bila mafanikio.


Lakini jana, Mwinjilisti wa Kanisa hilo la mtaa wa Mtakatifu Filipo Mazizini, Ezra Sangaye aliibuka na kusema kuwa uwamuzi ya Askofu Mkuu, Mokiwa siyo wa kiroho na ameingilia uhuru wa kuabudu kwa kuwa hajawahi kufika katika kanisa hilo hata siku moja tangu kuanza kwa mgogoro huo.

Akizungumza na gazeti hili Mwinjilisti Sangaye, alisema Askofu Mokiwa alifanya uwaamuzi ambao kimsingi haujazingatia imani na kwamba mgogoro huo ungeweza kumalizika.

"Taarifa za kufungwa kwa kanisa hazijanifurahisha mimi kama mtumishi wa Mungu, bado jambo hili lingeweza kuzungumzwa likamalizika," alisema Sangaye na kuongeza:

"Mokiwa hakututendea haki kwa kuwa hajawahi kufika katika kanisa hilo hata mara moja kipindi chote cha mgogoro ingawa yeye ni kiongozi wa kiroho. Hivyo akiwa kiongozi mkuu wa Anglikana hajatutendea haki amesikiliza maelezo ya upande mmoja,"alisema.

Kwa upande wake Charles Chilimo muumini wa kanisa hili alisema, Mokiwa angepaswa kufika katika kanisa hilo ili aweze kusikiliza maelezo ya pande zote na sio kujichukulia uwaamuzi.

"Hili ni suala la kiroho, alichokifanya Askofu sio sahihi hasa ukizingatia yeye ni tabaka la juu na sisi ni tabaka la chini, alipaswa kufika kwenye eneo husika ili apate maelezo ya kina," alisema Chilimo.

Inspekta wa Polisi Leonard Sesoma aliyekuwa akilinda eneo la kanisa hilo baada ya kufungwa aliliambia gazeti hili jana kuwa wapo waumini wa kanisa hilo waliofika pale siku ya jana kwa ajili ya ibada ambapo walikuta kanisa limefungwa.

"Hakuna vurugu yoyote ila saa 12.30 asubuhi wapo waumini waliofika hapa wakidai wanataka kufanya ibada, lakini tulipowaeleza kuwa kanisa limefungwa walielewa na kuondoka.

Katika maelezo yake juzi, Askofu Mkuu Dk Mokiwa alisema, "Tumeamua kufunga Mtaa wa Mtakatifu Filipo Mazizini tangu leo, kutokana na migogoro ya kiutawala na viongozi wa Kanisa la Anglikana Tanzania ambao wako nje ya mamlaka ya kijiografia na kiutawala," alisema Dk Mokiwa.

Dk Mokiwa alifafanua kuwa vikao mbalimbali vilifanyika pamoja na kujaribu kutafuta njia za kurejeza utulivu, lakini bado kikundi cha watu wachache kimeendelea na uchochezi akieleza kuwa kikundi hicho kina lengo la kutekeleza agenda zake za siri.

http://www.mwananchi.co.tz/news/4-h...askofu-dk-mokiwa-kulifunga-kanisa-ukonga.html
Mzozo wa Anglikana Monday, 16 May 2011 09:59 Wachungaji wampinga Askofu Mkuu
*Polisi walinda kanisa kwa mabomu
Na Waandishi Wetu, jijini

POLISI jijini Dar es Salaam wamelazimika kutumia silaha na mabomu ya kutoa machozi ili kuimarishaulinzi katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Filipo Mazinini, baada ya Askofu wa kanisa hilo, Valentino Mokiwa, kutangaza
kulifunga.

Mbali ya uamuzi wa askofu huyo, lakini baadhi ya wachungaji wa kanisa hilo hawakubaliani na uamuzi huo kwa madai kuwa, hawapo chini ya askofu, bali wapo chini ya jimbo.

Dar Leo, jana lilishuhudia kundi la askari Polisi wakiwa na silaha, wakilinda kanisa hilo ambalo lilikuwa limefungwa kwa makufuli mawili.

Baadhi ya waumini jana asubuhi walifika kwa ajili ya kuendelea na ibada, lakini walikutana na polisi hao waliokuwa wametanda kila kona ya kanisa hilo.

Waumini hao ambao hawakufahamu kuwa kanisa hilo limefungwa, walioneakana kushikwa na butwaa huku wengine wakitafuta njia nyingine ya kuweza kuabudu siku hiyo.

Hata hivyo, licha ya askofu huyo kuepuka kutokea kwa hatari katika kanisa hilo kutokana na kuwepo kwa mgogoro kati ya waumini na mchungaji wa kanisa hilo, John Makanyaga, kumezua utata kwa baadhi wachungaji na waumini kwa kupinga uamuzi huo.

Wamedai kuwa, hawakubaliani na uamuzi wa askofu huyo kwani huo si uamuzi wa waumini wote, bali ni uamuzi wa viongozi wachache.

Akizungumza na gazeti hili leo asubuhi, Mchungaji wa Kanisa la Tungi Kigamboni, Obed Ntigogozwa, amesema kuwa, ni kweli mwezi mmoja sasa kanisa hilo limekuwa kwenye mgogoro ambao ulitakiwa viongozi wa ngazi za juu kukaa chini na kuamua ni kitu gani kifanyike ili kuondokana na hali hiyo.

Amesema kuwa, uamuzi wa askofu Mokiwa kulifunga kanisa hilo, siyo sahihi kwani kanisa hilo lipo chini ya jimbo la si askofu Mokiwa.

"Hatukubaliani na uamuzi huo, sisi kama kanisa la Tungi Kigamboni na Ukonga wenye mapokeo kama yetu, tunapinga kufungwa kwani waumini wataweza kupata shida na kusababisha kuhama dhehebu," alisema mchungaji huyo.

Amesema kuwa, kinachoonekana hapo ni askofu Mokiwa kukubaliana na vitendo vilivyokuwa vikifanywa na mchungaji huyo ambaye waumini wake wamefikia hatua ya kumkataa.

Hata hivyo, baadhi ya waumini wa kanisa hilo waliozungumza na Dar Leo, wamesema kuwa, hawakubaliani na uamuzi huo kwani inaonyesha dhahiri kuwa, askofu huyo amewaingilia uhuru wao.

"Binafsi na wengine sikubaliani na uamuzi huo kwani kiwanja hiki tumekinunua kwa michango na tumelijenga aknisa kwa nguvu zetu," alidai muumini mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

Mwishoni mwa wiki, Askofu Mokiwa alitangaza kufungwa kwa kanisa hilo kwa kuhofia kutokea kwa machafuko, kama umwagikaji wa damu baada ya kufikia uamuzi kwenye kikao na baadhi ya viongozi wa kanisa hilo kwa kushirikiana na polisi.

Askofu Mokiwa amesema kuwa, katika uchunguzi wamebaini kuwa, kuna kikundi cha watu 15, ndicho chenye kusababisha fujo kwa kushirikiana na kiongozi mmoja.

"Amani itakaporejea tena katika kanisa hilo, litafunguliwa na tumefanya hivyo kwa kuepuka kutokea kwa umwagikaji wa damu, " amesema askofu Mokiwa.



 
hivi hili ndo lile kanisa la mashogaaa? hakika washapaishwa mbinguni
na mwenzao camping jana /kila siku migogoro wanapata wapi muda
wa kuzungumza na muumba wao jamaniii? au ni mafisadi nini
 
Back
Top Bottom