Automata
JF-Expert Member
- Mar 3, 2015
- 3,347
- 4,614
Baba Askofu Mhashamu Beatus Kinyaiya, O.F.M. Cap.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma, Mhashamu Beatus Kinyaiya, amewataka Wakatoliki kuhakikisha wanadumu katika sala na kwenda Kanisani na siyo kusubiri waletwe Kanisani wakiwa ndani ya jeneza.
Askofu Mkuu Kinyaiya aliyasema hayo hivi karibuni kwenye Ibada ya Misa Takatifu ya Sakramenti ya Kipaimara, iliyofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Peter Clavery, Mbezi Louis Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam.
“Mjitahidi kwenda Kanisani kusali na ninyi waimarishwa yale mliokubaliana na Mwenyezi Mungu, mkayafanyie kazi siku zote za maisha yenu”, alisema Askofu Kinyaiya na kuongezea, “Hii isiwe ndiyo mwisho wenu wa kufika Kanisani baada ya kupokea Sakramenti ya Kipaimara…bali endeleeni kuja Kanisani kwa Ibada na Sakramenti mbalimbali, msisubiri mletwe Kanisani mkiwa ndani ya jeneza”, mwisho wa kunukuu.
Askofu Kinyaiya alisema kuwa vijana hao wanatakiwa kutambua kuwa wao kwa sasa ni mabalozi katika familia zao, kwa kuwaamsha wazazi na walezi wao kwenda Kanisani na kushiriki Jumuiya ili kuondoa hali ya ubaya ndani ya familia zao.
Source: Tumaini Letu