Askofu Kakobe Asipuuzwe: Ni kama David Koresh na Camp Davidians!

QUOTE=Ndege ya Uchumi;739512]I'm asking a technical question!

Umeme wa Msongo Mkubwa unapaswa kupita wapi kufika Majumbani kwetu?[/QUOTE]
Umeme wa msongo mkubwa sio unaoingia majumbani, huu wa msongo huenda kwenda kituo cha kupoozea umeme kama pale Ubungo disribution station hapo hupoozwa na kupelekwa kwenye trasfoma pozo ambayo ndio from there, huingiza umeme majumbani.

Huu umeme wa msongo mkubwa una madhara ya magnetic interfiarance kwenye electro magnetic waves zozote zinazopita karibu, kama wenye TV ya Analog, ikikaa karibu na simu ya mkononi, simu ikiita utasikia interfiarace ya sauti.

Hoja ya Kakobe, amedhamiria kufungua kituo cha redio na televisheni hapo kanisani kwake hivi karibuni, hivyo anahofia interfiarance ya muingiliano na mitambo yake.

Wataalamu wameshamthibitishia kuwa hakuna madhara ila Mzee sio tuu ni mbishi, bali pia ni king'ang'anizi. Ni hapa ndipo lilipokuja angalizo langu, jee huku ni kumtimikia Mungu?. Anatumia human shield, hivi ndio mapenzi ya Bwana?.
 
Electrifying: Is living under power lines harmful to your health?
March 23, 2007

Dear Cecil:

I've always heard that living under or near power lines was harmful to your health. The other day after driving by a community located next to a massive power station with so many cables running out of it that you could actually hear the hum of electricity over the traffic, I got to wondering: is there any truth to this common belief?

— Carlos G., via e-mail

Two ways you can look at this. To judge solely from the amount of research, we're facing the gravest threat to humanity since nuclear war. Over the past 30 years, scientists have published close to 25,000 articles on the health effects of non-ionizing radiation (the kind emitted by power lines). We've had population, occupational, and laboratory studies scrutinizing everything from high-voltage transmission lines to electric blankets. When you look at the results, though, you have to wonder why the fuss. All the investigations to date have yet to produce any clear indication that low-level electromagnetic fields from power lines are a health hazard to the general public. I won't say there's no danger whatsoever, but the perception bears no relation to the threat.

Some background. Magnets and moving electric currents radiate energy into space, generating the invisible aura we call an electromagnetic field (EMF). The stronger the magnet or current, the more pronounced the field. These fields penetrate solid objects with relative ease and produce readily detectable effects, one of the better known of which is the broadcasting industry. Long ago some genius realized: Cheezit, if music moguls can turn teenage minds to mush using nine-volt transistor radios, what deviltry might we be unwittingly visiting on ourselves with a 128,000-volt high-tension line? Thus the busy investigative agenda adverted to above.

The first high-profile study to assert a link between power lines and cancer was a 1979 plotting of childhood leukemia rates against residential distance from power lines in Denver - the closer the cables, the higher the incidence of leukemia. This study didn't actually measure EMF strength in the homes, nor did it control for possible confounding factors such as income levels. (Possibly housing near power lines is occupied predominantly by poor people, whose health is worse overall.) But it did prompt lots of other research, most of which uncovered nothing.

I'll say this, though. Evidence for a link between EMF exposure and childhood leukemia turns up just often enough that it can't be entirely dismissed. Although the vast majority of studies in the U.S., Canada, and the UK have found little connection between leukemia and proximity to power lines, a large 2005 study received a lot of press coverage for showing a modest, if baffling, correlation. This was the so-called Draper study, an examination of most childhood leukemia cases among kids born in Britain between 1962 and 1995. Draper and his colleagues found a clear relationship between the disease and residential distance from high-voltage power lines, even after adjusting for poverty levels. However, the study showed a leukemia increase even at distances where the electromagnetic energy radiated from power lines was much less than that generated by ordinary household wiring and appliances. The researchers conceded, "We have no satisfactory explanation for our results in terms of causation by magnetic fields, and the findings are not supported by convincing laboratory data or any accepted biological mechanism."

