BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 422
- 1,049
Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Askofu Flavian Kasala amewataka Watanzania kusimamia ukweli na haki katika kumuenzi Rais wa awamu ya tano, hayati John Magufuli.
Askofu Kasala ametoa rai hiyo leo Alhamisi Machi 17, 2022 kwenye ibada ya misa ya kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha hayati John Magufuli inayofanyika katika uwanja wa Magufuli Chato.
Amesema Hayati Magufuli alisimamia ukweli na kile anachokiamini, hivyo kuwataka wananchi na viongozi kushuhudia ukweli huo katika maisha yao.
“Tukisimamia ukweli na haki, marehemu wetu wanazo dhawabu walizoondoka nazo, tuko tayari kuyachukua hayo kuwa kama dira ya maisha yetu?” amesema na kuongeza:
“Njaa ya haki ni pale katika ubinadamu wako unaposema siwezi kushuhudia kuona mtu akiwa anaonewa, ananyanyaswa na kudhulumiwa.
“Maudhi kwa ajili ya haki yanakuja pale tu mmoja anaposimamia haki bila kijibakiza na kusimamia haki ni kujitoa sadaka lakini bora niudhiwe lakini haki itendeke,” amesema Askofu Kasala.
Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021 kwa maradhi ya moyo katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu, mwili wake ulizikwa Ijumaa Machi 26, 2021 katika kijiji cha Mlimani wilayani Chato Mkoa wa Geita katika makaburi ya familia.
Chanzo: Mwananchi