Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 780
- 1,831
Askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa, Mhashamu Romanus Mihali, amewataka Wakristo, hususan waumini wa Kanisa Katoliki, kutimiza wajibu wao wa kusimamia haki, amani na uadilifu, hasa katika masuala ya uchaguzi, wakisisitiza kuwa kutotenda haki ni dhambi kubwa.
Askofu Mihali alitoa wito huo wakati wa homilia ya Misa ya Sikukuu ya Krismasi (Noeli) iliyoadhimishwa katika Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, Kihesa, jimboni Iringa.
Akizungumza na waumini, Askofu Mihali alisema Mkristo Mkatoliki amepewa dhamana ya kusimamia taratibu za uchaguzi kwa haki na kwa kuzingatia dhamiri safi, bila kuyumbishwa na shinikizo au maelekezo yanayokiuka misingi ya haki.
“Wewe Mkristo Mkatoliki umepewa wajibu wa kusimamia uchaguzi. Je, unasimamia uchaguzi vizuri? Ukielekezwa kufanya kinyume cha haki, unapaswa kusimama imara kama Mkristo na kusema hili si la haki, sitafanya,” alisema Askofu Mihali.
Aliongeza kuwa Mkristo anayeshiriki au kunyamazia vitendo vya udhalilishaji wa haki anapaswa kutambua kuwa anafanya dhambi, akisisitiza kuwa kuchezea dhamiri za watu bila kutubu ni kosa kubwa mbele ya Mungu.
Katika ujumbe wake wa Krismasi, Askofu Mihali aliwakumbusha waumini kuwa maadhimisho ya Noeli yanapaswa kwenda sambamba na kuishi maisha ya haki, unyenyekevu na amani, kama kielelezo cha kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
Chanzo na SAUTDIGITAL