Some contend the increase in leukemia is related to that humming you hear from electrical lines and equipment. High-voltage power lines can ionize the air around them, an effect called corona discharge. In addition to buzzing, these discharges create pollutants such as ozone and nitrogen oxides and ionize other airborne pollutants, making them more likely to stick in your lungs when inhaled. A problem with this theory is that ozone and nitrogen oxides aren't especially carcinogenic, and no link has been demonstrated between them and leukemia.

Another conjecture is that some people have "electromagnetic hypersensitivity," or EHS. People claiming to suffer from EHS have a strange assortment of symptoms, including skin disorders, fatigue, difficulty concentrating, heart palpitations, and even digestive problems. However, according to the World Health Organization, EHS doesn't stand up to double-blind testing and could be attributable to anything from poor ergonomics to stress to psychiatric conditions.

Despite the lack of evidence linking power lines to health problems, consumer advocacy groups still urge limits on exposure, and research plods along. Even if a risk is established, it may not be big enough to warrant action. As the British Medical Journal commented following the Draper study, the net negative health effect of power lines in the UK could be five cases of leukemia annually, compared to 32,000 children injured and 200 killed each year in car accidents. Most will surely concede electricity's benefits outweigh a few additional cancer cases, provided they're not one.

— Cecil Adams
 
hao watu hukaa hapo mchana na usiku,kina mama kwa kina baba,kwa vijana.swali ni je,wanafanya kazi zao saa ngapi?na hao kina mama wanakaa na waume zao saa ngapi?ndio maana watu husema wafuasi wa kakobe ni masikini,sababu mtu analala na kushinda kanisani anafanya kazi saa ngapi?na kamwe hukuti wale wenye magari wanakesha hapo na kushinda hapo,ni wale pangu pakavu tia mchuzi kama mimi,ukimwona na kiatu soli imekaa upande,wanatia huruma kwa kweli,tena wengine ni vibibi!!!!!

hatumsemi vibaya,ila ni kweli serikali inabidi iingilie katui kama ilivyofanya kwa wale waumini wa kwenda ulaya bila passport kwa IMANI.kama ni haki yao wanafuatilia kwanini serikali isiwapatie ili kuokoa hawa wananchi na mateso???pale nje pana baridi na mbu wakali!!!!!!!
 
Rudi mwanzo na msome Pasco vizuri kabla ya kumjibu. Usiweke mbele hisia zako katika hoja.

Halafu chakaza, wengi wanaojibu hawajasoma vizuri maelezo ya Pasco. Nashindwa kuelewa kama kweli Pasco alimhoji Kakobe kwa nini kakobe asingekuwa wazi hata kama Pasco ameonyesha hali ya uoga kidogo? Si angemueleza tu sababu za yeye kufanya hivyo ili kuondoa dukuduku moyoni mwake?
 
Mkuu watu ambao wameshakutana na "power za Kakobe" si tu ma senior managers na madirector bali hata mawaziri na viongozi wa ngazi mbali mbali za kitaifa na kimataifa. Ukitaka kufahamu tembelea mojawapo ya ibada pale kanisani na uwaone washiriki ndipo utakapotambua ya kuwa Askofu huyu ana "nguvu" kama asemavyo Pasco

kinachokutisha ni vyeo vikubwa vya watu au elimu yao? remember a person can be educated and still retains some of their conceived ideas and beliefs even if suchideas and beliefs are wrong provided they dont devote to seeking the truth.The educated people might not neccessarily have the relevant knowledge to be models to other people.Remember this "Nakushukuru Baba kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na kuwafunulia watoto wadogo." In real sense sio watoto bali wanyenyekevu wa moyo.
 
Baada ya leo Baba Askofu kuandika waraka wa Mungu kwa JK, hapa nimepita kufanya rejea!.
Pasco
 
Kiufupi hakuna waziri au katibu mkuu wa wizara aliekua analala nje pale. Hilo ndo nililokua nasisitiza. Kusali sawa ila sio kukesha wakilinda kanisa
 
Baada ya leo Baba Askofu kuandika waraka wa Mungu kwa JK, hapa nimepita kufanya rejea!.
Pasco

Pasco, nakubaliana na mawazo yako kwenye rejea yako. Ila mkuu siku hiyo saa yako nayo ilikuwa inatetemeka au....? Maana ulipita saa 8.39 usiku lakini uka-post uzi wako saa 7.40 usiku huo huo!
 
