Askofu Kakobe: Rais Magufuli ni mchapakazi, watu wa namna hii ni wachache sana, sisi tumepata neema

Kwani Kakobe nae anachapa kazi au anapokea mapato kwa kuwalaghai binadam?
 
Hivi inaruhusiwa kumuombea toba MTU mwingine kwa niaba ?? Nadhani Kakobe angejiongeza tu atubu!! Kwa niaba ili sasa mapambio yanoge kwa chorus
 
kuna haja ya kuweka EFD kwenye makanisa ya kiroho, tumeshuhudia wachungaji wao wengi ni matajiri kupindukia kwa pesa za waumini wao.
Akina kakobe, gwajima na wengineo ni wezi sana.
 
Nina hela/mali nyingi kuliko serikali hii-Kakobe

Baada ya kupelekewa TRA kumkagua, kauli ika badilika ikawa hii:

Nilimaanisha nina pesa/mali nyingi kuliko serikali na akiba yangu imehafadhiwa kwa baba mbinguni-Kakobe
U-Turn matata
 
Askofu Kakobe amesema anabarikiwa sana na kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu na kwamba Rais Magufuli ni mchapa kazi kweli kweli.

Kakobe amesema watu wenye hulka ya kufanya kazi kwa uzalendo uliotukuka aina ya Dr Magufuli ni wachache sana barani Afrika na sisi kama taifa hii ni neema.

Askofu Kakobe amewataka Watanzania kujijengea tabia ya kufanya kazi kwani katika maisha halisi hakuna njia ya mkato wala mteremko.

Mwisho, Kakobe amesema huko duniani kwenye maendeleo watu hufanya kazi kweli kweli na hata likizo zao ni siku 15 tu kwa mwaka na wengi hawachukui likizo mfano Japan, Marekani, Singapore na Korea kusini.

Chanzo: TBC

Maendeleo hayana vyama!
naomba mumkumbushe mtumishi Kakobe yule afisa wa TRA aliekuwa mkoa wa kodi Kinondoni (Mwenge Office) aliekua na cheo cha Assistant Regional Manager - Audit, alipotoa ripoti ya ukaguzi wa kanisa la Full Gospel kuwa halikua na shida na wala hakuna kodi ilikwepwa, alivuliwa uo Umeneja na kuhamishiwa Kigoma

Hivi Kakobe anajua kweli kama kuna watu wamepoteza ugali na kuondolewa mjini sababu ya kusema kweli?
 
Ukinijibu swali ili nami naungana nawe ...Hivi Rais wa nchi ndiye ananunua ndege,kujenga SGR n.k au pesa za walipa kodi ndiyo zinafanya hivyo?
Mbona umeshajijibu wewe mwenyewe kwamba ndege zinanunuliwa na Rais kadhalika SGR inajengwa na Rais kwa kutumia fedha za kodi.

Uliza swali usilete majawabu!
 
Askofu Kakobe amesema anabarikiwa sana na kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu na kwamba Rais Magufuli ni mchapa kazi kweli kweli.

Kakobe amesema watu wenye hulka ya kufanya kazi kwa uzalendo uliotukuka aina ya Dr Magufuli ni wachache sana barani Afrika na sisi kama taifa hii ni neema.

Askofu Kakobe amewataka Watanzania kujijengea tabia ya kufanya kazi kwani katika maisha halisi hakuna njia ya mkato wala mteremko.

Mwisho, Kakobe amesema huko duniani kwenye maendeleo watu hufanya kazi kweli kweli na hata likizo zao ni siku 15 tu kwa mwaka na wengi hawachukui likizo mfano Japan, Marekani, Singapore na Korea kusini.

Chanzo: TBC

Maendeleo hayana vyama!
Ila Kakobe naomba ufute na ile kauli yako dhidi ya Rais wetu ,naamini unaikumbuka
 
@"johnthebaptist,

Kila MTU anapenda anataka afanye kazi hakuna alalaye kusubiria kufa na njaa.

Shida mazingira yana vikwazo vingi ayachochei watu kufanya kazi kama walivo nchi zilizoendelea, wao wana sera nzuri ziwafanyazo watu wao kufanya kazi.
mishahara inalipwa kazi kwa saa unajua utapata $ ngapi
 
Kama vile nyie munavyomuita membe na wenzake ni wasaliti
Kwanza mkuu naomba unielewe Mimi Sina kadi ya chama chochote kile na Wala Siyo Mwanachama wa chama Cha siasa chochote nchini Bali Mimi Ni mpiga Kura TU Ambaye huwa natumia akili yangu kuchagua kiongozi ninayemuona kwangu Ni sahihi bila kujali chama chake..

Ila pia kwa vile Mimi Ni mpiga Kura huwa Sina budi kufuatilia mienendo ya kila chama na viongozi wake ili kujilidhisha kabla ya kufanya uchaguzi.. na hata bandiko nililoliweka nimetumia facts zaidi Hadi kuandika vile Ila kuhusu Mambo ya Membe na watu wake nitakujibu kwa Mimi nilivyofuatilia mienendo ya Mr Membe Kama ifuatavyo;
Membe Ni mtu Ambaye anauchu Sana na kiti Cha urais na anapoona huko aliko Kama Hamna dalili za kupata anachokipata Anaamua kuwa against na serikali hivyo Basi mpaka sasahivi Nina uwezo wa kusema Membe Ni msaliti kwa asilimia fulani hivi.
 
kuna haja ya kuweka EFD kwenye makanisa ya kiroho, tumeshuhudia wachungaji wao wengi ni matajiri kupindukia kwa pesa za waumini wao.
Akina kakobe, gwajima na wengineo ni wezi sana.

Makanisa, misikitini, NGO's sehemu zote za kiroho wawe wazi kuhusu mapato, matumizi, mipango nk. Waweke hivi vitu hadharani, angalau kwa waumini wao.

Hizi account zipitiwe na competent independent Accountant. Of course wengi ni wazuri lakini wahuni pia ni wengi wamejificha huko.

Waweke profit and loss account, (mapato na matumizi) balance sheet, pia kazi gani wamefanya kwa mwaka uliopita na mwaka huu/ ujao watafanya nini, mipango yao?

Naamini Yesu angefanya hivyo ukiangalia maisha yake of course alikuwa homeless, nguo mbili tatu na kandambili.

Kila kitu alikuwa anapeleka kusaidia wengine wenye matatizo. (The least among us)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom