Askofu Kakobe Asipuuzwe: Ni kama David Koresh na Camp Davidians! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu Kakobe Asipuuzwe: Ni kama David Koresh na Camp Davidians!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Jan 11, 2010.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,572
  Likes Received: 18,393
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,
  Saa hizi ni Saa 8:39 za usiku!, yaani usiku wa manane, nimepita nje ya kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, la Askofu Zakaria Kakobe, nikashuhudia mamia ya waumini wake wamekaa kwenye viti na meza nje ya kanisa hilo huku limepambwa na disco lights zinazobadilika badilika rangi, kwa mgeni aweza dhania ni night club fulani.

  Nimeshauri asipuuzwe kwa sababu mimi ni mmoja ambaye ninatoa ushuhuda jamaa ana nguvu, yaani he has powers! Niliwahi fanya nae mahojiano miaka ya nyuma, nikamuuliza hiyo daraja ya Uaskofu alipewa na nani?. Alijibu na Mungu mwenyewe!. Nikauliza kuhusu tuhuma mbalimbali zinatupwa kwake na watu wa mataifa, zikiwepo yeye kuwa tajiri wakati waumini wake wako kwenye umasikini uliotopea, kuhusu Mkewe kuwa ndio Mweka hazina, kuhusu kama hayupo inawekwa kanda kuhubiri.

  Na swali la mwisho nilimuuliza kuhusu ukweli kuwa waumini wake wanavuliwa dhahabu na anaziteketeza kwa moto, nikamuomba angalau anionyeshe lilipo hilo tanuru nishuhudie smelted gold deposits kwa macho yangu mwenyewe.

  Askofu alinyamaza, akaniangalia machoni kwa kunikazia macho kama anahasira fulani, nami nikajisikia baridi ya ghafla nikataka kuanza kutetemeka na kusikia kizunguzungu ile staili ambayo hatimaye watu huanguka chini. Nikajishika imara kwenye kiti, nikwamwambia Askofu, nimeyaondoa maswali yangu yote, hana haja ya kuyajibu tena!. End of interview.

  Huu ni uthibitisho tosha kuwa Askofu Zakaria Kakobe ananguvu fulani, hivyo sio wa kupuuzwa.

  Kitendo cha kuwaona waumini wake kwa mamia, wanalala macho usiku kucha kwa kumsikiliza Askofu wao akiwaamuru kuhakikisha wanaipinga serikali in the name of God, ninaamini hao walala nje, wanalala macho hapo nje kwa imani 100 kwa 100 kuwa huko nako ni kumtumikia Mungu Baba na sio kumtumikia binadamu mwenye jina la Askofu.

  Kwa lugha nyingine, Nguvu za Askofu Kakobe zimewahypnotize waumini wake kwa kiwango cha juu, kiasi kwamba, chochote atakachowaambia wafanye, watafanya, ndivyo ilivyokuwa kwa David Koresh na wafuasi wake wa Camp Davidians na Askofu Kibwetere na wafuasi wake ambao mwisho wao wote waliishia kuteketezwa kwa moto na kujilipua kwa mabomu kwa ahadi ya safari ya mbinguni kwenye uzima wa milele, imewadia!.

  Kama kuna yoyote ambaye ni muumini ama aliwahi kuwa muumini akatusaidia sisi akina Tomaso, kwa kutupa ushuhuda wa msingi wa nguvu za Baba Askofu Zakaria Kakobe kama ni za Mwanga au za giza ili nasi tumuaminiye na tumfuate, vinginevyo huyu ni mtu mwenye nguvu za ajabu na siyo wa kupuuzwa hata kidogo!.

  David Koresh wa Camp Davidian alipuuzwa hivi hivi, Joseph Kibweteere nae alipuuzwa hivi hivi, kilichofuata sote tunakijua.

  NB. Mode, hii siyo ya dini na imani, ni ya politics of religion.

  Paskali
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,345
  Likes Received: 19,527
  Trophy Points: 280
  Ukiwa na imani kama mfano wa punje ya haradani unaweza kuuhamisha hata mlima. believe me.usimfananishe kakobe na kibwetere.
   
 3. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  why do people subscribe to things like this. The man preys on people with no hope and difficult troubles in their lives. Shameful really.
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Huu ndio udaku?? Mi nilifikiri una jipya ? We kama hukunywa chai asubuhi, glucose levels zipo chini ukataka kuanguka unataka kumpa Kakobe mdhamana wa afya yako duni??
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,572
  Likes Received: 18,393
  Trophy Points: 280
  Ni punje ya haradali-Simfananishi Kakobe na Kibwetere nimezungumzia the powers within him, kuwalaza waumini wake nje in the name of God, hivi hao waumini wanaamini kutekeleza wito wa mkuu wao kulala nje kwao ni sehemu ya ibada ama just blind faith?.

  Ni hapo kwenye blind faith ilipocapitalize Coresh na Kibwetere.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,572
  Likes Received: 18,393
  Trophy Points: 280
  Ndio maana nimawashuhudia has powers, ni kweli 'The man preys on people with no hope and difficult troubles in their lives' ndio maana nikauliza huko kuwalaza macho hapo nje ni sehemu ya Ibada?.
   
 7. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,657
  Likes Received: 21,875
  Trophy Points: 280
  Kama kila akifanyacho anatumwa na Mungu wake, basi 1995 Mungu wake alishindwa kumuweka madarakani Mrema maana alizunguka na kutuambia "Huyu ndiye yeye yule anayetakiwa"
  Naungana nawe Mkuu Pasco, Kakobe asipuuzwe kabla hatujayaona makubwa na tukabaki kujutia yakitokea kama kawaida yetu ya kupuuzia ilivyo.
   