Pasco, nakubaliana na mawazo yako kwenye rejea yako. Ila mkuu siku hiyo saa yako nayo ilikuwa inatetemeka au....? Maana ulipita saa 8.39 usiku lakini uka-post uzi wako saa 7.40 usiku huo huo!
Du!, asante mkuu, nilikuwa sijanote hii kitu!, usikute!.
Kwenye ule uzi wa waraka kwa JK kuna mtu amedai kuwa umeme emegoma kupita kwenye hizo nguzo mbili mbele ya kanisa la FGBF!. Sijathibitisha!. Akiwa ni kweli, itanibidi nitubu!.
Pasco
 
Saa hizi ni Saa 8:39 za usiku!, yaani usiku wa manane, nimepita nje ya kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, la Askofu Zakaria Kakobe, nikashuhudia mamia ya waumini wake wamekaa kwenye viti na meza nje ya kanisa hilo huku limepambwa na disco lights zinazobadilika badilika rangi, kwa mgeni aweza dhania ni night club fulani.

Nimeshauri asipuuzwe kwa sabubu mimi ni mmoja ambaye ninatoa ushuhuda jamaa ana nguvu, yaani he has powers! Niliwahi fanya nae mahojiano miaka ya nyuma, nikamuuliza hiyo daraja ya Uaskofu alipewa na nani?. Alijibu na Mungu mwenyewe!. Nikauliza kuhusu tuhuma mbalimbali zinatupwa kwake na watu wa mataifa, zikiwepo yeye kuwa tajiri wakati waumini wake wako kwenye umasikini uliotopea, kuhusu Mkewe kuwa ndio Mweka hazina, kuhusu kama hayupo inawekwa kanda kuhubiri.

Na swali la mwisho nilimuuliza kuhusu ukweli kuwa waumini wake wanavuliwa dhahabu na anaziteketeza kwa moto, nikamuomba angalau anionyeshe lilipo hilo tanuru nishuhudie smelted gold deposits kwa macho yangu mwenyewe.

Askofu alinyamaza, akaniangalia machoni kwa kunikazia macho kama anahasira fulani, nami nikajisikia baridi ya ghafla nikataka kuanza kutetemeka na kusikia kizunguzungu ile staili ambayo hatimaye watu huanguka chini. Nikajishika imara kwenye kiti, nikwamwambia Askofu, nimeyaondoa maswali yangu yote, hana haja ya kuyajibu tena!. End of interview.

Huu ni uthibitisho tosha kuwa Askofu Zakaria Kakobe ananguvu fulani, hivyo sio wa kupuuzwa.

Kitendo cha kuwaona waumini wake kwa mamia, wanalala macho usiku kucha kwa kumsikiliza Askofu wao akiwaamuru kuhakikisha wanaipinga serikali in the name of God, ninaamini hao walala nje, wanalala macho hapo nje kwa imani 100 kwa 100 kuwa huko nako ni kumtumikia Mungu Baba na sio kumtumikia binadamu mwenye jina la Askofu.

Kwa lugha nyingine, Nguvu za Askofu Kakobe zimewahypnotize waumini wake kwa kiwango cha juu, kiasi kwamba, chochote atakachowaambia wafanye, watafanya, ndivyo ilivyokuwa kwa David Koresh na wafuasi wake wa Camp Davidians na Askofu Kibwetere na wafuasi wake ambao mwisho wao wote waliishia kuteketezwa kwa moto na kujilipua kwa mabomu kwa ahadi ya safari ya mbinguni kwenye uzima wa milele, imewadia!.

Kama kuna yoyote ambaye ni muumini ama aliwahi kuwa muumini akatusaidia sisi akina Tomaso, kwa kutupa ushuhuda wa msingi wa nguvu za Baba Askofu Zakaria Kakobe ili nasi tumuaminiye na tumfuate, vinginevyo huyu ni mtu mwenye nguvu za ajabu na siyo wa kupuuzwa.

NB. Mode, hii siyo ya dini na imani, ni ya politics of religion.
PASCO, yaani yaani kwa jinsi ulivyo short-minded, hadi nakuonea huruma. sitaki kuamini kama wewe ni mwandishi wa habari (umesema ulishawahi kumhoji), unaonyesha uko biased kupita kiasi upande mmoja, na you have very little information about kakobe and his church na wapentecoste wote na imani yao. hivi mtu kama wewe ukileta habari kwenye gazeti au kwenye media yeyote kusambazia raia, si hatari jamani, yaani wewe ni mtupu kichwani na sijui ulisoma hadi kiwango gani na ulisomea nini?
 
Mkuu Hute, pole!, unaonekana umeumia!.
Upande wa elimu nilibahatika kusoma mpaka mwisho wa ile elimu ya lazima kwa Tanzania bara!, ni darasa la saba!, hivyo na mimi niliishia Darasa la saba tena enzi hizo tukifundishwa na walimu wa UPE!.

Sifa kubwa ya elimu ya darasa la saba ni kujua kusoma na kuandika!. Hivyo najua kusoma na kuandika ndio maana umeweza kunisoma!. Kufuatia kupenda kwangu kuandika ndika nikawa mwandishi wa habari, kwa sababu sifa pekee ya kuwa mwandishi wa habari kwa Tanzania, ni kujua kusoma na kuandika!.

Kuandika ni one thing, na content ya unachokiandika ni another thing!. Hivyo mimi kama Mtanzania, nina haki ya kusema au kuandika chochote, na wewe kama Mtanzania pia unazo haki hizo, ikiwemo kukosoa chochote mwingine yoyote aliyekiandika!. Unapomkosoa mwandishi kuwa "has very little information" on something, kusema tuu "you have very litle information" doesn't help a thing kama hiyo much more information huiweki humu!.

Mimi nimesema humu kama mwandishi, nimefanya appointment na Askofu Kakobe, nimemuhoji!, nimethibitisha "he has powers!", kitu nilichosema nimeshindwa kuthibitisha ni jee hizo "powers ni za Mungu au za mungu?!. Wewe mwenye more information you can give what you have or can counter kile kidogo nilichonacho kwa kuleta kikubwa!.

Ila pia naelewa kuwa kwa hawa viongozi wa dini wenye "powers", kuna baadhi ya wafuasi wao sio tuu ni wafuasi, au waumini, bali wanakuwa ni watupu hadi kuwaabudia wakifikiri huyu ndie Mungu kumbe ni mungu tuu!.

Naomba nikupe incident moja ya zamani ilitokea hapo kanisani!. "Muumini mmoja wa FGBF yule mama maarufa aliyekuwa akiishi Chang'ombe alipofariki, waumini walikusanyika hapo Kanisani asubuhi, na kutembea kwa miguu toka hapo Mwenge hadi makaburi ya Chang'ombe!, pale makaburini walifika wakiwa hoi, uchovu, vumbi ya njiani huku wamenyong'onyea fulani (sijui kama walikula!", Baba Askofu Kakobe aliwasili makaburini with brand new VX!, by then mawaziri wakitumia GX!, wabunge walikuwa hawana!. Amepiga suti ya ukweli (kama mtu hajui suti, hawezi kuijua suti ya ukweli na suti isiyo ya ukweli kama hizi za Mchina), na chini amevalia kiatu cheusi cha "snake skin!". Ukimuangalia Askofu na kumlinganisha na waumini wake, you can tell the diference and the contrast!. Nikamkumbuka yule Mchungaji Mwema!, Aliandamana na kondoo wake!, alifanana na Mchunga Kondoo!.

Tafuta lile neno "utawatambuaje!"

Pole tena!,

mama yangu na baba yangu hadi sasahivi wanasali kwa kakobe, wamesali pale miaka mingi sana. mimi nilipokuwa kijana sijaondoka kwa wazazi wangu nilisali kwa kakobe miaka mingi sana. ninamfahamu kakobe mno. kakobe ni mchungaji ambaye hajawahi kumiliki VX unayoitaja, gari ya kakobe kipindi kile cha huo msiba ilikuwa ni nissan patrol ile ya zamani, hata AC haina ni mkweche kwa kifupi, pamoja na kwamba ibada yake moja tu inaingiza milioni nyingi kwa siku, lakini hela zote anazitumia kwenye injili. kakobe ni mchungaji anayeishi maisha ya kimasikini hadi watoto wake wanaishi maisha ya kimasikini. nyumbani kwake kule uswahilini mwananyamala mtembelee kule usisikie vya kwenye magaazeti.