 8. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Pasco, hayo ni majungu bwana. Ila sikushangai, Yesu mwenyewe aliambiwa anatoa Pepo kwa nguvu ze Belzebuli, itakuwa Kakobe? Umepita makanisa mangapi ukakuta hawapo makanisani time hizo? Kama haumuamini Kakobe, mwache akae, nyamaza kimya enedelea na kazi zako.
   
 9. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,657
  Likes Received: 21,875
  Trophy Points: 280
  Rudi mwanzo na msome Pasco vizuri kabla ya kumjibu. Usiweke mbele hisia zako katika hoja.
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,149
  Trophy Points: 280
  huyo ndiyo kakone bwana.
   
 11. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #11
  Jan 11, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  huyu mzee ''kwa mtizamo wangu'' NINASHAURI ASIPUUZWE!the man is decent,let's be honest people
   
 12. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  ooops....! i have been kimya to some ishuz but this ''MADE A SNAKE COME OUT''
  mleta hoja amejaribu kwa upeo wake kueleza jinsi mtu huyu KAKOBE alivyo na nguvu....! amejaribu pia kuwafananisha na watu anaowajua yeye au watu ambao public itawajua kwa urahisi.
  all in all KAKOBE has virtues/powers from above,is a charismatic leader and a follower of JESUS THE CHRIST......!
  Yale yafanywayo kwake laiti yangefanywa kwa WATU WA MADHEHEBU FULANI nadhani tunge-expirience something else.KUVUNJIWA KANISA,KUAMBIWA ANAKUSANYA DHAHABU ZA WATU NA MENGINEYO TELE WA TELE.....!
  Ukiona simba kalowana usidhani ni paka.....all have been done to this man naye amejaribu kuelezea malalamiko yake kwa maneno tu (diplomatic,peacefully,dialogue) je mtu kama huyu akisema SASA BASI inakuwaje......YOUUUUUUU DECISION MAKERS WATCH OUT.........!
  We see some of your decisions yanavyowaumiza watu e.g MAJEMBE SAGA e.t.c
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Jan 11, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Wewe bwana wacha kupotosha watu humu. Kwani mbona watu wa dini nyingine hukutanika kwa nia mbalimbali na hamuwasemi ??
   
 14. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #14
  Jan 11, 2010
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Naungana na Pasco kuwa tuwe wanagalifu na Mtu kama Kakaobe. waumini wake wanaweza kulala mbele ya buldoza ili wafe kuzuia ujenzi wa laini za umeme.
   
 15. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #15
  Jan 11, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  KAKOBE is a disaster waiting to happen.
  Leo akiwaambia waumini wake laleni barabarani watalala.Kunyweni sumu kuprotest watakunywa.
  You only have to press Kakobe na athari zake utazipata kwa waumini wake.
  Hiyo sehemu anayoipigania hana legal right ya aina yoyote kwa vile iko ndani ya hifadhi ya barabara.
   
 16. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #16
  Jan 11, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Watu humu mnataka kuimba kiitikio cha wimbo hata msiojua. Hivi kuandamana na kusimamia jambo unaloliamini kuna ubaya gani?? Hivi wale wanaoprotest jambo fulani ni lazima wawe wamekuwa brain-washed??
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Jan 11, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Paco uko right kabisa, huyu mtu anahitaji very close watch. na serikali iache kuchanganya vitu, ifuate taratibu za sheria
   
 18. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #18
  Jan 11, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ulichofulia ni kumwangalia usoni. Ulipaswa kuangalia moyo wake. Ungemfaidi zaidi kama ungemuuliza Mungu kibali chake kwanza ili kumvaa mtu huyo na kumuuliza kwa ujasiri. Hakukujibu lakini maswali yako yalikuwa ya kimsingi kabisa ambayo ni kweli yanasemwa nje. Ungekuja nje na majibu ya kuifaa jamii kwa sana. Lakini huenda wewe ulishaijenga nguvu yake mapema, hata alipokuangalia labda hizo "nguvu" alizo nazo zilikukoroga zaidi mpaka ukaamua kufuta maswali. Kwa nini ulifuta? Ulikuwa unamtania?

  Sasa angekuja Obama ukamhoji na makachero wake wana silaha zilizochanganyikiwa si ndio ungezimia kabisa?

  Nguvu ofcourse lazima anazo, akini ni nguvu gani? Hata Elia alipokutana na wachawi wa Nebukadneza walitisha kwa mbwembwe zao, lakini kwa kuwa alikuwa anajua anamtumikia nani alidiriki kuwadhihaki wachawi wale, mpaka watu wakakiri Mungu wak Elia ni zaidi. Tumeambiwa tuzijaribu kila roho, maana sio zote ni za Mngu zijaposema kazituma Mungu, kwa wengine dini ni biashara safi sana, ndio maana utawala muhimu inashika familia - mtunza pesa mama, msemaji mkuu baba, mkuu wa Kanisa baba, n'k.

  Leka
   
 19. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #19
  Jan 11, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280
   
 20. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #20
  Jan 11, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Kaka niamini mimi, lazima Tanesco wafanye mazungumzo na hawa waumini na wasithubutu kujaribu kupitisha nyaya hizo bila ridhaa yao, kama hujaona vita kali jaribu kucheza na imani ya watu.

  Hata mi nilipita nikaona wanalala nje nafikiri wana zaidi ya wiki sasa, mtu anayelala nje yupo tayari kwa lolote mkuu

  Tanesco ikijaribu kufanya kazi yao kwa nguvu ya serikali basi yatakuwa ya mwembechai mengine.

  Ni kweli kakobe ana nguvu - we kama unabisha nenda kaongee na yeye leo utamkuta pale then uje utupatie update.
   
Loading...