huo msiba unausema wazazi wangu walienda pia, na hawakutembea kwa mguu. ukienda pale kanisani pake, siku za ibada unaweza kukosa sehemu ya kupaki gari, watu wa pale si masikini sanaa kama unavyoamini wewe, hata wale wanawake usione wamevaa vilemba utashangaa kwao wana maisha mazuri kuliko hata wewe mwandishi wa habari za aina hii. kuna viongozi hata wa serikalini wengi tu pale na wafanya biashara wengi tu, ukichukulia watu wake wote hawanywi pombe, they know how to save na kuwekeza. nilivyokuwa naliona jina la PASCO humu nilikuwa naliheshimu kuwa mtu atakuwa msomi na mwenye uelewa na busara, but for this nimepata picha yako halisi huyu pasco ni wa namna gani.

kama watu mnamsema kwasababu ya kumponda kwenye kura ya katiba au umeme kupita pale (ambao kweli haukupita nenda kamwulize badra masoud na ngereja watakwambia). kuhuru bunge la katiba, ninamsapoti kabisa.

walokole tz they make something like 10 million population kwasasa. na hata wakristo wasio walokole yaani wale waanglikana, walutheran,wakatoliki n.k wanasali kotekote, wanasali makanisa yao na wanasali makanisa ya kilokole pia. vilevile, ni kweli kwamba wachungaji wa kilokole wote wana nguvu na sauti sana kwa waumini wao, waumini wa kilokole wanaweza kumsikiliza mchungaji wao ambaye anadharaulika kuliko hata rais wa nchi. vilevile walokole wanachukiwa sana kutokana na misimamo yao ya aina hii ya kiimani. na kwasababu they make a good substantial part of this society, walitakiwa kuwakilishwa kwenye bunge la katiba ili maslahi yao yasidhulumiwe.

mashehe wenye misimamo mikali kama KUNDECHA na RUGO sijui, wamewekwa kwenye bunge la katiba. kundecha ni pacha wa shehe ponda kwa wale wanaomfahamu. lakini walokole hata mmoja hawajawekwa. walitakiwa wawepo ili mambo yale ya kiimani wasuluhishane kwenye hicho kitengo chao cha usuluhishi na katiba iwe ya wote isiegemee upande mmoja kwasababu kundecha na wale wengine yakija masuala ya dini watataka mambo ya kiimani yao mengi yaingie lakin mambo yakiimani za kilokole walio zaidi ya milioni kumi yahayaingia kwasababu hawapo pale, na wale waliopo pale hawajui mambo ya msingi ya kidini au hata waliopo wapo tu ila si kama wametoka ulokoleni bali ni wabunge wa ccm.

ukitaka kuamini kuwa walokole ni wengi, na wachungaji wao wana nguvu kubwa, utaona mwakani kama wachungaji wa PCT wakiamua kupiga kampeni dhidi ya ccm, ndio utawajua. kumbuka kipindi cha kikwete walokole waliwaambia waumini wao kuwa kikwete ni chaguo la Mungu na walokole walimpa kura kikwete. wakiambiwa ccm ni adui wa Mungu hawataipigia kura hata mara moja.

walokole wamesahaulika, na ajabu zaidi rais kikwete anamsogelea mchungaji mmoja tu wa kilokole ambaye waumini wake hata alfu hamsini hawafiki, askofu gamanywa ambaye kanisa lake ni moja tu pale mbezi na kule mbagala, hana makanisa mikoani.

wachungaji wa PCT aliowaacha wana makanisa karibia kila kijiji cha tz, na analosema askofu dsm ndilo litakaloenda hadi kijijini kaabisa.
 
hao watu hukaa hapo mchana na usiku,kina mama kwa kina baba,kwa vijana.swali ni je,wanafanya kazi zao saa ngapi?na hao kina mama wanakaa na waume zao saa ngapi?ndio maana watu husema wafuasi wa kakobe ni masikini,sababu mtu analala na kushinda kanisani anafanya kazi saa ngapi?na kamwe hukuti wale wenye magari wanakesha hapo na kushinda hapo,ni wale pangu pakavu tia mchuzi kama mimi,ukimwona na kiatu soli imekaa upande,wanatia huruma kwa kweli,tena wengine ni vibibi!!!!!

hatumsemi vibaya,ila ni kweli serikali inabidi iingilie katui kama ilivyofanya kwa wale waumini wa kwenda ulaya bila passport kwa IMANI.kama ni haki yao wanafuatilia kwanini serikali isiwapatie ili kuokoa hawa wananchi na mateso???pale nje pana baridi na mbu wakali!!!!!!!

waumini wa kakobe ni maskini? magari yanayopaki pale jumapili ni ya nani? au kiwango cha mtaanzania maskini ni kumiliki magari kama waumini wa kakobe kama ni hivyo basi tanzania sasa ina maendeleo
 
KAKOBE is a disaster waiting to happen.
Leo akiwaambia waumini wake laleni barabarani watalala.Kunyweni sumu kuprotest watakunywa.
You only have to press Kakobe na athari zake utazipata kwa waumini wake.
Hiyo sehemu anayoipigania hana legal right ya aina yoyote kwa vile iko ndani ya hifadhi ya barabara.

pembeni kuna ghorofa la katoliki nalo lipo kwenye hifadhi ya barabara au?
 
Saa hizi ni Saa 8:39 za usiku!, yaani usiku wa manane, nimepita nje ya kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, la Askofu Zakaria Kakobe, nikushuhudia mamia ya waumini wake wamekaa kwenye viti na meza nje ya kanisa hilo huku limepambwa na disco lights zinazobadilika badilika rangi, kwa mgeni aweza dhania ni night club fulani.

QUOTE]

Ndugu yangu inawezekana kakobe akawa na nguvu ...lakini kwa kuwa yeye naye ni mwanadamu anaweza kutumia nguvu au ushawishi wake vibaya....hainiingii akilini kuona kakobe anapingana na serikali..bila sababu za msingi..

umeme unapita ndani ya hifadhi ya barabara ambayo inamilikiwa na TANROAD ..ambao wameshawapa kibali TANESCO...ndani ya hifadhi ya barabara ndipo panapohusu upanuzi wa barabara,mitaro,simu,gesi,umeme,maji etc...zote hizo ni huduma za jamii...ambazo ndugu kakobe hazipiti kwenye eneo la miliki yake....isitoshe hata mabango yake ameweka kwenye eneo la TANROADS tena bila kibali chochote...kimsingi kakobe hana haki yeyote pale zaidi nafikiri anazo hasira ....labda kwa kushindwa kuzuia kisheria wakati eneo lake lote la parking la kanisa alilojengaga barabarani lilipobomolewaga wakati wa kupisha upanuzi wa barabara ya Sam nujoma.........

serikali ya kikwete ina staha sana na huruma nadhani ...nafikiri angekuwa ni mkapa angembomolea kama alivomvunjia parking mwaka 2005.....na kakobe anautumia vibaya upole wa kikwete....

jambo lingine ambalo ni hatari kwa usalama ..linalotokea mara ya pili sasa ni la baadhi ya viongozi wa dini kama hawa kutumia misingi ya imani kuwachochea waumini wao kufanya jambo...tuliona wakati viongozi wa dini walipotumia imani kali ya kikristo kuingiza DECI na kuwafanya waamini kuwa DECI ni mkombozi aliyeletwa na YESU.....sasa kakobe anawafanya watu waache kulala makwao na wake zao au waume zao ...wanakesha wanaumwa na mbu kulinda eneo ambalo si la kwao kisheria ....nafikiri iikiendelea hivi badi anao uwezo wa kuwashawishi wajichome moto kama kibwetere[samahani kwa kufikia hapo]...lakini ndiko tunakoelekea kama tutaruhusu watu watumumie imani za waumini wau ..kuwatumikisha watakavyo!!!......

ni bora watu wa usalama wakawa makini na kuibuka kwa fundamenalism ...iwe kwenye christian everngelism au muslim ...zote ni sawa ...pamoja na kuwa ndugu zetu yao inatokuwa movements tofauti na ya wakristo ambayo mtu mmoja anaweza kuwakusanya watu kama mazoba na wakasahau kila kitu na kumfuata yeye....badala ya Mungu!!!
kakobe ni mchungaji mwenye matawi zaidi ya mia nne nchi nzima ana huduma ya kimataifa yenye makao makuu marekani tembelea www.bishopzacharykakobeinternationalministries.org na ana heshima kubwa kwa mataifa ya africa ulaya na america na kila alipofanya huduma Mungu wa kakobe alioonekana aina hii ndo watumishi wa Mungu wa kanisa la kwanza walivyokuwa kuanzia petro. paulo yohana japo hajawafikia lakini anajitahidi maana ishara hizi zitaambatana na wanaoniamini kwa jina langu watatoa pepo wataweka juu ya wagonjwa nao watapata afya kuna watu kwenu mnawaita maaskofu kata pepo tu hawezi kutoa ujue huyo hajaamini bado ila ni kipofu kama mshirika wake
 
mama yangu na baba yangu hadi sasahivi wanasali kwa kakobe, wamesali pale miaka mingi sana. mimi nilipokuwa kijana sijaondoka kwa wazazi wangu nilisali kwa kakobe miaka mingi sana. ninamfahamu kakobe mno. kakobe ni mchungaji ambaye hajawahi kumiliki VX unayoitaja, gari ya kakobe kipindi kile cha huo msiba ilikuwa ni nissan patrol ile ya zamani, hata AC haina ni mkweche kwa kifupi, pamoja na kwamba ibada yake moja tu inaingiza milioni nyingi kwa siku, lakini hela zote anazitumia kwenye injili. kakobe ni mchungaji anayeishi maisha ya kimasikini hadi watoto wake wanaishi maisha ya kimasikini. nyumbani kwake kule uswahilini mwananyamala mtembelee kule usisikie vya kwenye magaazeti.

huo msiba unausema wazazi wangu walienda pia, na hawakutembea kwa mguu. ukienda pale kanisani pake, siku za ibada unaweza kukosa sehemu ya kupaki gari, watu wa pale si masikini sanaa kama unavyoamini wewe, hata wale wanawake usione wamevaa vilemba utashangaa kwao wana maisha mazuri kuliko hata wewe mwandishi wa habari za aina hii. kuna viongozi hata wa serikalini wengi tu pale na wafanya biashara wengi tu, ukichukulia watu wake wote hawanywi pombe, they know how to save na kuwekeza. nilivyokuwa naliona jina la PASCO humu nilikuwa naliheshimu kuwa mtu atakuwa msomi na mwenye uelewa na busara, but for this nimepata picha yako halisi huyu pasco ni wa namna gani.

kama watu mnamsema kwasababu ya kumponda kwenye kura ya katiba au umeme kupita pale (ambao kweli haukupita nenda kamwulize badra masoud na ngereja watakwambia). kuhuru bunge la katiba, ninamsapoti kabisa.

walokole tz they make something like 10 million population kwasasa. na hata wakristo wasio walokole yaani wale waanglikana, walutheran,wakatoliki n.k wanasali kotekote, wanasali makanisa yao na wanasali makanisa ya kilokole pia. vilevile, ni kweli kwamba wachungaji wa kilokole wote wana nguvu na sauti sana kwa waumini wao, waumini wa kilokole wanaweza kumsikiliza mchungaji wao ambaye anadharaulika kuliko hata rais wa nchi. vilevile walokole wanachukiwa sana kutokana na misimamo yao ya aina hii ya kiimani. na kwasababu they make a good substantial part of this society, walitakiwa kuwakilishwa kwenye bunge la katiba ili maslahi yao yasidhulumiwe.

mashehe wenye misimamo mikali kama KUNDECHA na RUGO sijui, wamewekwa kwenye bunge la katiba. kundecha ni pacha wa shehe ponda kwa wale wanaomfahamu. lakini walokole hata mmoja hawajawekwa. walitakiwa wawepo ili mambo yale ya kiimani wasuluhishane kwenye hicho kitengo chao cha usuluhishi na katiba iwe ya wote isiegemee upande mmoja kwasababu kundecha na wale wengine yakija masuala ya dini watataka mambo ya kiimani yao mengi yaingie lakin mambo yakiimani za kilokole walio zaidi ya milioni kumi yahayaingia kwasababu hawapo pale, na wale waliopo pale hawajui mambo ya msingi ya kidini au hata waliopo wapo tu ila si kama wametoka ulokoleni bali ni wabunge wa ccm.

ukitaka kuamini kuwa walokole ni wengi, na wachungaji wao wana nguvu kubwa, utaona mwakani kama wachungaji wa PCT wakiamua kupiga kampeni dhidi ya ccm, ndio utawajua. kumbuka kipindi cha kikwete walokole waliwaambia waumini wao kuwa kikwete ni chaguo la Mungu na walokole walimpa kura kikwete. wakiambiwa ccm ni adui wa Mungu hawataipigia kura hata mara moja.

walokole wamesahaulika, na ajabu zaidi rais kikwete anamsogelea mchungaji mmoja tu wa kilokole ambaye waumini wake hata alfu hamsini hawafiki, askofu gamanywa ambaye kanisa lake ni moja tu pale mbezi na kule mbagala, hana makanisa mikoani.

wachungaji wa PCT aliowaacha wana makanisa karibia kila kijiji cha tz, na analosema askofu dsm ndilo litakaloenda hadi kijijini kaabisa.
Mkuu Hute, kwanza asante kwa kueleza unachokijua kumhusu Askofu Kakobe na sipingani na wewe, pia nakiri kukosea aina ya gari kweli ni Nissan Patrol au Safari, ilionekana kama mpya, labda kutokana na matunzo!. Pia nakiri wengi wa waumini wa kanisa la Kakobe ni matajiri na wana magari, ila wengi zaidi hawana magari na kwenye ule msiba walitembea kwa miguu!.

Naomba nisizidi kumsakama huyu sijui kama ni man of God or man of god!, naomba niwaache wenye imani zenu!, japo sijafanya utafiti rasmi, ila Badra na Ngeleja are reachable!, kama ni kweli umeme pale haupiti, then ndio nitazidi kutishika na kuogopa, kwa sababu Mungu alisisitiza mpeni Kaizari yaliyo ya Kaizari na mpeni Mungu, yaliyo ya Kimungu, umeme ni ya Kaizari!, sababu za kuuzuia usipite hapo, zilikuwa genuine enzi za analojia, sasa ni digitali, hakuna tena interference, sasa huyu ni Mungu kweli anazuia umeme usipite kuwahudumia mamia kwa maelfu ya watu for no apparent justified reasons?!. I doubt!.

Mambo ya katiba ni mambo ya Kaizari, siamini kama ni kweli ni Mungu ndie aliyemweleza Kakobe maneno ya unabii kwenye ule waraka wa vitisho kwa JK, naamini Kakobe atakuwa kaambiwa na mungu, hivyo hakuna chochote kitakacho tokea!, ila pia kama ni kweli umeme pale haupiti, then serikali inazijua nguvu za mungu wa Kakobe, hivyo soon watamuungamia vinginevyo nizo nguvu zilizozuia umeme usipite, zinaweza kukisambaratisha Chama Cha Mapinduzi!.

Zishindwe!.

Pasco
 
kakobe ni mchungaji mwenye matawi zaidi ya mia nne nchi nzima ana huduma ya kimataifa yenye makao makuu marekani tembelea www.bishopzacharykakobeinternationalministries.org na ana heshima kubwa kwa mataifa ya africa ulaya na america na kila alipofanya huduma Mungu wa kakobe alioonekana aina hii ndo watumishi wa Mungu wa kanisa la kwanza walivyokuwa kuanzia petro. paulo yohana japo hajawafikia lakini anajitahidi maana ishara hizi zitaambatana na wanaoniamini kwa jina langu watatoa pepo wataweka juu ya wagonjwa nao watapata afya kuna watu kwenu mnawaita maaskofu kata pepo tu hawezi kutoa ujue huyo hajaamini bado ila ni kipofu kama mshirika wake
Mkuu Doma, hakuna mashaka kuhusu umaarufu wa Akafu Kakobe na haswa anapokuwa nje ya nchi, kwani nilishuhudia kwenye TV, ile ziara yake ya Rwana na Burundi, swali linabaki jee hizi ni nguvu za Mungu au mungu?!.
Pasco
 
Kama kuna yoyote ambaye ni muumini ama aliwahi kuwa muumini akatusaidia sisi akina Tomaso, kwa kutupa ushuhuda wa msingi wa nguvu za Baba Askofu Zakaria Kakobe ili nasi tumuaminiye na tumfuate, vinginevyo huyu ni mtu mwenye nguvu za ajabu na siyo wa kupuuzwa.NB. Mode, hii siyo ya dini na imani, ni ya politics of religion.

Lowassa nadhani anamtambua T.B. Joshua who is no difference na Kakobe. Think before you ink Pasco
 
Last edited by a moderator:
mimi huwa sipendi kuchanganya "imani za watu" na " hisia zangu buinafsi" ,japo natamani KUPROVE kama mf. TB Joshua ni mtumishi wa MUNGU au wa mungu, hivi kuna njia ya kuprove?
 
Back
Top Bottom